02/08/2025
πππππ πππ πππ πππππππ πππππππ
Happy New month wakuu! Weka Like tuanze mwezi na 10k Likes kwa hii post.
ππππ π
Haya! Hii ni ya Monday
Meanwhile,Neema aliwaleta akina Mark pahali aliwaleta na akawaambia watakua wanakaa hapa..Mark akamwambia hatuezi toshea wote hapa lakini Naomi alimwambia relax,usiwe na haraka alafu for your information kaa ukijua iam your new boss...Mark akamuuliza unamaanisha? Naomi akamwambia nilibuy farm na hii yote nilifanya ju ya Neema π€£π€£π€£Mark anaona that deal is too good to be good.
Eddy na yeye,aliitwa na partner wake,akamwambia sikiza Eddy, shares zako zoote unanipea,so kuanzia leo hauna anything..Eddy akamuuliza unamaanisha,this is my restaurant lakini jamaa akampea papers akamwambia ni uweke tu sahihi..Eddy alijam,akataka kugonga huyu jama lakini punde si punde, cousin wa Karen akafika akiwa na rungu,akaambia Eddy,ni ufanye venye umeambiwa ama kaumaneπ€£π€£π€£
Eddy,akidhani ni mchezo,aligongwa,mbaya mbovu.
Rachael alikuja akapata Jojo na Amani wakiongea hapo akawauliza mnadu? Amani akamwambia its my wife and I having a talk..Rachael akamuuliza ooh,so its now your wife? Amani akamwambia eeh,huyu ni my wife sasa πππ
Woiye Eddy,mwanaume ametandikwa,mbaya mbovu,kisha akaambiwa sikiza,tusikie ati umeenda polisi utaona moto. Eddy ashaambiwa kila kitu venye kulienda na venye hawa wako related na Karen.
Mark alikuja akamuita Neema akamuuliza babe,do you trust Naomi? Neema akamwambia lets give her a benefit of doubt tuone. Naomi alikuja na offer ingine akaambia akina Mark na Neema wawe k**a business partners. Yani Neema hawaamini venye Naomi amekua mzuri haraka hivi lakini wachunge,hakuna uzuri hapa,Naomi anataka kuwatandika bila wao kujua.
Kumbe Rachael alikuja kutafuta Isaac,anataka some money. Isaac akamuuliza so unataka nifanye nini? Rachael akamwambia nataka pesa,ama ni wewe ulichoma? Isaac akamwambia acha ujinga,iam not involved..na k**a mshaanza kusuffer then iam happy. Rachael alimwambia nipe pesa zangu,Isaac akamwambia sikiza, nilikufanyia your dirty work so hauna right ya kuniitisha anything wewe mwanamke ππRachael,akarukwa!
ππππ π
Rachael anacomplain ati kanyumba huku ni kadogo...Babu yeye anampea tu Ian moyo anamwambia usijali hizi mashida ni kukupa nguvu. Babu aliuliza Jojo hali ya Amani na Jojo akamwambia my husband ako sawa amelala..Rachael akamwambia hata maybe anaeza kufa ju ya suffocation ya hii kanyumba kadogo πππ
Naomi alikuja akaambia Neema wafanye renovation ya hii hotel. Mark akamwambia shida pesa tutatoa wapi za renovation? Naomi akamwambia msiwe na wasiwasi.I g*t you. So Naomi akamtuma Mark pahali kupick something ndio arudi so Mark akaambia Neema acha akimbie anarudi.
Lakini cheki,wakati Mark ametoka,kuenda pahali Naomi amemtuma,Naomi on other side akatext mtu fulani,akamwambia "he is out in a few,make it a clean shot and don't miss it"..Hii ina maana,Naomi hajatuma Mark kuchukua anything,amemtuma kuenda kuuliwa,wah! Makosa.
Sharon na yeye,wakiwa nyumbani,Dancan alikuja,akawaambia mnajuaje,kuna jamaa nimepea zile pesa lakini nampigia simu hashiki. Ilikua aende kuniwekea kwa bank lakini hashiki simu tangu asubuhi. Dancan ashaconiwa tena..Sharon kusikia hivyo,alipiga nduru moja safi,mnbaya mbovu πππPesa za haramu hazisaidii mtu. Sharon hadi anashindwa mtu mmoja anaeza kuaje mjinga hivi πππ
Jojo ashaanza uchokozi..alitime Rachael akitoka akasongesha tray ikaanguka,Rachael akamwambia I hope you don't expect nitoe hii mess hapa...πππ
Mark,mtego wenye aliekewa ni wa kugongana na gari kwa barabara. Akiwa tu barabara,mbele yake kuna gari lilikuja na speed,mbaya mbovu. Mark,ati sasa anajaribu kuhepa,lakini it was too late, aligongwa,kisha akatupwa kwa mtaro,mbaya makosa..wah! Mark,kwisha maneno,hadi Neema akiwa tu hotel alifeel a certain sharp pain ya moyo,akajua there is something wrong.
Naomi alipigia huyo jamaa simu kuconfirm and akaambiwa yeah, Mark is no more! Kisha akaambiwa nakutumia malipo yako sasa hivi. Kulingana na Naomi,1 down, 3 to go,thats Neema,Jojo na Ian.
Huku kwa Isabelle,kuna parcel Jojo alitumiwa na anonymous..Jojo kufungua akasoma,na note inasema "I will not leave you in peace my dear"..Jojo akashtuka,hadi Isabelle akamuuliza shida ni nini? Jojo akadanganya akasema ni prank tu...kumbe Amani alisikia,akakuja akauliza nani huyo anakuprank? Jojo akamwambia its nothing,relax...lakini we can see,Jojo ameshtuka na huyo note yenye ametumiwa.
Makarao waliitwa kuchunguza hii ajali na chenye walipata ni ID ya Mark pekee,yeye ama mwili wake haukupatikana.
Neema akiwa kazini,anafeel tu vibaya vibaya,lakini punde si punde,akapigiwa simu na new number,akaambiwa kuna ajali imefanyika hapa,kwa gari tumepata ID ya Mark Sifa lakini mwili wake ama yeye mwenyewe hapatikani,wah! Makosa sana...Mark,ameenda wapi?