Paul Makonda Yupo Kazini

Paul Makonda Yupo Kazini MAHALI SAHIHI KWA WOTE WANAOUNGA MKONO KAZI ZA MKUU WA MKOA WA ARUSHA MHE. PAUL MAKONDAđź«¶

18/04/2025

Viongozi wa Dini kutoka madhehebu mbalimbali mkoani Arusha leo wameungana katika ibada maalum ya Ijumaa Kuu kumuombea Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. Paul Christian Makonda, kwa ajili ya uongozi wake na ustawi wa Mkoa wa Arusha.

Ibada hiyo ya Pasaka – Ijumaa Kuu imefanyika katika viwanja vya Sheikh Amri Abeid na kuhudhuriwa na waumini kutoka madhehebu tofauti, ikiwa ni ishara ya mshik**ano na upendo wa kiroho katika kipindi hiki muhimu cha Kikristo.

PROF. KABUDI ASIFU UBUNIFU WA RC MAKONDA, KUIWEKA ARUSHA KWENYE RAMANI KIMATAIFA.Mkuu wa Mkoa wa Arusha amekutana na kuf...
08/03/2025

PROF. KABUDI ASIFU UBUNIFU WA RC MAKONDA, KUIWEKA ARUSHA KWENYE RAMANI KIMATAIFA.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa sanaa, utamaduni na michezo Prof. Palamagamba Kabudi, ambaye yupo mkoani Arusha kukagua maendeleo ya Ujenzi wa uwanja wa michezo unaojengwa Mkoani Arusha kwaajili ya mashindano ya Kandanda kwa mataifa ya Afrika maarufu k**a AFCON 2027.

Katika mazungumzo yao, Mhe. Kabudi amempongeza Mhe. Makonda kwa mashindano na matukio mbalimbali ya kimichezo aliyoyaratibu na kuyasimamia, ikiwemo Land Rover Festival 2024, ambayo imesaidia kuitangaza Arusha kimataifa na kutoa fursa za kiuchumi kwa wananchi wa Mkoa wa Arusha waliouza bidhaa na huduma mbalimbali wakati wa tamasha hilo pamoja na mashindano mengine ya kimichezo yaliyofanyika Jijini Arusha tangu kuteuliwa kwake.

Kwa upande wake Mhe. Makonda ameeleza kuwa Mkoa wa Arusha unazidi kufunguka kitalii ambapo kwasasa Utalii wa safari na michezo ndiyo ajenda kuu ya Mkoa na Rais Samia pia anaendelea na mpango wake wa kutambulisha utalii wa matibabu katika Mkoa huo kando ya utalii wa kitamaduni ambao Mkoa wa Arusha utaanzisha maonesho yake kuanzia mwezi Machi mwaka huu, kwa kukutanisha jamii mbalimbali za kigeni zilizopo mkoani hapa kwaajili ya kuonesha tamaduni zao mbalimbali.

Mashindano ya AFCON 2027 yatafanyika kwa ushirikiano wa wenyeji wa nchi tatu, Tanzania, Kenya na Uganda ambapo kwa Tanzania viwanja kadhaa vitatumika katika michuano hiyo ikiwemo uwanja mpya unaojengwa na serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan, eneo la Bondeni city Jijini Arusha, serikali pia ikitarajia kujenga mji wa biashara pembezoni mwa uwanja huo ili kutoa fursa kwa wakazi wa Arusha kunufaika kiuchumi.

RAIS SAMIA AWASILI ARUSHA KUONGOZA MAADHIMISHO SIKU YA WANAWAKE DUNIANI.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Sam...
08/03/2025

RAIS SAMIA AWASILI ARUSHA KUONGOZA MAADHIMISHO SIKU YA WANAWAKE DUNIANI.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluh Hassan leo Jumamosi Machi 08, 2025, amewasili Mkoani Arusha kupitia uwanja wa ndege wa Kimataifa KIA, na kupokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Nurdin Babu na Viongozi wengine wa Chama Cha Mapinduzi na serikali. Rais yupo Mkoani Arusha kuongoza maadhimisho ya siku ya wanawake kitaifa katika viwanja vya Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha.

Dkt. Mpango kwenye kikao kazi cha tano cha Serikali MtandaoMakamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. ...
11/02/2025

Dkt. Mpango kwenye kikao kazi cha tano cha Serikali Mtandao

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango amewasili kwenye kikao kazi cha tano cha Serikali mtandao, kinachofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC).

Dkt. Philip Mpango amepokelewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. George Simbachawene pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. Paul Christian Makonda.

27/01/2025

RAIS SAMIA KUWA MGENI RASMI MAADHIMISHO SIKU YA WANAWAKE KITAIFA JIJINI ARUSHA.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa Mgeni rasmi kwenye maadhimisho ya siku ya wanawake duniani ambapo Kitaifa maadhimisho yanatarajiwa kufanyika Jijini Arusha, tarehe nane mwezi Machi 2025.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda amebainisha hayo leo Ijumaa Januari 24, 2025 wakati akizungumza na wanahabari Ofisini kwake Jijini Arusha, akisema maadhimisho hayo yataambatana na shughuli mbalimbali kwa siku nne mfululizo, ikiwemo maonesho ya kibiashara, Michezo mbalimbali kwa wanawake pamoja na burudani zikazoambatana na nyama Choma za Ng'ombe zaidi ya mia tano.

Ametumia fursa hiyo pia kuwataka wanawake wa Mkoa wa Arusha kuchangamkia fursa mbalimbali zitakazoambatana na maadhimisho hayo, akiwaalika wanawake kufika kwenye Ofisi za Wakuu wa Wilaya kwaajili ya kuwasilisha mawazo yao mbalimbali yatakayowasaidia kuweza kunufaika na Uenyeji wa Arusha kwenye maadhimisho hayo ya siku ya wanawake Kitaifa.

Mhe. Makonda amesema tayari Mkoa umeanza maandalizi ya Maadhimisho hayo, akiisihi jamii ya Mkoa wa Arusha kwa maana ya mtu mmoja mmoja pia kujiandaa, kwani kutakuwa na utoaji wa zawadi maalum kwa wanawake/ akinamama, zawadi ambazo zitatolewa na Watu mbalimbali kwa Wazazi wao k**a sehemu ya shukrani kwa malezi.

24/01/2025
LEOPARD TOURS WATOA PIKIPIKI 20 KWA POLISI ARUSHA, KUFADHILI MATIBABU KWA WASIOJIWEZAMtendaji Mkuu wa Leopard Foundation...
24/01/2025

LEOPARD TOURS WATOA PIKIPIKI 20 KWA POLISI ARUSHA, KUFADHILI MATIBABU KWA WASIOJIWEZA

Mtendaji Mkuu wa Leopard Foundation inayomilikiwa na Kampuni Mama ya Leopard Tour inayojishughulisha na masuala ya Utalii Mkoani Arusha, Ndugu Zuher Fazal leo Ijumaa Januari 24, 2025 kwaniaba ya Taasisi hiyo, amekabidhi Pikipiki 20 kwa Jeshi la Polisi Mkoani Arusha katika jitihada za kusaidia kuimarisha ulinzi na usalama Mkoani Arusha.

Wakati wa makabidhiano hayo kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda, Ndugu Fazal amemshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa usimamizi wake mzuri wa sekta ya utalii nchini, akisema kuimarika kwa Sekta hiyo pamoja na mafanikio makubwa yanayopatikana chini ya Serikali ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, ndicho kilichowahamasisha kujitoa kuchangia Vitendetakazi hivyo kwa Jeshi la Polisi.

Kwa Upande wake Mhe. Makonda,licha ya kuishukuru Leopard Foundation, ameahidi kuendelea kutengeneza mazingira mazuri kwa wafanyabiashara wa Mkoa wa Arusha kwaniaba ya Mhe. Rais Samia ili wafanyabiashara hao waendelee kuwa chachu ya maendeleo ya uchumi wa Mkoa wa Arusha kupitia fursa mbalimbali za ajira wanazozizalisha pamoja na mchango wao wanaourudisha kwenye Jamii.

Leopard Foundation inayotoa usaidizi wa Kijamii katika mapambano dhidi ya umaskini pamoja na kusaidia katika elimu, usimamizi wa mazingira na afya, imeingia makubaliano pia na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha katika kusaidia huduma za matibabu kwa wahitaji wasiojiweza kiuchumi wanaofika Ofisini kwa Mkuu wa Mkoa kwaajili ya matibabu.

BILIONI 14.4 KULIPWA FIDIA, UTEKELEZAJI MRADI WA MAGADI SODA WILAYANI MONDULI.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk...
23/01/2025

BILIONI 14.4 KULIPWA FIDIA, UTEKELEZAJI MRADI WA MAGADI SODA WILAYANI MONDULI.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ameridhia kutoa Jumla ya Shilingi Bilioni 14.4 k**a fidia kwa Wakazi wa Vijiji vinne vilivyopo kwenye Kata ya Engaruka Wilayani Monduli Mkoani Arusha ikiwa ni muendelezo wa mkakati wa Serikali ya awamu ya sita katika uendelezaji wa miradi ya Kimkakati yenye tija kwa Taifa.

Kwaniaba ya Rais Samia leo Alhamisi Januari 23, 2025, Waziri wa Viwanda na biashara Mhe. Dkt. Seleman Jaffo wakati akizindua ugawaji wa fidia hizo kwa awamu ya kwanza yenye takribani Bilioni 6.2, amewataka wasimamizi wa zoezi hilo kuhakikisha kuwa ulipaji wa fidia hizo unamalizika kabla ya Februari 15, 2025, na kuaigiza shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) kushughulikia malalamiko yote ya ya fidia kwa wananchi wa eneo hilo.

Katika hatua nyingine Waziri Jafo aliyeambatana na Viongozi mbalimbali akiwemo Naibu Waziri wa Wizara ya ardhi Mhe. Jofrey Pinda, amesema serikali imeweka mpango maalum wa kuhakikisha kuwa eneo la Engaruka linakuwa na barabara zinazopitika muda wote sambamba na upatikanaji wa umeme mkubwa wa Kilowati 33 ili kusaidia katika shughuli za uendeshaji wa viwanda viwili vikubwa vinavyotarajiwa kutekeleza mradi huo.

Akizungumza katika Uzinduzi huo, Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Makonda, amesema Arusha ni miongoni mwa mikoa yenye bahati na kadri siku zinavyosonga, Mkoa huu utatoa fursa mbalimbali za maendeleo kwenye sekta za Kilimo, Madini na Michezo, zitakazosaidia wananchi kujikwamua na umaskini akihimiza kuendelea kupewa kipaumbele cha ajira kwa wazawa wakati wa utekelezaji wa miradi mbalimbali inayotekelezwa kwenye Mkoa wa Arusha.

Akisoma taarifa ya utekelezaji wa mradi huo wa Kimkakati, Mkurugenzi mwendeshaji wa NDC Dkt.Nicolaus Shombe amesema mradi huo wa magadi soda umechukua zaidi ya miaka 29 tangu mchakato wake ulipoanza baada ya NDC kufanya utafiti wake na kubaini uwepo wa magadisoda yenye kufikia mita za ujazo Bilioni 3.8 sawa

Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Selemani Jafo akiwasili kwenye uzinduzi wa zoezi la ulipaji fidia katika mradi wa mag...
23/01/2025

Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Selemani Jafo akiwasili kwenye uzinduzi wa zoezi la ulipaji fidia katika mradi wa magadi soda, hafla hiyo inayofanyika leo Januari 23, 2025 eneo Engaruka Monduli mkoani Arusha.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. Paul Christian Makonda ameshiriki mazishi ya Baba mzazi wa Mtangazaji wa Jahazi HD , marehe...
23/01/2025

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. Paul Christian Makonda ameshiriki mazishi ya Baba mzazi wa Mtangazaji wa Jahazi HD , marehemu Burhani Mandi aliyefariki January 20, 2025 Jijini Dar es Salaam na kuzikwa Leo katika makaburi ya Njiro Jijini Arusha.

MKURUGENZI WA UN WOMEN NA RC MAKONDA, WAJADILI USHIRIKIANO KATIKA MASUALA YA KIJINSIAMkurugenzi wa Nchi wa shirika la Um...
22/01/2025

MKURUGENZI WA UN WOMEN NA RC MAKONDA, WAJADILI USHIRIKIANO KATIKA MASUALA YA KIJINSIA

Mkurugenzi wa Nchi wa shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya wanawake (UN Women), Hodan Addou, amefanya ziara Mkoani Arusha ambapo amekutana na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. Paul Christian Makonda, kujadili masuala muhimu yanayohusu usawa wa kijinsia na uwezeshaji wa wanawake katika masuala ya kiuchumi.

Katika mazungumzo yao yaliyofanyika Ofisini kwa Mkuu wa Mkoa huo leo tarehe 22 Januari, 2024, Mhe. Makonda amesema kuwa, Mkoa wa Arusha umekuwa ukiendesha shughuli za kuwawezesha wanawake kiuchumi sambamba na kuzuia masuala ya ukatili wa Kijinsia kwa wanawake na Watoto na uhamasishaji wa wanawake kushiriki katika masuala ya Uongozi wa ngazi mbalimbali.

Mhe. Makonda ameongeza kuwa, Kupitia Mradi wa UN WOMEN ujulikanao k**a WLER “Strengthening Women And Girls’ Meaningful Participation, Leadership, And Economic Rights”. Ulionufaisha Halmashauri tatu (3) za Mkoa wa Arusha wanawake wamekuwa wakipatiwa elimu kuhusu masuala ya kiuchumi na kutojihusisha na mikopo umiza badala yake kutumia fursa ya Mikopo isiyo na riba ya 10% inayotolewa kwenye Halmashauri zote Nchini.

“Tuna dhamira ya kuhakikisha kuwa wanawake na wasichana wa Arusha wanapewa nafasi za kiuchumi, kijamii, na elimu. Tunaamini kuwa kwa kushirikiana na UN Women, tunaweza kufanya mabadiliko makubwa,” amesema Mhe. Makonda.

Kwa upande wake Mkurugenzi Hodan Addou amesema kuwa UN Women imekuwa ikifanya kazi kwa karibu na Serikali katika kuhakikisha kuwa wanawake wanapata nafasi sawa katika sekta zote za maendeleo na kusisitiza umuhimu wa kushirikiana katika mipango ya maendeleo jumuishi inayozingatia mahitaji ya wanawake vijijini na wale walioko katika mazingira magumu.

“Uwezeshaji wa wanawake si tu suala la haki za binadamu bali ni msingi wa maendeleo endelevu na tunafurahi kuona Mkoa wa Arusha ukichukua hatua madhubuti katika kusimamia usawa wa kijinsia,” amesema Bi. Addou.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Makonda Ndani ya Mkutano Mkuu Maalum wa Chama cha Mapinduzi CCM Taifa, unaofanyika kati...
19/01/2025

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Makonda Ndani ya Mkutano Mkuu Maalum wa Chama cha Mapinduzi CCM Taifa, unaofanyika katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete Convection Centre Dodoma.

Address

Arusha

Telephone

+255788821721

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Paul Makonda Yupo Kazini posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Paul Makonda Yupo Kazini:

Share