29/04/2026
Aprili 27, 2026 — Katika Kikao cha 17 cha Bunge, Mbunge wa Jimbo la Butiama, Dkt. Wilson Mahera, aliuliza swali kuhusu usambazaji wa maji katika mradi wa Mugango–Kiabakari–Butiama kwa wananchi wa jimbo hilo.
Dkt. Mahera alisema kipaumbele kilipaswa kutolewa kwa vijiji 10 ambavyo ni Kisamwene, Busirime, Masurura, Kitasakwa, Ryamisanga, Kamugendi, Kyankoma, Kwisaro, Isaba na Nyanza ili wananchi waweze kupata huduma ya maji safi na salama.