M-Boys Africa tv

  • Home
  • M-Boys Africa tv

M-Boys Africa tv News for everybody

Klabu ya Simba Sc imethibitisha kumsajili mshambuliaji Seleman Mwalimu ‘Gomez’ kwa mkataba wa mkopo wa mwaka mmoja akito...
28/08/2025

Klabu ya Simba Sc imethibitisha kumsajili mshambuliaji Seleman Mwalimu ‘Gomez’ kwa mkataba wa mkopo wa mwaka mmoja akitokea Wydad Casablanca ya Morocco.
Mwalimu (19) raia wa Tanzania aliyejiunga na Wydad mnamo Januari 2025, akitokea Singida Black Stars baada ya kuonesha kiwango bora wakati akiitumikia Fountain Gate Fc kwa mkopo kutoka Singida Black Stars na kufunga magoli 6 kwenye nusu ya kwanza ya msimu wa 2024/25.
Ikumbukwe kuwa mkataba huo hautakuwa na kipengele cha kumnunua endapo utafikia mwisho

Mtangazaji wa Televisheni ya Al Ahly Mohammed Saied alimuuliza Fadlu Davids: "Je! Ni siri gani nyuma ya kushikilia kambi...
28/08/2025

Mtangazaji wa Televisheni ya Al Ahly Mohammed Saied alimuuliza Fadlu Davids: "Je! Ni siri gani nyuma ya kushikilia kambi huko Misri?"
Fadlu Davids alijibu:
"Angalia Ligi ya Mabingwa wa CAF na uone ni timu ipi iliyofanikiwa zaidi, utapata Al Ahly. Ndio sababu nataka kupata uzoefu huo na kushindana dhidi ya wapinzani sawa, kuelewa siri ya mafanikio yao. Pamoja na hayo, Misri ni nzuri na watu wake ni rafiki sana."

Ft 'Azam FC ya funga mashindano ya msimu wa mapema wa APR FC katika nafasi ya 2 baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya mwenyej...
24/08/2025

Ft '
Azam FC ya funga mashindano ya msimu wa mapema wa APR FC katika nafasi ya 2 baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya mwenyeji APR usiku wa leo. 🔥
Kocha Florent Ibenge atakuwa anatarajia hii ni mwanzo tu wa msimu mkubwa kwa watengenezaji wa ice cream!

Klabu ya JKT Tanzania imeitaarifu klabu ya Simba SC kuwa walipe pesa walizokubaliana kwa muda uliopangwa na nyongeza ya ...
24/08/2025

Klabu ya JKT Tanzania imeitaarifu klabu ya Simba SC kuwa walipe pesa walizokubaliana kwa muda uliopangwa na nyongeza ya wachezaji watatu na ikiwa hawatatekeleza hayo wao watavunja usajili na kuwabakisha wachezaji wao ambao ni Wilson Nangu na Yakoub Suleiman
David Kameta, Valentino Mashaka na Awesu Awesu wanatakiwa na JKT Tanzania ili uhamisho wa beki Wilson Nangu na golikipa Yakoub Suleiman ukamilike kuelekea msimu ujao

24/08/2025

Manchester United wameendelea na mwanzo wao wa kusuasua msimu huu, United wamepata matokeo mabovu dhidi ya Fulham na hatimaye wakinusurika kwa sare ya ya 1-1.....
Huku Staa wao "BrunoFernandes" akikosa mkwaju wa Penati kipindi cha kwanza.....
Umeonaje kiwango cha Man United??

Send a message to learn more

Kiungo mshambuliaji mpya wa klabu ya Simba Neo Maema,ameeleza jinsi alivyoifahamu klabu hiyo na kusema alikuwa anaifaham...
24/08/2025

Kiungo mshambuliaji mpya wa klabu ya Simba Neo Maema,ameeleza jinsi alivyoifahamu klabu hiyo na kusema alikuwa anaifahamu,lakini aliifuatilia zaidi msimu uliopita walipokuwa wanacheza na klabu ya Stellenbosch ya Afrika kusini nyumbani na ugenini kwenye hatua ya nusu fainali ya kombe la shirikisho barani Afrika,na kuimwagia sifa kuwa ilicheza vizuri sana licha ya kuwa baadae walitolewa katika hatua ya fainali na klabu ya Rs Berkane.
Kiungo huyo ameongeza kwa kusema uzoefu alioupata akiwa katika klabu ya mamelodi atauleta katika timu yake mpya ya Simba.
Alisema "Ni heshima kubwa sana kwangu na familia yangu kuwa nahodha wa timu ya taifa ya Afrika kusini na uzoefu nilioupata Mamelodi nitauleta Simba” Amesema Neo Maema kwenye mahojiano maalum na

Mtoko wa Yanga unaupa asilimia ngapi????
24/08/2025

Mtoko wa Yanga unaupa asilimia ngapi????

Albamu mpya ya CICI inayozunguka CICI imefikia homa ya homa, shukrani kwa moja ya mshangao wake wa kufurahisha zaidi - u...
24/08/2025

Albamu mpya ya CICI inayozunguka CICI imefikia homa ya homa, shukrani kwa moja ya mshangao wake wa kufurahisha zaidi - ushirikiano wake na Diamond Platnumz wa Tanzania.
Duo alijiunga na Vikosi vya Chini, wimbo wa upendo wa kitamaduni ambao unachanganya mizizi ya R&B ya Ciara na nyimbo za Diamond na saini za bongo flava.
Ingawa Low hakuonekana kwenye toleo la kawaida la 14 la CICI, lililotolewa kimataifa mnamo Agosti 22, 2025. Mashabiki waliopata hakiki za moja kwa moja na viunzi vya media vya kijamii wanaamini kuwa itaongoza toleo linalokuja la Deluxe.
Akiongea kwenye Klabu ya Kiamsha kinywa, Ciara alikuwa amejaa sifa kwa mshirika wake wa Afrika Mashariki. "Diamond ni dope," alisema, na kuongeza, "vibe ilikuwa sawa. Alileta nguvu nyingi na ukweli kwenye rekodi. Ninapenda kuchunguza sauti mpya na kuungana na tamaduni tofauti, na wimbo huu unahisi kuwa maalum."

Lionel Ateba Mbida amesaini mkataba wa miaka miwili (2) yakuitumikia klabu ya Al - Shorta ya nchini Iraq 🇮🇶. _ Klabu ya ...
24/08/2025

Lionel Ateba Mbida amesaini mkataba wa miaka miwili (2) yakuitumikia klabu ya Al - Shorta ya nchini Iraq 🇮🇶.
_ Klabu ya Simba SC kwa deal hilo wamepata $300,000 ambayo ni sawa sawa na Million 740 za kitanzania.
_ Al shorta msimu Jana yaani 2024/2025 walimaliza nafasi ya kwanza (1) na alama 87 hivyo Timu hio itashiriki kombe la mabingwa barani Asia ( Asia Champions league )

24/08/2025

Kylian Mbappé amefunga magoli mawili huku Vinicius Junior akifunga moja na kusaidia 'assist' lingine wakati Real Madrid ikiilaza Real Oviedo 3-0 katika dimba la Nuevo Carlos Tartiere
FT: Real Oviedo 0-3 Real Madrid
⚽ 37' Mbappé (🅰️ Arda Guler)
⚽ 83' Mbappé (🅰️ (Vinicius Jr)
⚽ 90+3' Vinicius Jr (🅰️ Brahim Diaz)

Address


Alerts

Be the first to know and let us send you an email when M-Boys Africa tv posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to M-Boys Africa tv:

  • Want your business to be the top-listed Media Company?

Share