31/07/2025
Jamani Kesi za defilement hua zinahuzunisha sana.
Kupata mtoto wa miaka sita ambaye amedhulumiwa kwa muda na mtu miaka 40+ ni jambo la kutamausha.
But mostly watoto wanahitaji ukaribu na baba zao pia not just their mothers.
I say it again here that there is a very crucial role for you as the father pale nyumbani beyond provision.
Mtoto wa k**e anakuhitaji sana kumkinga dhidi ya unyanyasaji wa kingono kupitia;
✅️Kuwa chanzo cha heshima na upendo.
👉Mthamini, msikilize na umpe nafasi ya kujieleza.
Akikuona unamheshimu na yeye mwenyewe ajue kujiheshimu nyumbani atajua anavyofaa kutendewa duniani.
✅️Mfundishe kujiamini na Kujilinda.
Mpe ujasiri wa kuripoti vitisho hata k**a ni from close people.
👉Mostly watoto hudhulumiwa na wanaume na wewe mwenyewe unaweza kujua mbinu nyingi wanaume wanazoeza kutumia to lure a girl in to s*x. Mjengee uwezo wa kutambua mbinu hizi za kisiri na za kumnyanyasa.
Mshauri kusema wazi ikiwa jambo linamfanya askie vibaya.
✅️Be a role model wa Tabia nzuri
Epuka lugha ya mzaha au ya kudhalilisha mbele ya yule binti yako.
Jiheshimu, heshimu wanawake pale nyumbani na wengine huko nje.
✅️Linda mazingira ya binti yako
Fahamu watu anaotangamana nao kuanzia
Walimu, jamaa na hata marafiki.
ANAYEDHULUMU MTOTO WAKO HUA NI MTU WA KARIBU KABISA MOSTLY.
Chukua hatua mapema ukiona ishara zisizo za kawaida.
Weka mawasiliano wazi, awe huru kukusmbia kitu chochote.
✅️Fanya Mazungumzo ya mapema kuhusu mipaka.
Yes, boundaries!
Usiogope kuongea naye kuhusu;
👉mipaka ya mwili wake
👉Ruhusa ya kusema hapana kwa mguso wowote asiopenda.
👉Tofauti kati ya mguso salama na wa hatari.
💙💙💙Kuwa baba si tu kumpatia mtoto mahitaji ya kimaisha bali pia ni kumlinda, kumwelekeza, na kumpa ujasiri wa kusema "HAPANA" pale anapohisi hatari.
Remember anayedhulumu mtoto wako mara nyingi ni mtu wa karibu, inawezekana ikawa unakula naye, na kusalimiana naye, anakuja kwako na kutoka! TUWE MAKINI.