
28/01/2025
YAKO MPENDWA,
Nataka nishare na wewe kuhusu kuinuwa viwango vya imani.
1.Ukiona majaribu,changamoto,misukosuko,/mapito yamezi fahamu kuwa wokovu wako umekaribia
2.Ukiona unapitia hayo na huoni msaada,hapo anza kuikaza misuli ya kuamini kwako kuhusu MUNGU
3.Ukiona k**a dunia imekutenga fahamu kuna MUNGU haja kutenga
4.Ukipitia kipindi hicho usikate tamaa ikaze misuli yako ya imani
5.Kuna wakati unaweza ukakiona kichuguu ukazani ni mlima,usiione kuwa changamoto yako kuwa ni special no, bali ichukulie kuwa ni ya kawaida tu
6.Ukipitia jambo ukahisi na kuona kuwa ni zito,inua kiwango chako cha kuamini hilo linapita tu na wala halitadumu kwako
7.Ukipitia jaribu faham kuwa liko ndani ya uwezo wa utatuzi wako
8.Tambua kila jaribu halikosi mlango wa kutokea hilo litapita tu
9.Fahamu jaribu huimarisha misuli ya imani,dhahabu ili ing'ae lazima ipitishwe kwenye moto
10.Tambua mtungi wa mfinyazi ili uhifadhi maji lazima upitishwe kwenye moto.
ACHA KUOGOPA ANZA KUAMINI WEWE NI MSHINDI