23/09/2022
Anasema Mmoja wa wachawi..
Nilikuwa nawatuma Majini kwa watu kuwaroga..
Baadhi yao niliwatumia Majini lakini Wanarudi na kusema Tunaskia Sauti zao lakini Hatuwaoni..
Baadhi yao niliwatumia Majini wanarudi wakisema Tumewaona lakini wametupotelea..
Wengine niliwatumia Majini lakini Wanarudi wakisema hawakuwaona..
Kisha nikawatumia Jini Muradah na hao wana Nguvu kuliko wale niliowatuma Kabla, Lakini wao pia wanarudi na kusema hawajawapata waliokusudiwa..
Kisha Nikawatumia Jini Ifreet na wao ni Majini wenye Nguvu, lakini wao pia wanarudi wakisema tumeenda Mashariki na Magharibi ya Ardhi lakini hatukumpata Huyo Mtu..
Nikawauliza Vipi hamujampata na yeye Yuko Nyumbani kwake au kazini kwake mahali kadhaa na Kadhaa wanasema tumeenda hatujampata..
Alipotubia Huyu Mchawi Anasema "Nikajuwa watu wako Tofauti Kulingana na Kinga zao..
Kuna wale ambao hawana Kinga hao ni Rahisi kuwaingia..
Kuna wale ambao wanajilinda kwa Dua lakini Mara nyingine wanasahau kuzisoma na Swala zao Mara wanaghafilika Hawa ndio wale Majini wanaskia sauti zao lakini Hawawaoni..
Wale ambao wanajilinda kwa Dua na Ibada kila wakati Hawa ndio wale Majini hawawezi kuwaona kabisa hata K**a wataishi Kati yao..
"Unaposoma Qur'an tunajaalia Baina yako na Baina ya wale ambao Hawaamini Akheerah Hijaab iliositiriwa (Kizuwizi)..
Qur'an Duaa Sadaka Na Ibada Za Lazima ndio Kinga yako Ndugu yangu Muislamu...
Kujiepusha Na Maasia na Kumridhisha Allah Ndio Kinga yako Ndugu yangu...