25/05/2026
https://youtu.be/jQKUEfq9_ko?si=W0t4BuwTLhGqSboh
MEDIA
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Monduli Mhe.kisioki Moitiko afanya ziara stendi ya Kata ya Monduli mjini nakuahidi kutoa kiasi cha milioni 10 pamoja na kuelekeza kufungwa taa 10 Ili kufanya ukarabati wa stendi ya Kata ya Monduli mjini.
Aidha Mwenyekiti wa uongozi usafirishaji Ndugu.Abdula Lema ashukuru Halmashauri ya Monduli Kwa kuona umuhimu wa stendi hio huku akiahidi kuonyesha ushirikiano na uaminifu kwenye Kila shilingi katika matumizi yake mara baada ya kupokea fedha hizo.
Pia Diwani wa Kata ya Monduli mjini Mhe.Hussein Olekuney akikisisitiza kushirikiana na wafanya biashara pamoja na wananchi wa eneo la stend kufanya uamuzi Kwa pamoja Ili kuleta tija Kwa matumizi ya fedha hizo.