
10/09/2025
Mgombea urais wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu
Hassan ameendelea na kampeni zake za uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 kwa kuzungumza na wananchi wa Wilaya ya Iramba mkoani Singida, akiahidi kuendeleza miradi mikubwa ya kijamii na kiuchumi.
Amesema Serikali itakamilisha ujenzi wa vituo vitatu vya afya eneo la Mtoa, Mwandegembe na Irungu ili kuboresha huduma za afya.
Katika elimu, ameeleza kuwa shule mpya ya Amali na Shule ya Sekondari ya Mbelekese zimekamilika, hatua itakayoongeza nafasi za masomo kwa wanafunzi.
Samia amesema tenki kubwa la maji Kizonzo lenye ujazo wa lita 300,000
limekamilika na Serikali itaendeleza mradi wa maji kutoka Ziwa Victoria kuhakikisha wananchi wanapata maji safi.
Pia, kupitia sekta ya madini, Serikali imeanzisha soko la dhahabu litakalowawezesha wachimbaji wadogo kupata masoko ya uhakika na kuongeza kipato chao.