18/06/2026
Katibu wa NEC- Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM, Kenani Kihongosi, amewasili leo Juni 18, 2026, katika Kata ya Ruaha Mbuyuni, Wilaya ya Kilolo mkoani Iringa, kuanza ziara yake ya siku nne mkoani hapa
Mara baada ya kuwasili, Kihongosi alipokelewa na viongozi wa CCM katika shina namba 10 pamoja na wananchi wa Ruaha Mbuyuni, na kupokea taarifa za uhai wa chama na kukagua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika eneo hilo.
Ziara ya Kihongosi mkoani Iringa imeanza leo Juni 18 hadi 21, 2026, ikiwa na lengo la kuimarisha chama, kusikiliza wananchi na kuhamasisha amani, mshikamano na ushiriki wa wananchi katika shughuli za maendeleo.