Maphone Tv

Maphone Tv Content creator
Photographer& videograher
Phone 255610603760

Unamkubali kwa bulimia ngap??
21/06/2026

Unamkubali kwa bulimia ngap??

Sasa hii Fashion sijui tuipe jina Gani ndugu zangu ebu kila mmoja ajaribu kuipa jina analoona Linafaa😂😂 Mimi naona iitwe...
21/06/2026

Sasa hii Fashion sijui tuipe jina Gani ndugu zangu ebu kila mmoja ajaribu kuipa jina analoona Linafaa😂😂 Mimi naona iitwe 😂

Hawa Ni Comedian Maarufu Sana Bongo wana Followers Wengi Wana Views wengi Lakini Chakushangaza awachekeshi ila Video Zao...
20/06/2026

Hawa Ni Comedian Maarufu Sana Bongo wana Followers Wengi Wana Views wengi Lakini Chakushangaza awachekeshi ila Video Zao Zinaenda Viral Sana Swali je ni Nyota tu zimeng'aa au Watu Wameamua kuwaonea huruma jinsi Walivyo

Upewe shi ngapi kulala hapa???
20/06/2026

Upewe shi ngapi kulala hapa???

Headmaster
20/06/2026

Headmaster

  | Furaha ya timu ya taifa ya Canada ya kupata ushindi wao wa kwanza wa kihistoria kwenye Kombe la Dunia 2026 kwa kuiba...
19/06/2026

| Furaha ya timu ya taifa ya Canada ya kupata ushindi wao wa kwanza wa kihistoria kwenye Kombe la Dunia 2026 kwa kuibamiza Qatar mabao 6-0 imegubikwa na simanzi nzito baada ya Ismaël Koné, kulazimika kutolewa nje ya uwanja kwa machela baada ya kupata jeraha baya linaloonekana kuwa ni kuvunjika mguu.

Tukio hilo la kusikitisha lilitokea mapema kipindi cha pili katika uwanja wa BC Place baada ya Koné kufanyiwa madhambi na mchezaji wa Qatar, Assim Madibo, ambaye alionyeshwa kadi nyekundu.

Hata hivyo, dakika 10 tu baada ya Koné kutolewa uwanjani, mchezaji aliyeingia kuchukua nafasi yake, Nathan Saliba, alifunga goli la nne la Canada.

Saliba aligusa mioyo ya mashabiki wengi kwa kusherehekea goli hilo huku akiwa ameinua juu jezi namba 8 ya mchezaji mwenzake huyo aliyeumia.

  Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, amesema Hezbollah italipa gharama kubwa kufuatia mapigano na mashambulizi y...
19/06/2026

Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, amesema Hezbollah italipa gharama kubwa kufuatia mapigano na mashambulizi ya hivi karibuni dhidi ya wanajeshi wa Israel kusini mwa Lebanon.

Netanyahu alisema alifanya mashauriano ya kiusalama na Waziri wa Ulinzi pamoja na Mkuu wa Majeshi baada ya kile alichokieleza kuwa shambulizi dhidi ya vikosi vya Israel.

Aliongeza kuwa aliliagiza Jeshi kujibu kwa nguvu, akidai kuwa takribani maeneo 80 yaliyolengwa yanayohusishwa na Hezbollah yalishambuliwa na makumi ya wapiganaji kuuawa.

Aidha, alisema Jeshi lililenga kituo cha amri cha Hezbollah katika eneo la Bekaa na kusisitiza kuwa operesheni za kijeshi zitaendelea ili kuzuia vitisho dhidi ya Israel.

Netanyahu pia alisema vikosi vya Israel vitaendelea kuwepo katika kile alichokiita ukanda wa usalama kusini mwa Lebanon kwa muda utakaohitajika kulinda jamii za kaskazini mwa nchi hiyo.
#

Uswisi imesema mazungumzo yaliyokuwa yamepangwa kufanyika leo nchini humo kati ya Marekani na Iran kuhusu makubaliano ya...
19/06/2026

Uswisi imesema mazungumzo yaliyokuwa yamepangwa kufanyika leo nchini humo kati ya Marekani na Iran kuhusu makubaliano ya kumaliza mzozo Mashariki ya Kati hayatofanyika k**a ilivyopangwa.

Sababu ya kuahirishwa kwa mazungumzo hayo hazijaelezwa.

 : Mshambuliaji wa DR Congo, Yoane Wissa, amezawadiwa nyumba ya vyumba vitatu jijini Kinshasa na kampuni binafsi. Tuzo h...
19/06/2026

: Mshambuliaji wa DR Congo, Yoane Wissa, amezawadiwa nyumba ya vyumba vitatu jijini Kinshasa na kampuni binafsi. Tuzo hii imetolewa kwake k**a heshima baada ya kuonyesha kiwango kizuri kwenye Kombe la Dunia la 2026. Zawadi hii inalenga kutambua mchango wake na kuwapa motisha wachezaji wengine kupambana kwa uzalendo mkubwa.

Zawadi hiyo imekuja baada ya kufunga bao la kihistoria dhidi ya Ureno kwenye mechi yao ya ufunguzi. Goli hilo lilikuwa la kwanza kwa DR Congo katika historia ya mashindano hayo makubwa duniani. Lilisaidia timu hiyo kupata sare ya 1-1 na kujipatia alama yao ya kwanza kabisa.

Wissa, ambaye anacheza Ligi Kuu ya Uingereza, sasa anatazamwa k**a shujaa wa kitaifa nchini mwao. Mashabiki kote nchini DRC wamesherehekea kwa furaha kubwa mafanikio hayo yaliyoiletea nchi yao heshima. Tukio hili linaacha alama ya kudumu ya jinsi nchi inavyothamini mafanikio makubwa ya wanamichezo.

  Mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina la Salome John (25), mkazi wa mtaa wa Kilimahewa wilayani Mpanda, amefariki duni...
19/06/2026

Mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina la Salome John (25), mkazi wa mtaa wa Kilimahewa wilayani Mpanda, amefariki dunia baada ya kudaiwa kung’atwa na mbwa anayesadikiwa kuwa na ugonjwa wa kichaa cha mbwa.

Taarifa za awali zinaeleza kuwa Salome aling’atwa na mbwa huyo takribani miezi miwili iliyopita, huku ikidaiwa kuwa hakupata nafuu baada ya tukio hilo.

Hali yake ilianza kuzorota kadri siku zilivyokuwa zikienda kabla ya kufikia hatua mbaya zaidi.

Wananchi wa eneo hilo wameeleza kusikitishwa na kifo hicho, huku wakitoa wito kwa jamii kuchukua tahadhari pindi mtu anapong’atwa na mbwa au mnyama mwingine anayehisiwa kuwa na ugonjwa wa kichaa cha mbwa ili kupata matibabu mapema.

Address

Dar Es Salam
Rabat-Sale

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Maphone Tv posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share