
15/07/2025
PSG KUVUNJA REKODI: OFA YA €250M KWA COLE PALMER YAWEKA HISTORIA MPYA YA USAJILI!
Kwa mujibu wa taarifa za hivi karibuni, Paris Saint-Germain (PSG) wanapanga kutoa ofa ya kuvunja rekodi ya dunia ya €250 milioni ili kumnasa kiungo Mshambuliaji wa Chelsea, Cole Palmer. Hii ni zaidi ya ofa ya awali ya €200 milioni ambayo PSG walikuwa tayari kuwasilisha kwa Chelsea. Kwa sasa, Chelsea wameweka bei ya €250 milioni kwa Palmer, wakionyesha kuwa hawako tayari kumuuza kwa kiasi chochote chini ya hicho.
Cole Palmer, ambaye alijiunga na Chelsea kutoka Manchester City mnamo 2023 kwa ada ya £40 milioni, aliibuka kuwa Mchezaji muhimu katika kikosi cha The Blues. Katika msimu wa 2024/25, alifunga mabao 27 na kutoa pasi 15 za mabao katika mashindano yote, akichangia kwa kiasi kikubwa mafanikio ya Chelsea kushinda UEFA Conference League na FIFA Club World Cup.
Kwa sasa, mashabiki wa soka wanapaswa kusubiri kuona ikiwa PSG wataweza kuvunja Benki na kumshawishi Chelsea kumuuza Nyota wao.
Toa maoni yako