20/09/2025
MASOMO YA MISA YA JUMAPILI
DOMINIKA YA ISHIRINI NA TANO KATIKA KIPINDI CHA KAWAIDA MWAKA C
SEPTEMBA 21 2025
RANGI YA LITURUJIA: KIJANI💚
MADA YA DOMINIKA:
JINSI YA KUWA MSIMAMIZI MWEREVU WA MALI ZA ULIMWENGU HUU.
_Je! Tunaweza kuwaita matajiri wa wakati wa Amosi ni werevu? Walikuwa matajiri kwa kudanganya maskini, hawakuheshimu "'siku takatifu" na walijishughulisha na tamaa zao za ubinafsi. Katika macho ya watu hakika walikuwa na werevu, lakini machoni pa Mungu walijiangamiza. Hii ndio tunafundishwa na somo la kwanza. Yesu anatuambia katika Injili kuwa sisi ni "werevu" ikiwa tunatumia mali za ulimwengu huu kusaidia wengine. Kwa njia hii tunapata kitu cha kipekee chenye thamani, urafiki na maskini. Kuelewa ukweli huu, ambao ni mgumu sana kukubali, tunahitaji sala. Paulo anatuambia hili katika somo la pili.
ANTIFONA YA KUINGIA*
_Mimi ndimi wokovu wa watu, asema Bwana. Katika shida yoyote wataniita, nami nitawasikiliza; nami nitakuwa Bwana wao hata milele._
KOLEKTA
Ee Mungu, uliyaweka maagizo yote ya sheria takatifu katika upendo kwako na kwa jirani: utujalie kuzishika amri zako, tupate kustahili kuufikia uzima wa milele. Kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo Mwanao...
SOMO LA KWANZA
Amosi 8:4-7
Bwana alinena dhidi yao wanaonunua watu maskini kwa fedha.
Somo katika kitabu cha Nabii Amosi
Sikilizeni haya, enyi mnaomkanyaga mnyonge, na kuwaangamiza watu maskini wa nchi; ninyi mnaosema: Sikukuu ya mwezi mwandamo itakwisha wakati gani, tupate kuuza ngano? Nayo siku ya Sabato, tupate kufungua ghala ya ngano? Tutapunguza vipimo, tutapandisha bei, tutageuza mizani ziwe za uongo! tutauza hata makapi ya ngano, tupate kuwanunua watu maskini kwa fedha, na wanyonge kwa jozi ya viatu! Bwana ameapa kwa utukufu wa Yakobo: Hakika sitasahau kamwe matendo yao.
Neno la Bwana.
ZABURI YA KUITIKIZANA
Zaburi 1 13:1-2,4-6,7-8(K 1a na 7a)
K. Msifuni Bwana, humwinua mnyonge kutoka mavumbini.
au: Aleluya.
Enyi watumishi wa Bwana, sifuni,
lisifuni jina la Bwana.
Jina la Bwana litukuzwe / tangu sasa na hata milele.
K.
Bwana ni mkuu juu ya mataifa yote;
utukufu wa Mungu ni juu ya mbingu.
Ni nani aliye k**a Bwana,
Mungu wetu, aketiye juu kabisa,
ainamaye atazame chini mbinguni na duniani?
K.
Humwinua mnyonge kutoka mavumbini,
kutoka jalalani humpandisha maskini,
amketishe pamoja na wakuu,
pamoja na wakuu wa watu wake.
K.
SOMO LA PILI
1Timotheo 2:1-8
Maombezi yatolewe kwa ajili ya watu wote kwa Mungu, ambaye ataka watu wote waokolewe.
Somo katika barua ya kwanza ya Mtakatifu Paulo kwa Timotheo.
Mpendwa: Kwanza kabisa ninayowaomba hasa ndiyo, dua na sala, maombezi na shukrani zitolewe kwa ajili ya watu wote, kwa ajili ya wafalme na wote wenye mamlaka, tupate raha na utulivu kwa kuishi maisha ya uchaji wa Mungu na ya mwenendo mwema. Hayo ni mema, tena yampendeza Mungu, mwokozi wetu, ambaye anataka watu wote waokolewe, na watambue yaliyo kweli. Kwa maana kuna Mungu mmoja, na mpatanishi baina ya Mungu na
wanadamu ni mmoja, ndiye mwanadamu Kristo Yesu, huyo alijitoa mwenyewe kuwa fidia kwa ajili ya watu wote. Ndio ushuhuda nyakati zake. Kwa hiyo nimewekwa mimi niwe mtangazaji na mtume, tena mwalimu wa mataifa katika imani na ukweli. Hayo maneno yangu ni kweli, si uongo. Kila mahali mnaposali napenda wanaune wainue mikono kwa utakatifu, si kwa hasira na ubishi.
Neno la Bwana.....
SHANGILIO LA INJILI
2 Wakorintho 8:9
Aleluya. Aleluya.
ljapokuwa Yesu Kristo alikuwa tajiri, alijifanya fukara kwa ajili yenu, ili ninyi mpate kutajirika kwa ufukara wake.
INJILI
Luka 16:1-13
_Hamwezi kumtumikia Mungu na fedha._
Somo la Injili takatifu ilivyoandikwa na Luka..
Wakati ule: Yesu aliwaambia wafuasi wake, Tajiri mmoja alikuwa na karani naye alish*takiwa kwake kwamba anatapanya mali zake. Akamwita, akamwambia, Je, nasikia nini juu yako? Toa hesabu ya ukarani wako, kwa maana huwezi kuwa karani tena, Karani huyo akasema moyoni mwake, 'Nifanyeje? Maana, Bwana wangu ananiachisha kazi ya ukarani. Kulima, siwezi, na kuomba k**a maskini naona haya. Najua la kufanya, ili baada ya kutolewa katika ukarani, wanikaribishe nyumbani kwao. Akawaita wadeni wa bwana wake mmoja mmoja, akamwambia wa kwanza, 'Una deni gani kwa bwana wangu? Naye akajibu, Mapipa mia ya mafuta. Akamwambia, Twaa hati yako ya deni; kaa upesi, andika, hamsini. Kisha akamwambia mwingine, Nawe una deni gani? Akasema, Mifuko mia ya ngano.' Akamwambia, Twaa hati yako ya deni, andika, themanini. Bwana akamsifu karani mdanganyifu kwa sababu alifanya werevu. Maana wana wa dunia hii ni werevu katika mahusiano yao kuliko wana wa mwanga. Nami nawaambieni, jifanyieni rafiki kwa mali inayoharibika, ili mnapoishiwa nayo wawapokee katika makao ya milele. Aliye mwaminifu kwa mambo madogo ni mwaminifu pia kwa mambo makubwa; kadhalika asiye mwaminifu kwa mambo madogo, si mwaminifu kwa mambo makubwa. Basi, k**a hamwi waaminifu kwa mali isiyo haki, nani atawakabidhi mali ya kweli? Na k**a hamwi waaminifu kwa mali ya mwingine, nani atawapa yenu wenyewe? Hakuna mtumishi awezaye kutumikia mabwana wawili, ama atamchukia wa kwanza na kumpenda wa pili au atamjali wa kwanza na kumdharau mwingine. Hamwezi
kumtumikia Mungu na fedha.
Injili ya Bwana.... Sifa kwako Ee Kristo