Mega fm Arusha

Mega fm Arusha โ€ข Your go-to station for the hottest hits and the latest news! 92.9MHz
Arusha, Tanzania
Contact . +255788163855

MATOKEO mabovu katika mechi mbili mfululizo yamemtibulia Kocha wa Chelsea, Enzo Maresca kwa mashabiki wengi wakitaka aon...
29/09/2025

MATOKEO mabovu katika mechi mbili mfululizo yamemtibulia Kocha wa Chelsea, Enzo Maresca kwa mashabiki wengi wakitaka aondoke, lakini mabosi wa mabingwa hao wa Dunia wamesema bado wanamwamini na watamjadili mwisho wa msimu.

Chelsea ilikumbana na kichapo cha pili mfululizo Ligi Kuu England kutoka kwa Brighton wikiendi iliyopita cha mabao 3-1 nyumbani, baada ya kutoka kuchapwa na Manchester United mabao 2-1 ugenini.

Hata hivyo, licha ya kelele hizo za mashabiki, mabosi wa wababe hao wa darajani, wanaamini kocha huyo bado anaweza akatimiza malengo ambayo wamemwekea na anahitaji kuendelea kupewa muda ili kujenga timu na walishawishika sana kutokana na kiwango ilichoonyesha Chelsea katika michuano ya Kombe la Dunia la Klabu.

Mashabiki walikataa utetezi wa Maresca aliyedai timu imepoteza mechi hizo mbili kwa sababu ya kadi nyekundu, wakidai kadi haikuwa sababu bali kocha huyo ameshindwa na hana kiwango cha kuipa mafanikio timu yao.

Hata hivyo, kadi hizo nyekundu za Robert Sanchez na Trevoh Chalobah zinachukuliwa kwa uzito mkubwa na viongozi wa juu wa klabu ambao wanaamini zimechangia sana timu kufanya vibaya.

Akiwa na Chelsea, Maresca amepoteza mechi tano tu katika miezi sita iliyopita na katika mechi hizo, nne kati ya hizo timu hiyo ilimaliza ikiwa pungufu.

๐…๐”๐‹๐‹ ๐“๐ˆ๐Œ๐„ : CAF CL [ AGG 5-0] YANGA SC 2-0 WILIETE SC โšฝ๏ธ 71โ€ Pacome โšฝ๏ธ 87โ€ Andabwile
27/09/2025

๐…๐”๐‹๐‹ ๐“๐ˆ๐Œ๐„ : CAF CL [ AGG 5-0]

YANGA SC 2-0 WILIETE SC
โšฝ๏ธ 71โ€ Pacome
โšฝ๏ธ 87โ€ Andabwile

Vijana wawili wa Kisomali waliok**atwa wakiwa wanakanyaga bendera ya Kenya katika Uwanja wa Nyayo wakati wa mechi kati y...
27/09/2025

Vijana wawili wa Kisomali waliok**atwa wakiwa wanakanyaga bendera ya Kenya katika Uwanja wa Nyayo wakati wa mechi kati ya Mogadishu City Club dhidi ya Kenya Police FC, wamefikishwa mahak**ani.

Vijana hao wenye umri wa miaka 14 na 17 wanakabiliwa na mashtaka ya kuharibu alama ya kitaifa ya umoja (bendera ya Kenya), na kusababisha vurugu ikiwa ni kinyume cha sheria.

Hata hivyo, Hakimu Mkazi Rose Gitau ameagiza wapelekwe katika kitengo cha Ulinzi wa Watoto cha Gigiri na kuagiza uchunguzi wa kijamii ufanyike kisha ripoti iwasilishwe mahak**ani kabla ya kujibu mashtaka hayo.

Aidha, ndugu wa vijana hao wameomba wawe chini ya ulinzi wao, lakini mahak**a imekataa maombi hayo kwa kuwa si wazazi wao wa damu.

Kocha wa Wiliete ya Angola, Bruno Ferry amesema timu yake haina cha kupoteza kwenye mchezo wa kesho ambapo wataingia na ...
27/09/2025

Kocha wa Wiliete ya Angola, Bruno Ferry amesema timu yake haina cha kupoteza kwenye mchezo wa kesho ambapo wataingia na akili ya kubadilisha matokeo.

Ferry amesema wanatambua matokeo mabaya waliyoyapata nyumbani kwao ambayo yalitokana na uchanga wa kikosi kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, lakini wamejipanga kusahihisha makosa.

Nyota wa Arsenal, William Saliba, anaripotiwa kuwa amekubaliana na mkataba mpya ambao utamuweka klabuni hata baada ya ul...
27/09/2025

Nyota wa Arsenal, William Saliba, anaripotiwa kuwa amekubaliana na mkataba mpya ambao utamuweka klabuni hata baada ya ule wa sasa kumalizika mwaka 2027.
Mfaransa huyo anatarajiwa kusaini rasmi siku chache zijazo, kwa mujibu wa taarifa za The Athletic.

"Katika miaka mitano ijayo tutaanza utekelezaji wa mradi wa kimkakati wa reli ya viwango vya kisasa Mtwara kwenda Mbamba...
26/09/2025

"Katika miaka mitano ijayo tutaanza utekelezaji wa mradi wa kimkakati wa reli ya viwango vya kisasa Mtwara kwenda Mbamba Bay, mpaka kule Mchuchuma na Liganga." - Mgombea Urais wa Tanzania kupitia CCM, Dkt. Samia Suluhu kwenye kampeni Mtwara Mjini

kutoka kwa msemaji wa   amesema yeye ndio msemaji aโ€œMimi ndio Msemaji ninayeisemea timu yenye nidhamu Tanzania ndio maan...
26/09/2025

kutoka kwa msemaji wa amesema yeye ndio msemaji aโ€œMimi ndio Msemaji ninayeisemea timu yenye nidhamu Tanzania ndio maana wikiendi hii Mashabiki wetu wataingia uwanjani kushuhudia burudani. Wapinzani wetu wameingia jana saa 10 jioni tayari kwa mchezo wa hapo kesho majira ya saa 11 katika uwanja wa Mkapa.

โ€œHatupaswi kubweteka kutokana na matokeo yaliyopita. Bila shaka mmewasikia wapinzani wetu wakisema kuwa bado wana imani ya kubadilisha matokeo. Kocha wa timu pinzani bado anayo matumaini makubwa.

โ€œHuu ni mpira wa miguu tunapaswa kuwa makini sana. Mashabiki wetu wanapaswa kujua ni wajibu wetu kujitokeza kwa wingi kesho kuisapoti timu yetu na kufungua Msimu wa Ligi ya Mabingwa kwenye uwanja wa nyumbaniโ€ Ally Kamwe

โ€œTumekuja na kauli mbiu ya ๐Œ๐…๐”๐Œ๐Ž ๐”๐Œ๐„๐Š๐”๐๐€๐‹๐ˆ maalum kwa ajili ya mchezo wa kesho tu. Tuna jambo la tofauti mtaliona kesho ...
26/09/2025

โ€œTumekuja na kauli mbiu ya ๐Œ๐…๐”๐Œ๐Ž ๐”๐Œ๐„๐Š๐”๐๐€๐‹๐ˆ maalum kwa ajili ya mchezo wa kesho tu. Tuna jambo la tofauti mtaliona kesho mkija uwanja wa Mkapa. Kuna moto mkali sana utawashwa kesho.

โ€œUongozi wetu umeweka kiingilio rafiki sana eneo la Mzunguko kuwa ni Tsh 3000 tu, na hii ni kuhakikisha tunakuja kwa wingi tuweze kuishangilia timu yetu. Tiketi kwenye majukwaa mengine ni VIP C 10,000, VIP B 20,000 na VIP A ni 30,000.โ€

Baada ya aliyekuwa KochaMkuu wa Simba Fadlu Davis kuaga kupitia ukurasa wake wa Instagram, na aliyekuwa msaidizi wake Da...
22/09/2025

Baada ya aliyekuwa KochaMkuu wa Simba Fadlu Davis kuaga kupitia ukurasa wake wa Instagram, na aliyekuwa msaidizi wake Darian Wilken ameaga kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Ameandika:

โ€œSi rahisi kuaga, hasa kwa klabu maalum k**a Simba SC. Kwa muda wangu hapa, nimekuwa na fursa ya kufanya kazi pamoja na sio tu wachezaji wazuri lakini pia klabu nzima na jumuiya ambayo ina shauku, uthabiti, na tamaaโ€.

โ€œMsimu uliopita ulikuwa ni safari ya ajabu ya kuacha alama, sa-fari iliyojaa changamoto, ukuaji, na nyakati zisizoweza kusahaulika uwanjaniโ€.

โ€œKwa wachezaji, ninataka kuwashukuru kwa kujitolea kwenu, bidii yenu, na imani yenu katika mchakato huu. Siku baada ya siku, ulitoa kila kitu, na ilionyesha jinsi tulivyofanya pamoja k**a kitengo. Imekuwa heshima kuwa sehemu ya safari yako na kushiriki katika ushindi na masomo njianiโ€.

โ€œKwa klabu na wafuasi wake, natoa shukrani zangu za dhati kwa imani iliyowekwa kwangu na kwa uchangamfu ambao nilikaribishwa nao. Simba SC ni zaidi ya timu; ni familia, na ku-wa sehemu ya familia hiyo imekuwa uzoefu ambao ni-taendelea kuwa nao daimaโ€.

โ€œNinapochukua hatua inayofuata katika njia yangu, ni-naondoka bila chochote ila heshima na shukrani kwa kile tuli-chofanikiwa pamoja. Siku zote nitajivunia kuwa sehemu ya Simba SC na nitaendelea kuifuatilia na kuiunga mkono klabu hiyo kwa masikitiko makubwaโ€.

โ€œAsante sanaโ€.

Hatimaye aliyekuwa Kocha wa Simba, Fadlu Davids ameaga rasmi baada ya tetesi kusambaa katika mitandao ya kijamii na kuto...
22/09/2025

Hatimaye aliyekuwa Kocha wa Simba, Fadlu Davids ameaga rasmi baada ya tetesi kusambaa katika mitandao ya kijamii na kutoonekana kwake timu ikirudi kutoka Botswana ilipokwenda kucheza dhidi ya Gaborone United mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Kupitia ujumbe alioandika kocha huyo katika ukurasa wake wa Instagram unakamilisha tetesi za kuondoka kwake klabuni hapo na kuwa taarifa rasmi japo klabu ya Simba bado haijatoa taarifa rasmi kumhusu.

Katika ujumbe aliouchapisha Fadlu muda mchache uliopita, amewashukuru mashabiki, viongozi na wachezaji kwa kipindi alichokuwa klabuni hapo japo akikiri ni ngumu kuaga.

Ameandika; โ€œNi kwa moyo mzito naiaga Simba SC.

Tangu nilipowasili, nilihisi shauku ya klabu hii kubwa na upendo wa mashabiki wake wa ajabu. Kwa pamoja tulipigana, kusherehekea, na kuimarika kupitia kila ushindi na kila changamoto.

Shukrani zangu za dhati kwa Rais Mo Dewji kwa uongozi wake wa kutia moyo, maono, na msaada wake wa kila mara.

Kwa wachezaji: endelea kupigana, endelea kuamini, na endelea kuinua beji kwa heshima.

Kwa wafanyikazi na wasimamizi: asante kwa uaminifu wako na kujitolea bila kuchoka nyuma ya pazia.

Kwa mashabiki wa Simba: wewe ndiye mapigo ya moyo wa klabu hii. Sauti zako, nyimbo zako, shauku yako isiyoyumba zitasikika katika kumbukumbu yangu. Asante kwa kukaribisha familia yangu k**a yako.

Simba daima itakuwa sehemu yangu, na ninaitakia klabu mafanikio, mafanikio na vikombe mbeleni.
Asanteni Sana, forever Nguvu Moja โค๏ธ๐Ÿฆ

Kocha Fadlu Davidsโ€

Fadlu amedumu Simba kwa siku 444 tangu alipojiunga nayo Julai 5, 2024 akitokea Raja Athletic Club, amefanikiwa kuifikisha timu hiyo kwenye fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika, licha ya kushindwa kutwaa ubingwa huo.

Dkt. Samia awasili Tunduru kunadi sera za CCMMgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduz...
22/09/2025

Dkt. Samia awasili Tunduru kunadi sera za CCM

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Samia Suluhu Hassan, amewasili katika Uwanja wa CCM wilayani Tunduru mkoani Ruvuma ambako ananadi sera za CCM kuelekea uchaguzi mkuu utakaofanyika mwezi Oktoba mwaka huu.

Dkt. Samia anahitimisha ziara ya kampeni katika Mkoa wa Ruvuma kwa kuzungumza na wananchi wa Tunduru ambapo kesho Septemba 23, 2025 anatarajiwa kubisha hodi katika Mkoa wa Mtwara ambako ataendelea na shughuli k**a hiyo.

Mahak**a Kuu ya Tanzania Masijala Ndogo ya Dar es Salaam imetupilia mbali mapingamizi ya Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Li...
22/09/2025

Mahak**a Kuu ya Tanzania Masijala Ndogo ya Dar es Salaam imetupilia mbali mapingamizi ya Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu ya kutaka aachiwe huru kutokana na ubatili wa hati ya mashtaka.

Uamuzi huo umetolewa leo na Jopo la majaji, wakiongozwa na Jaji Dunstan Ndunguru ambaye alisema pingamizi la kwanza la Lissu lilishatolewa uamuzi mapema na kwamba pingamizi lililosalia lilihusu uhalali wa hati ya mash*taka pamoja na hoja ya kwamba viambatanisho na maelezo ya mashahidi hayakuwa sahihi.

Kuhusu hoja ya kwamba hati ya mashtaka ilifanyiwa marekebisho, Jaji Ndunguru alisema hakuna ushahidi unaoonesha hivyo kwani hati iliyosomwa mbele ya msh*takiwa ndiyo hiyo hiyo iliyowasilishwa Mahak**a Kuu bila mabadiliko.

Kutokana na hatua hiyo, mahak**a imesema mapingamizi yote hayana msingi wa kisheria hivyo yanatupiliwa mbali.

Lissu, ambaye anakabiliwa na mashtaka ya uhaini, alidai kuwa hati ya mashtaka ni batili kwa kuwa haioneshi maelezo ya kosa wala nia ya kutenda kosa la uhaini ambayo ni viini muhimu katika hati ya mashtaka.

Address

AICC
Arusha

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Mega fm Arusha posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share

Category