07/04/2025
BEKI wa kati wa Real Madrid, Antonio Rudiger, amemtaja mshambuliaji wa Atletico Madrid, Julian Alvarez, k**a mshambuliaji mgumu zaidi kuwahi kumkabili kwenye La Liga.
-
Akihojiwa na Alkass Sports, Rudiger alijibu moja kwa moja:
👉🏽 “Julian Alvarez wa Atletico Madrid.”
-
Alvarez, mshindi wa Kombe la Dunia 2022 na timu ya taifa ya Argentina, alijiunga na Atletico Madrid msimu uliopita akitokea Manchester City. Akiwa na umri wa miaka 25. Straika huyo ameanza vyema maisha yake nchini Hispania kwa kufunga mabao 23 na kutoa pasi za mwisho 5 katika mechi 46 kwenye mashindano yote.
-
Katika La Liga pekee, amefunga mabao 11 na kusaidia mawili katika mechi 29, huku Atletico Madrid wakiwa nafasi ya tatu kwenye msimamo, wakiwa na pointi 57, tisa nyuma ya vinara Barcelona.
-
Alvarez yupo kwenye kiwango kizuri akiwa amefunga mabao sita katika mechi zake sita za mwisho za La Liga, ikiwemo bao katika sare ya 1-1 dhidi ya Real Madrid kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu mwezi Februari.
-
Kabla ya kujiunga na Atletico, Alvarez aliisaidia Manchester City kwa mabao 36 na pasi 17 za mabao katika mechi 103, akishinda mataji mawili ya EPL na yale mataji matatu ya kihistoria (treble) msimu wa 2022-23.
-
Kwa upande mwingine, Rudiger alijiunga na Real Madrid akitokea Chelsea majira ya joto 2022. Tangu wakati huo, amecheza karibu mechi 150, akifunga mabao 7 na kutoa pasi 3, huku akishinda La Liga na Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu uliopita chini ya kocha Carlo Ancelotti.
-