Jamvi la habari

Jamvi la habari Gazeti Bora la Kiswahili lenye kuhabarisha, kuelimisha, kuburudisha na Kufunza. Tuwasiliane kupitia :

Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mwenyekiti Mstaafu wa CHADEMA Freeman Mbowe wakati wa uzinduz...
17/07/2025

Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mwenyekiti Mstaafu wa CHADEMA Freeman Mbowe wakati wa uzinduzi wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete Convention center (JKCC) Mkoani Dodoma leo July 17,2025.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa pamoja na viongozi mbalimbali kwenye hafla ...
17/07/2025

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa pamoja na viongozi mbalimbali kwenye hafla ya uzinduzi wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 iliyofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete (JKCC) Jijini Dodoma tarehe
17 Julai, 2025.

Mwenyekiti Mstaafu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Freeman Mbowe, ni miongoni mwa Wageni wanaoshiriki kwe...
17/07/2025

Mwenyekiti Mstaafu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Freeman Mbowe, ni miongoni mwa Wageni wanaoshiriki kwenye uzinduzi wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 leo Julai 17, 2025 katika Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete (JKCC) Jijini Dodoma, ambapo Mgeni rasmi ni Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Mbowe hajaonekana hadharani kwenye shughuli za kisiasa na kijamii tangu alipostaafu na kutangaza anapumzika.

Powered by: 🍺

17/07/2025
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa viongozi kwa nafasi mbalimbali.Kwa ...
16/07/2025

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa viongozi kwa nafasi mbalimbali.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jioni hii Julai 16 na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Moses Kusiluka, viongozi walioteuliwa ni Omari Juma Mkangama kuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Ludewa, Juma Abdallah Njeru kuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Mpanda na Bi. Hellen Emmanuel Mwambeta kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Siha.

Wengine ni Francis Genes Kafuku ameteuliwa kuwa
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu, Dkt. Adam Omar Karia ameteuliwa kuwa Mkuu wa Chuo cha Maji kwa kipindi cha pili, Balozi Dkt. Aziz Ponary Mlima ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalum ya Kiuchumi (TISEZA),
Rais pia amemteua Jenerali Mstaafu Venance Salvatory Mabeyo ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro kwa kipindi cha pili, Dkt.
Harrison George Mwakyembe ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) kwa kipindi cha pili.

Aidha, Filbert Michael Mponzi ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Bodi ya Sukari Tanzania kwa kipindi cha pili na Dkt. Leonada Raphael Mwagike ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Kudhibiti Ununuzi wa Umma (PPRA) kwa kipindi cha pili.

16/07/2025

Mtoto wa kitanzania aliyeonesha uwezo wake kujenga miundombinu ya baadhi ya sehemu za Tanzania

Mtazamo wako ni nini kuhusu kipaji hiki cha mtoto huyu?

✍🏼

Siku ya leo wakati Lamine Yamal anaenda kutambulishwa kuwa mchezaji atakayevaa jezi No 10 kuanzia msimu ujao Barcelona a...
16/07/2025

Siku ya leo wakati Lamine Yamal anaenda kutambulishwa kuwa mchezaji atakayevaa jezi No 10 kuanzia msimu ujao Barcelona aliongozana na Bibi yake pamoja na wazazi wake wote

Powered by: 🍺

✍🏼

SERIKALI YAJA NA MKAKATI WA KUWAWEZESHA WAZALISHAJI CHUMVI NCHINI▪️Serikali kupunguza ada ya kodi ya pango kwa mwaka kwa...
16/07/2025

SERIKALI YAJA NA MKAKATI WA KUWAWEZESHA WAZALISHAJI CHUMVI NCHINI

▪️Serikali kupunguza ada ya kodi ya pango kwa mwaka kwa Leseni ya chumvi

▪️Rais Samia apongezwa kwa kiwanda cha kusafisha chumvi Lindi

▪️Wazalishaji wa chumvi wafurahia kuanza kwa kodi ya zuio

▪️Serikali kudhibiti uingizaji wa chumvi kiholela nchini

*Dar es Salaam*

Katika kuwajengea uwezo wazalishaji wa chimvi nchini,Serikali imekuja na mikakati mbalimbali kufikia azma hiyo ikiwemo upunguzaji wa ada ya pango kwa mwaka ya leseni (Annual Rent) za uchimbaji mdogo wa chumvi nchini ili kusaidia kupunguza gharama za uzalishaji na kuchochea uzalishaji wa wingi wa chumvi nchini.

Hayo yamesemwa jana tarehe 15 Julai, 2025 na Waziri wa Madini, *Mheshimiwa Anthony Mavunde (Mb)* Jijini Dar es Salaam alipokuwa akifunga Kikao cha wadau wa sekta ndogo ya chumvi chini ya Chama cha Wazalishaji wa Chumvi Tanzania (TASPA).

“*Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan* ameendelea kutubeba sekta ya madini na wachimbaji kwa ujumla. Ni yeye aliyetuelekeza kusikilize kilio chenu na kutatua changamoto zinazowakabili ili mnufaike na shughuli mnazofanya”

“Ametuelekeza Wizara ya Madini tuliridhie ombi lenu na kupunguza ada ya pango ya mwaka ya leseni ya uchimbaji mdogo kutoka Shilingi 45,000 mpaka Shilingi 20,000 kwa hekta, hili linakwenda kupunguza gharama za uzalishaji na kuongeza ubora wa chumvi ya mzalishaji mdogo” alieleza Mhe. Mavunde.

Aidha, *Waziri Mavunde* alibainisha kuwa hatua mbalimbali zinazochukuliwa na Serikali ikiwemo udhibiti wa chumvi inayoingizwa kutoka nje ya nchi, zimepelekea bei ya chumvi ghafi kuongezeka na hivyo kuwanufaisha zaidi wazalishaji wadogo wa chumvi nchini.

Uanzishwaji wa kodi ya zuio ya asilimia mbili (2%) kwenye mauzo ya chumvi ghafi kwa wazalishaji wenye leseni za PML imekuwa ni neema na manufaa kwao badala ya utaratibu wa awali wa kufanyiwa makadirio ya kodi ya mapato, ambao ulikuwa ni kero kubwa kwa wazalishaji wadogo.

Leo hii katika gazeti la JAMVILAHABARI
16/07/2025

Leo hii katika gazeti la JAMVILAHABARI

Winga wa Man City Jeremy Doku raia wa Belgium mwenye asili ya Ghana anabarikiwa na Asantehene - Mtawala wa Ufalme wa Ash...
15/07/2025

Winga wa Man City Jeremy Doku raia wa Belgium mwenye asili ya Ghana anabarikiwa na Asantehene - Mtawala wa Ufalme wa Ashanti nchini Ghana anayeitwa Otumfuo Osei Tutu II

Powered by: 🍺

✍🏼

Mchezaji wa Simba Sc Mohamed Hussein ameondoa utambulisho wake wakuwa mchezaji wa Simba Sc kwenye bio yake ya Instagram ...
15/07/2025

Mchezaji wa Simba Sc Mohamed Hussein ameondoa utambulisho wake wakuwa mchezaji wa Simba Sc kwenye bio yake ya Instagram

Hapo awali Mohamed Hussein kwenye ukurasa wake wa Instagram kwenye bio yake aliandika yupo chini ya Simba Sc ila sasa ameondoa utambulisho huo

Nini mtazamano wako kuhusu hili jambo la Mohamed Hussein?

Powered by: 🍺

✍🏼

Kiongozi wa Ngome ya Vijana Taifa Chama cha ACT Wazalendo, Abdul Omary Nondo, maarufu Abdul Nondo, amechukua fomu ya kuo...
15/07/2025

Kiongozi wa Ngome ya Vijana Taifa Chama cha ACT Wazalendo, Abdul Omary Nondo, maarufu Abdul Nondo, amechukua fomu ya kuomba kuteuliwa na chama chake kugombea ubunge Jimbo la Kigoma Mjini katika mchaguzi mkuu ujao.

Nondo amekabidhiwa fomu hiyo leo, Julai 15, 2025, na Katibu wa chama hicho wa Jimbo la Kigoma Mjini, Idd Adamu.

Hii ni mara yake ya pili kutangaza nia ya kugombea ubunge katika jimbo hilo, ambapo, k**a ilivyokuwa katika Uchaguzi Mkuu wa 2020, atachuana tena na mbunge wa zamani wa jimbo hilo, Zitto Kabwe, ambaye alichukua fomu mapema Aprili 18, 2025.

Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa fomu, alisema:”Naamini safari hii wajumbe na chama changu watanipa ridhaa ya kupeperusha bendera katika jimbo hili, kwa lengo la kurejesha hadhi ya Kigoma Mjini.

“Jimbo hili si sehemu ya kutafuta sifa wala umaarufu; watu wa Kigoma wana uelewa wa kutosha na wanajua ni nani anayefaa kuwaongoza.”

Ni rasmi sasa Nondo atachukuana na wanaCCM waliotia nia ubunge wa kigoma mjini ambao ni Baba Levo,Baruani n.k

Powered by: 🍺

Address

Dar Es Salaam

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Jamvi la habari posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Jamvi la habari:

Share

SGR

"Miaka 120 ikiyopita Wakoloni waliona umuhinu wa kujenga reli na sisi kuelekea uchumi wa viwanda tunajenga Reli ya SGR huwezi kutenganisha Viwanda na Reli"-Masanja Kadogosa Mkurugenzi TRC