29/09/2025
TANGAZO LA KUJISAJILI NA SHULE YA KATEKESI KWA MUDA WA MIEZI MIWILI
Usajili kuanzia leo tarehe 26 September hadi 7 Oct, 2025. Tutachukua wanafunzi 50 tu. Hivyo wahi mapema kujisajili k**a tangazo hili litakavyoelekeza. Soma lote tafadhari.
Shule itaanza tarehe 10 October hadi 7 December, 2025.
Jerusalem Family Tv ambayo ni huduma ya uinjilishaji kwa njia ya vyombo vya habari tunapenda kuwajulisha kuwa.
Tumeandaa tena shule ya KATEKESI IKIWA NI MARA YETU YA KWANZA KUWA NA SHULE YA NAMNA HII. Itakuwa inafundishwa kwa njia ya mtandao katika Group la WhatsaPp.
LENGO LA SHULE ni kuwafundisha Wakristo Wakatoliki masomo ya KATEKISIMU kiundani zaidi ya pale ambapo umewahi kukutana nayo, ambapo yatachochea Imani zetu ndani ya kanisa na kutufanya tujitambue zaidi wapi tulipo na kuwa imara zaidi ndani ya Kristo. Ni shule ambayo itakuwa na masomo yanayoimarisha Imana ya Mkristo katika kumuabudu Mungu ukiwa hapa duniani. Hivyo k**a una lengo la kutaka kukua Kiroho zaidi ya hapo ulipo shule hii ni muhimu sana kwako.
Gharama ni bure hakuna ada wala malipo bali ghrama yako ni bando lako tu maana hutatakiwa kukosa hata kipindi kimoja cha masomo kwa muda wote wa miezi yote miwili ya shule.
MAMBO WATAKAYOSOMA
1. Kutakuwa na masomo kwa njia ya topic za kukusaidia juu ya maisha binafsi ya Kiroho.
2. Kutakuwa na masomo ya kukusaidi uifahamu zaidi Imani ya Kanisa Katoliki na mafundisho yake yanalenga nini kwa jamii ya waamini wake.
3. Kutakuwa na masomo ya Litrujia yatakayokusaidia ujue namna ya kumuona Mungu kupitia Litrujia ya Kanisa Katoliki.
4. Kutakuwa na masomo yatayokusaidia ufahamu mambo tata yanayotatiza Imani za Wakatoliki wengi k**a vile, Msalaba wa Sanamu kwanini? Mama Kanisa ni nani? Je ni kweli kanisa linaunga mkono ndoa za jinsia moja? Je ni kweli sikuhizi kanisa linaruhusu kuvunja ndoa? Waklero ni wakina nani? Na mengine mengi maswali tata uliyonayo juu ya kanisa utapata majibu yake kupitia shule hii.
5. Kwa yule ambaye tayari alikuwa ameshaanza kuwa na wasiwasi juu ya Imani ya Kanisa Katoliki na mapokeo yake shule hii itamsaidia kumpa majibu ya maswali yake yote aliyonayo.
6. Pia kutakuwa na mambo mengine mengi mazuri utakayojifunza ya kukusaidia kukuvusha mahali moja kwenye nyingine. Ikiwemo kujifunza jinsi ya kukua Kiroho ukiwa ndani ya kanisa.
SIFA ZA KUJIUNGA NA SHULE
1. Hakikisha wewe ni Mkristo ambaye unamalengo serious ya kutaka kukua Kiroho bila kulazimishwa bali kwa hiari yako mwenyewe.
2. Uwe una uhakika wa bando kwa muda wa miezi yote miwili. Kwani hatutakuelewa ukikosa masomo kisa bando utatolewa darasani kwa kufukuzwa shule.
3. Uwe tayari kusimamiwa na kuongozwa katika kila hatua ya kujifunza ili uweze kukua Kiroho.
4. Uwe tayari kujifunza masomo ya Kikristo yaliyochini ya miongozo ya Kanisa Katoliki bila kuleta usumbufu wa kutaka fundisho nje ya hapo.
5. Uwe tayari kusikiliza kila topic itakayokuwa inafundishwa kwenye shule pamoja na kushiriki kila zoezi litakalokuwa linatolewa kwa kumuheshimu kila mwalimu kwani nje na hayo unaweza fukuzwa shule.
6. Hakikisha unatenga muda wa kutosha kwaajili ya kusikiliza masomo na kufanya kila zoezi la shule kila siku kwani shule; kila somo moja litakuwa ni ndani ya lisali-moja.
JINSI YA KUJIUNGA NA SHULE
Unaweza ukajisajili sasa kusoma shule hii kwa kutuma jina lako kupitia namba +255 719 086 017 au +255 785 935 445 Tuma jina lako na mkoa uliopo kisha Andika neno NAOMBA KUJISAJILI NA SHULE.
Idadi tunachukua watu 50 tu. Idadi ikitimia kabla ya tarehe ya mwisho wa usajili tutafunga usajili. Kwani shule itaanza rasmi tarehe 10 October hadi 7 December 2025. Hivyo wahi mapema nafasi zikijaa hamisini hatutachukua watu tena itabidi msubiri msimu mwingine. Hivyo mnaalikwa sasa kuanza kujisajili bila kuchelewa. K**a unaswali uliza kupitia namba hizo pia.
*NYOTE MNAKARIBISHWA*