CROWN FM/TV MEDIA

CROWN FM/TV MEDIA media/news/entertainment

Calculator za wananchi zinademaje huko?
19/01/2025

Calculator za wananchi zinademaje huko?

Man city kafungwaArsenal kafungwaLiverpool kafungwa Yanga kafungwaTimu kubwa zote leo zimepoteza🥹🥹🥹 Faraja ni kubwa😁😁😁
03/11/2024

Man city kafungwa
Arsenal kafungwa
Liverpool kafungwa
Yanga kafungwa
Timu kubwa zote leo zimepoteza
🥹🥹🥹
Faraja ni kubwa
😁😁😁

16/09/2024
Cv ya Leonel Ateba Mshambuliaji Mpya wa Simba 2024/2025 | Straika Mpya wa Simba 2024/2025Klabu ya Simba Sc imekamilisha ...
15/08/2024

Cv ya Leonel Ateba Mshambuliaji Mpya wa Simba 2024/2025 | Straika Mpya wa Simba 2024/2025

Klabu ya Simba Sc imekamilisha uhamisho wa mshambuliaji Lionel Ateba kwa mkataba wa miaka miwili kwa ada inayodaiwa kuwa dola laki mbili (Tsh 542,000,000). Ateba (25) raia wa Cameroon alijiunga na USM Alger mnamo Januari, 2024 kwa dau la dola laki tatu akitokea Dynamo Douala ya nyumbani kwao Cameroon akiifungia USM Algers bao MOJA tu na ‘assist’ 8 kwenye mechi 16.

Cv ya Leonel Ateba Mshambuliaji Mpya wa Simba 2024/2025
Leonel Ateba, anayejulikana kwa jina kamili Christian Leonel Ateba Mbida, ni mchezaji wa kimataifa mwenye uraia wa Cameroon ambaye amejiunga na klabu ya Simba SC kwa msimu wa 2024/2025. Alizaliwa tarehe 6 Februari 1999, na kwa sasa ana umri wa miaka 25. Akiwa na urefu wa mita 1.83, Ateba ni mshambuliaji wa kati (Centre-Forward) ambaye pia ana uwezo wa kucheza k**a winga wa kushoto na kulia. Hii inamfanya kuwa mchezaji wa kipekee mwenye uwezo wa kushambulia kutoka pande zote za uwanja.

Wataleta timu kweli🤔🤔
11/07/2024

Wataleta timu kweli🤔🤔

Simba itakutana na mshindi wa mchezo wa hatua ya awali ya Kombe la Shirikisho barani Afrika kati ya Uhamiaji Fc ya Zanzi...
11/07/2024

Simba itakutana na mshindi wa mchezo wa hatua ya awali ya Kombe la Shirikisho barani Afrika kati ya Uhamiaji Fc ya Zanzibar dhidi ya Mshindi wa kombe la Shirikisho la Libya ambaye ataoatikana baadae.

Coastal Union wao watakutana na FC Bravos ya Angola katika hatua hiyo ya awali na mshindi wa jumla atakutana na FC Lupopo ya Congo DR katika hatua ya kwanza ya michuano hiyo ya Kombe la Shirikisho barani Afrika

Mabingwa wa Tanzania Bara, Yanga watapambana na Vitalo ya Burundi kwenye hatua ya awali ya ligi ya mabingwa barani Afrik...
11/07/2024

Mabingwa wa Tanzania Bara, Yanga watapambana na Vitalo ya Burundi kwenye hatua ya awali ya ligi ya mabingwa barani Afrika.K**a Yanga wataitoa Vitalo ya Burundi watacheza na mshindi kati ya SC Villa ya Uganda na Commercial Bank ya Ethiopia huku Azam FC wamepangwa kucheza na APR ya Rwanda kwenye hatua ya awali ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika.
K**a Azam FC wataitoa APR basi watapambana na mshindi kati ya JKU ya Zanzibar dhidi ya Pyramids FC ya Misri anayochezea nyota wa zamani wa Yanga Fiston Mayele

Rais William Ruto amelivunja baraza lake la mawaziri isipokuwa kwa nafasi ya Kiongozi wa mawaziri na Waziri wa Mambo ya ...
11/07/2024

Rais William Ruto amelivunja baraza lake la mawaziri isipokuwa kwa nafasi ya Kiongozi wa mawaziri na Waziri wa Mambo ya Nje, Musalia Mudavadi.

Uamuzi huo wa Rais Ruto ameutangaza leo, Alhamisi Julai 11, 2024 nchini Kenya akisema mabadiliko hayo yatasaidia kuunda serikali itakayosaidia kuongoza kasi ya utekelezaji wa mipango ya kukabiliana na changamoto nyingi zinazowakabili wananchi.

Katika hotuba yake hiyo iliyopokelewa kwa shangwe na wananchi wa Kenya hususan vijana maarufu (GEN Z), Ruto amesema, licha ya kuvunja baraza hilo nafasi ya Naibu wa rais haijaathiriwa na mabadiliko hayo pia.

Uamuzi huo alioutangaza Rais Ruto unahusishwa moja kwa moja na maandamano ya vijana wa Kenya waliokuwa wakipinga Muswada wa Sheria wa Bajeti Kuu ya Nchi hiyo ambao ulilalamikiwa kwakuwepo na ongezeko kubwa la kodi litakalomuumiza mwananchi wa kawaida na hivyo Rais Ruto kukataa kuusaini na kuurejesha muswada huo bungeni.

Hata hivyo Rais Ruto amesema itamchukua muda kufanya majadiliano ya kuunda baraza jipya la mawaziri litakalohusika na uendeshaji wa serikali suala lililopokelewa na maoni mseto kutoka kwa wananchi.

Rais Ruto amesema baraza hilo litaangalia namna ya kusaidia kuongeza ufanisi na kasi ya kukabiliana na mzigo wa madeni, kuongeza rasilimali za ndani, kupanua nafasi za kazi, kuondoa ubadhirifu wa fedha, kupunguza gharama na matumizi makubwa ya serikali na kukomesha ufisadi wa fedha za umma.

Je unahitaji kuipa thaman biashar yko? Bas unahitaj kuitangaza na kuipa muonekano mzuuri kwa wateja wako wasialiana nasi...
24/06/2024

Je unahitaji kuipa thaman biashar yko? Bas unahitaj kuitangaza na kuipa muonekano mzuuri kwa wateja wako wasialiana nasi kwa mahitaj mbal mbal Kam vile ÷
Logo design
Poster Design
Flayers / Brochure
Branding e.t.c
Contact us +255760895900

Mzee william anafanya kazi katika  kampuni inayohusika na maswala ya bima na kila siku huwa anatumia usafiri wa train an...
27/05/2024

Mzee william anafanya kazi katika kampuni inayohusika na maswala ya bima na kila siku huwa anatumia usafiri wa train anapoenda kazini na kurudi nyumbani

lakini siku moja inageuka chungu kwake baada ya kufukuzwa kazi bila sababu ya msingi na bosi wake,kwa uchungu anaingia katika train ambayo huwa anapanda kilasiku ili kurudi nyumbani .

ndani ya train anakutana na mama mmoja wa makamo ambae hajawahi kumuona ktk hiyo train aliyozowea kupanda kilasiku, mama alisogea katika siti ya Mzee william na kuanza kupiga story mbalimbali, story zilipo noga akamwambia Mzee william kwamba anampa kiasi cha dola elfu 25 kwa sharti la kumfanyia kazi ya kumtafuta mtu mmoja ndani ya train ambaye ana mzigo wake lakini hamwambii huyo mtu yupoje lakini anachomwambia ni kwamba mtu huyo ana begi tu leusi🤣

Mzee anachukulia suala Hilo la kupata Hela kimseleleko k**a masihara hivi, ila huyo mama anamwambia Mzee william akitaka kuamini aende katika bafu la treni kuna sehemu ataikuta hiyo hela na akimaliza kazi nzima atapewa tena dolla elfu 75(mamilion yakutosha) , jamaa anaenda bafuni anakuta kweli Kuna dola elf 25😍

Wazo likamjia la kutoka ndani ya train na kukimbia na hela Dola elf 25 bila kufanya kazi aliyopewa, lakini wakati anataka kutoka ndani train akakutana na mtu akampa bahasha ina pete ya mke wake🤔hiyo ni k**a onyo kwamba wanamjua na wanaweza kufanya chochote kwa mke wake hivyo inabidi arudi ndani ya train aendelee na kazi.kisanga ni namna ya kumpata huyo mtu , kwa nn anatafutwa na hilo begi lina nn !!!!!?

utamu wa movie unaanzaia hapa👉Mzee alizunguka train nzima kumtafuta huyo mtu ambae hajukikani ni mwanamke au mwanaume,too bad watu wenye mabegi meusi Wapo wengi🤔mpaka ilifika kipindi anaonekana k**a gaidi

Ila Muongozo aliopewa ni kwamba mtu huyo anayepaswa kumtafuta ni mtu ambae hajawahi kupanda hiyo train kwa hiyo akawa anaangalia mtu mmoja mmoja ambaye hajawahi kumuona ktk hiyo train , kuwafuatilia na kuwahoji kimitego mitego mpaka wakawa wanaingiwa na mashaka juu yake
The commuter jina la muvi

Address

Arusha

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when CROWN FM/TV MEDIA posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share