HB_TV HABARI ZA MASTAA WOTE UTAZIKUTA HAPA
�Kwa Matangazo
�Kwa Exclusive
�Kwa Habari
�: (+255) 738467864 |Email: [email protected]
���

WANAHABARI WAHAMASISHWA KURIPOTI MAGEUZI KATIKA SEKTA YA KILIMOWanahabari wametakiwa kuhabarisha Umma mageuzi makubwa ya...
28/03/2026

WANAHABARI WAHAMASISHWA KURIPOTI MAGEUZI KATIKA SEKTA YA KILIMO

Wanahabari wametakiwa kuhabarisha Umma mageuzi makubwa yanayofanywa na Serikali katika Sekta ya Kilimo ili wananchI wanufaike na fursa zinazopatika katika mnyororo mzima wa thamani wa sekta hiyo.

Ametoa wito huo Naibu Katibu Mkuu anayesimamia Zana za Kilimo na Umwagiliaji, Mha. Athumani Kilundumya alipokutana na wawakilishi wa magazeti ya “The Guardian na Nipashe”; na Kampuni ya Magazeti ya Serikali - TSN inayoendesha “Daily News na Habari Leo”.

Mazungumzo hayo yamefanyika tarehe 27 Machi 2026 katika moja ya kumbi ndogo za Wizara ya Kilimo zilizopo Mtumba, jijini Dodoma, ambapo Naibu Katibu Mkuu Mha. Kilundumya amewashukuru wawakilishi hao kwa ushirikiano na kuwataka kuimarisha kazi zao katika mitandao ya kijamii kwa kutoa elimu kwa wananchi kuhusu shughuli za Serikali katika sekta mbalimbali ikiwemo ya kilimo ili kuepuka mitazamo hası ambayo haina tija katika kujenga Taifa.

Aidha, Mha. Kilundumya ameeleza kuwa Serikali ya Awamu ya Sita, Awamu ya Pili chini ya Uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan inaendelea kuchukua hatua mbalimbali za kuimarisha Sekta ya Kilimo, ikiwemo ununuzi wa vifaa vya uchimbaji visima na uanzishwaji wa vituo vya zana za kilimo, hatua inayolenga kuongeza tija na upatikanaji wa huduma kwa wakulima nchini.

Kwa upande wake, Mhariri Mtendaji wa gazeti la The Guardian / Nipashe, Bi. Salome Kitomari ameishukuru Wizara kwa ushirikiano unaoendelea na kuahidi kuudumisha kwa manufaa ya pande zote.

Naye Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara kutoka Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN), Bi. Soter Salema, ameeleza kuwa TSN ipo tayari kukuza ushirikiano kwa kuitangaza Sekta ya Kilimo na mafanikio yake kwa Umma ikiwa ni pamoja na kushirikiana na Wizara katika maeneo mengine yenye kuleta tija kwa wakulima na wananchi kwa ujumla.

KUIMARISHA UBORA WA ELIMU: WALIMU WA AMALI ZA KIHANDISI KUNOLEWA INDIATanzania imeandika ukurasa mpya katika historia ya...
27/03/2026

KUIMARISHA UBORA WA ELIMU: WALIMU WA AMALI ZA KIHANDISI KUNOLEWA INDIA

Tanzania imeandika ukurasa mpya katika historia ya elimu ya ufundi kwa kupeleka walimu 150 wa Amali za Kihandisi nchini India.

Hatua hii kubwa ya kimkakati siyo tu safari ya mafunzo, bali ni uwekezaji wa kitaifa katika mustakabali wa elimu na uchumi wa viwanda, ikilenga kuongeza umahiri wa walimu na kuandaa kizazi cha wataalamu watakaoshindana kimataifa katika nyanja za teknolojia na uhandisi.

Zimesalia siku chache kabla ya kufikiwa kwa ukomo wa usajili wa hiari kwa taasisi zinazokusanya na kuchakata taarifa bin...
26/03/2026

Zimesalia siku chache kabla ya kufikiwa kwa ukomo wa usajili wa hiari kwa taasisi zinazokusanya na kuchakata taarifa binafsi nchini. Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC) imetangaza kuwa ifikapo tarehe 9 Aprili mwaka huu, itaanza kuchukua hatua kali za kisheria ikiwemo faini ya hadi shilingi bilioni tano kwa taasisi zitakazokiuka taratibu hizo.

Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC) leo Machi 26, 2026 imetoa msisitizo wa mwisho kwa taasisi zote za umma na binafsi nchini, ikizikumbusha kuwa muda wa usajili wa hiari unafikia tamati tarehe 8 Aprili, 2026.

Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari, Mkurugenzi Mkuu wa Tume hiyo, Dkt. Emmanuel Lameck Mkilia, amesema kuwa serikali imetoa muda wa kutosha tangu mwaka 2024 ili kutoa fursa kwa taasisi kujipanga.

“Serikali ilitoa muda wa kutosha wa kujisajili. Muda huo ulianza Aprili 2024 wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan alipozindua Tume. Muda uliongezwa mara mbili, mara ya mwisho ikiwa ni uamuzi wa Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Angellah Jasmine Mbelwa Kairuki, ambaye aliweka tarehe ya mwisho kuwa tarehe 8, Aprili, mwaka huu” amesema Dkt. Mkilia

Dkt. Mkilia amebainisha kuwa, kuanzia tarehe 9 Aprili, 2026, utekelezaji wa Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi Sura ya 44 utaanza rasmi, na taasisi yoyote itakayobainika kutokujisajili kwenye mfumo wa PDPC itawajibika kisheria.

“Kwa mujibu wa Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi, adhabu kwa mtu binafsi ni faini ya kuanzia Shilingi za kitanzania laki moja hadi Milioni 20 au kifungo cha hadi miaka 10 jela. Kwa upande wa taasisi na makampuni, adhabu ni faini kuanzia Shilingi Milioni moja hadi kufikia kiasi cha Shilingi Bilioni Tano za kitanzania, kulingana na aina ya ukiukwaji.

Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi inazigusa sekta zote muhimu zikiwemo Wizara na idara za Serikali, mabenki, kampuni za bima, hospitali, shule, vyuo, kampuni za simu, viwanda, sekta ya utalii, hoteli, kampuni za usafirishaji, kampuni za ujenzi, vyama vya siasa, vyama vya wafanyakazi, jumuiya za kidini, mashirika yasiyo ya kiserikali na taasisi nyingine nyingi.

Sheria hii ni ngao kwa mwananchi ambaye ndiye muhusika wa taarifa, kwani inalinda haki ya msingi ya faragha. Aidha, inajenga imani kati ya watoa huduma na wateja wao, jambo ambalo ni nguzo muhimu katika kukuza uchumi wa kidigitali na uwekezaji nchini.
=====================================

hakikisha una follow account yetu hii kuanzia sasa kwa habari mpya za kila siku

Konde na Kajala katika Track moja, Tuipe asilimia ngapi video hii?

✍️ Cc:

25/03/2026

hakikisha una follow account yetu hii kuanzia sasa kwa habari mpya za kila siku

Huu ujumbe wa Mwanamke kwa wanawake wenzake umekaa vipi ndugu zangu? 🙌

✍️ Cc:

K**ati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo imepitisha randama ya mpango na makadirio ya bajeti ya matumizi...
25/03/2026

K**ati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo imepitisha randama ya mpango na makadirio ya bajeti ya matumizi ya kawaida pamoja na mpango wa maendeleo kwa mwaka wa fedha 2026/2027 wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.

Mpango huo umepitishwa na k**ati Machi 24, 2026 chini ya Mwenyekiti wa K**ati hiyo, Mhe. Husna Sekiboko, ambae amesema mpango huu unakwenda kuwa chachu ya kuandaa vijana wenye ujuzi.

Mhe. Sekiboko amesisitiza kuhakikisha mtiririko wa fedha utakaowezesha miradi yote ya maendeleo inatekelezwa na kukamilika kwa wakati.

"Kwa kweli tumeshuhudia miradi mingi mikubwa mizuri ambayo inajenga imani ya wananchi kwa Serikali na kuongeza tija katika maendeleo" amesema Mhe. Sekiboko.

Pia ameiomba Wizara kushirikiana kwa Karibu na Wizara ya Fedha kuhakikisha fedha za miradi ya maendeleo kwa sekta ya elimu zinatolewa kwa wakati, na kwa mtiririko unaowezesha utekelezaji wenye ufanisi.

Kwa upande wake, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda, amewashukuru wajumbe wa K**ati hiyo kwa kupokea na kupitisha randama ya bajeti ya Wizara na ameahidi kuwa wizara itaendelea kuboresha mifumo na mazingira ya utoaji elimu ili kuhakikisha kila mtoto wa Kitanzania anapata elimu na ujuzi kwa usawa na ujumuishi.

21/03/2026
19/03/2026
18/03/2026

Address

Ubungo
Dar Es Salaam
14104

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when HB_TV posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to HB_TV:

Share

Category