Archievers actors Updates

Archievers actors  Updates This page is purposely made to enhance education through Comedy and short clips of different movies

MASOMO YA MISA YA JUMAPILI*  *DOMINIKA YA PENTEKOSTE MWAKA C*  *JUNI 8 2025*  *RANGI YA LITURUJIA: NYEKUNDU β™₯️*  *MADA Y...
11/07/2026

MASOMO YA MISA YA JUMAPILI*
*DOMINIKA YA PENTEKOSTE MWAKA C*
*JUNI 8 2025*
*RANGI YA LITURUJIA: NYEKUNDU β™₯️*
*MADA YA DOMINIKA:*
```ROHO, SHERIA MPYA KWA MKRISTO.```
*_Somo la kwanza na Injili vinaonyesha kushuka kwa Roho katika hali tofauti. Hadithi za Luka na Yohane zinakamilishana na zinatufundisha kuwa Roho ndiye sheria mpya, nguvu ambayo inawezesha wanadamu kufanya mema. Roho ndiye chanzo cha umoja (anafutilia mbali vizuizi) na mahali popote alipo, anaangamiza dhambi, Somo la pili linatuonyesha matokeo ya uwepo wa Roho katika jumuiya._*
*ANTIFONA YA KUINGIA:Hek 1:7*
_Roho wa Bwana ameujaza ulimwengu, naye anavifungamanisha vitu vyote; ana ujuzi wa kila sauti, aleluya._
*KOLEKTA*
```Ee Mungu, kwa njia ya fumbo la sherehe ya leo, unalitakatifuza
Kanisa lako lote lililoenea katika kila kabila na taifa; umimine
vipaji vya Roho Mtakatifu katika ulimwengu wote, na, yale
yaliyotendwa kwa neema yako mwanzoni mwa kuihubiri Injili,
uyaeneze pia sasa mioyoni mwa waamini. Kwa njia ya Bwana
wetu Yesu Kristo Mwanao...```
*SOMO LA KWANZA*
Matendo ya Mitume 2:1-11
_Wote wakaazwa Roho Mtakatifu, na wakaanza kusema lugha nyingine._
*Somo katika kitabu cha Matendo ya Mitume*
Sku ya Pentekoste ilipowadia, wote walikuwapo mahali pamoja. Mara uvumi ulitoka mbinguni k**a upepo mkali, ukaijaza nyumba yote walimokaa. Na ndimi k**a za moto zikawatokea.
zikagawanyika na kutua kwa kila mmoja wao. Wote wakajazwa Roho Mtakatifu, na wakaanza kusema lugha nyingine k**a
Roho Mtakatifu alivyowajalia kunena. Huko Yerusalemu
walikaa Wayahudi, watu wacha Mungu wa kila taifa lililoko
chini ya mbingu. Basi, uvumi huu ulipotukia, wengi walikutana,
wakashikwa na mshangao kwa sababu kila mmoja wao aliwasikia
wanasema lugha yake mwenyewe. Wote walishtuka, na kwa mshangao waliuliza, "Hao wote wanaosema si Wagalilaya? Kwa
namna gani kila mmoja wetu anaisikia lugha aliyozaliwa nayo?
Sisi Waparthi, Wamedia, Waelami, nasi tukaao Mesopotamia,
Yudea, na Kapadokia, Ponto, na Asia, Firigia na Pamfilia, Misri na wilaya za Libia kuelekea Kirene, pia wageni waliotoka Roma,
Wayahudi na waongofu, Wakrete na Waarabu, sote tunawasikia
wakisema kwa lugha zetu, matendo makuu ya Mungu."
*Neno la Bwana.*
*ZABURI YA KUITIKIZANA*
Zaburi 104: 1ab na 24ac, 29bc-30,31 na 34 (K. 30)
*K. Bwana, umtume roho wako na uufanye upya uso wa nchi.*
*au: Aleluya.*
Umsifu Bwana, ee nafsi yangu!
Ee Bwana, Mungu wangu u mkuu sana!
Ee Bwana, jinsi gani zilivyo nyingi kazi zako!
dunia imejaa viumbe vyako.
*K.*
Ukiondoa pumzi yao, wanakufa, na kuyarudia mavumbi yao,
Ukimtuma roho wako wanaumbwa,
na unafanya upya uso wa nchi.
*K.*
Utukufu wa Bwana na udumu milele:
Bwana na afurahie kazi zake!
Tafakari yangu na impendeze Mungu;
nami nitafurahi katika Bwana.
*K.*
*SOMO LA PILI*
Warumi 8:8-17
_Wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu ni wana wa Mungu._
*Somo katika barua ya Mtakatifu Paulo kwa Warumi*
Ndugu zangu: Wote walio wafuasi wa mwili hawawezi
kumpendeza Mungu. Ninyi, lakini, si wafuasi wa mwili, bali wa Roho, ikiwa Roho wa Mungu amekaa kweli ndani yenu. K**a mtu hana Roho wa Kristo, basi si mtu wake. Tena Kristo akiwa
ndani yenu, miili imekufa kwa sababu ya dhambi, lakini roho ni uzima kwa sababu ya uadilifu. Lakini Roho yake yeye aliyemfufua Yesu katika wafu akikaa ndani yenu, basi yeye aliyemfufua Kristo Yesu katika wafu ataiokoa pia miili yenu katika hali ya kufa na kuitilia uzima kwa nguvu ya Roho anayekaa ndani yenu. Basi, ndugu, tuna wajibu wetu, lakini si kwa mwili
tuishi k**a mwili unavyotamani. Maana mkiishi k**a mwili unavyotamani, mtakufa. Bali mkiyafisha mazoea maovu ya mwili kwa nguvu ya Roho, mtaishi. Kwani wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu ni wana wa Mungu. Kwa maana hamkupata roho ya utumwa mwogope tena, bali mmempokea roho
anayewafanya kuwa wana wa Mungu na kuita, "Abba! Baba!"
Roho mwenyewe hushuhudia roho zetu ya kuwa sisi ni watoto wa Mungu. Basi, tukiwa wana, tu warithi pia, yaani warithi wa Mungu wanaorithi pamoja na Kristo, tukiwa tunavumilia mateso pamoja na Kristo, tupate kutukuzwa pamoja naye.
*Neno la Bwana.*
*SEKWENSIA*
Uje, Roho Mtakatifu,
Tuangaze toka mbingu, Roho zetu kwa mwangao.
Uje Baba wa maskini,
Uje mtoa wa vipaji vya Mungu, Uje Mwanga wa mioyo,
Ee mfariji mwema sana,
Ee rafiki mwanana, Ewe raha mustarehe,
Kwa kazi u pumziko,
kwenye joto burudisho, U mfutaji wa machozi,
Ewe mwanga wenye heri,
Uwajaze waamini, Neema yako mioyoni,
Bila nguvu yako Wewe,
Mwanadamu hana kitu, Kwake yote yana koma,
Osha machafuko yetu,
Panyeshee pakavu petu, Na kuponya majeraha,
Elegeze ukaidi,
Pasha moto ubaridi, Nyosha upotovu wote,
Wape waamini wako,
Wenye tumaini kwako, Paji zako zote saba,
Wape tuzo ya fadhila,
Wape mwisho bila ila, Wape heri ya milele.
Amina. Aleluya.
*SHANGILIO LA INJILI*
Warumi 8:8-17
*Aleluya. Aleluya.*
_Njoo Roho Mtakatifu, Jaza nyoyo za waumini wako; washa moto wa mapendo ndani yao._
*Aleluya.*
*INJILI*
Yohane l4:15-16.23b-26
_Roho Makatifu atawafundisha yote._
*Somo la Injili takatifu ilivyoandikwa na Yohane*
Wakati ule: Yesu aliwaambia wafuasi wake, "Mkinipenda, mtashika amri zangu. Nami nitamwomba Baba, naye atawapa Msaidizi mwingine, ili awepo kwenu hata milele. Mtu akinipenda, atashika neno langu, na Baba yangu atampenda, nasi tutakuja kwake na kufanya makao kwake. Asiyenipenda hayashiki maneno yangu; na neno mnalolisikia si langu, bali ni la Baba aliyenituma. Hayo nimewaambia nilipokaa kwenu. Lakini Msaidizi, ndiye Roho Mtakatifu, ambaye Baba atamtuma kwa jina langu, atawafundisha yote na atawakumbusha yote niliyowaambia mimi."
*Injili ya Bwana.*
Pascal Oluloh
πŸ™
sunday reading follow me bac

07/05/2026

OYUO MOKAGO???

I used to think that 5 ants + 5 ants = Tenants πŸ˜‹
26/04/2026

I used to think that 5 ants + 5 ants = Tenants πŸ˜‹

BTN YOUR MUM AND YOUR DAD WHO IS  HARSH ?
22/03/2026

BTN YOUR MUM AND YOUR DAD WHO IS HARSH ?

WHO WAS THE FIRST MAN TO DIE ACCORDING TO BIBLE A) ADAMB.) ABRAHAM C) ABEL D) NOAH GIFT IS 500 FOR FIRST TO GET IT RIGHT
22/03/2026

WHO WAS THE FIRST MAN TO DIE ACCORDING TO BIBLE

A) ADAM
B.) ABRAHAM
C) ABEL
D) NOAH

GIFT IS 500 FOR FIRST TO GET IT RIGHT

22/03/2026

AYANA Updates

22/03/2026

# Following Highlights

11/03/2026
With Sonkid kenyansa – I'm on a streak! I've been a top fan for 4 months in a row. πŸŽ‰
11/03/2026

With Sonkid kenyansa – I'm on a streak! I've been a top fan for 4 months in a row. πŸŽ‰

Address

Doha
00000

Telephone

+254710824649

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Archievers actors Updates posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Archievers actors Updates:

Shortcuts

Share