08/09/2025
Nakumbuka ilikua siku ya ijumaa tarehe 19/7/2024, niliakwa pale WAA PRIMARY, kulikua na uzinduzi wa vyoo, hio ndo siku ambayo ndugu yangu Rashid Abdalla aliniuliza swali moja gumu sana, “Beka Unataka Nikusaidie Kitu Gani Kwenye Hii Career Yako Ya Usanii?” walai nilikaa kimya najichekea k**a zuzu😂😂😂mdomo wangu ulikua k**a umetiwa zege, hadi ikabidi yeye mwenyewe ndo anipe options nichague,akaniambia ukitaka naeza kukununulia camera uendeleze sanaa yako, ama naeza kukutaftia nafasi katika vipindi vyetu, nikawaza hii camera hata nikipewa sidhani k**a inamsaada sana kwangu mana kazi zangu nyingi huwa nafanyaga na simu, faster nkachagua option two, nikamwambia bro k**a ikitokea nafasi katika hivyo vipindi vyenu ukinipa walai ntashukuru, huo utakua msaada mkubwa sana kwangu,
Subra nimekua nayo mkwa mda mrefu lakini alhamdulillah here i am at Jiffy Pictures
Brother ameitimiza ile ahadi yake na soon mtaniona “CITIZEN”
Rashid Abdalla walai nakosa hata neno la pamoja la kutoa hizi shukran zangu kwako, ila ntasema tu ahsante kwa kunishika mkono mdogo wako, roho yako ni ya kipekee sana,nakosa hata mtu wa kukufananisha nae,Inshallah Mungu azidi kukumiminia baraka tele na akufanyie wepesi kwenye kila harakati zako za kila siku, binafsi nimeshukuru kwa hii nafasi na nakuahidi inshallah ntapiga kazi k**a punda kiufup HUKO CITIZEN KUTAWAKA MOTO🔥🔥🔥
KWALE TO THE WORLD
Juma Shibe Nurah Yusuf