14/04/2025
BARUA YA WAZI KWA UMMA WA WATANZANIA.
✍️ Anaandika Onesmo Mushi.
Ninaamini nyote ni wazima wa afya. Nina swali kwetu sote siku ya leo; JE, TUTAENDELEA KURUHUSU HAYA MPAKA LINI?
Mwaka 2019 tulitumia zaidi ya billioni 80 uchaguzi wa serikali za mitaa.
2020 tukatumia zaidi ya billion 300 uchaguzi mkuu.
2024 tumetumia zaidi ya billion 100 uchaguzi wa serikali za mitaa.
2025 tuna uhakika wa kutumia zaidi ya billioni 500.
Chaguzi zote hizi wala hazikufanyika (wote tunafahamu mwisho wa story ya 2025), ni sahihi zaidi kuziita UTEUZI.
Wakati tunatapanya kiasi hiki cha pesa kugharamia upumbavu, Tanzania ni nchi ya 167 kati ya nchi 183 kwenye human capital development index ya 2024.
Yani Tanzania ni moja kati ya nchi 20 za mwisho duniani kwa kuwa na watu waliodumaa kimaendeleo.
Wala hauhitaji sayansi ya anga kulithibitisha hili, unless umechagua kuwa mpumbavu.
Mpaka leo tuna watoto wanakaa chini kwenye shule za msingi na sekondari katikati ya jiji la Daresalaam kwa kukosa madawati, achana na zile za vijijini.
Mpaka leo era ya artificial intelligence shule zetu za msingi na sekondari za umma nchi nzima zina wastani wa kompyuta moja moja tu.
Wakati watoto wa viongozi wanasoma international schools k**a Feza wanakopata kila aina ya luxury kwa gharama ya kodi yako, kila mwalimu mmoja kwenye shule za umma anafundisha watoto zaidi ya 200.
Vitabu ni anasa kwenye shule za umma, masomo pekee yenye vitabu vingi ni masomo ya lugha ya kiingereza na hisabati ambayo yenyewe ndio angalau kitabu kimoja kinagombaniwa na wastani wa watoto wanne. Masomo mengine tulishamwachia Mungu, hayafai hata kuzungumzia.
Mpaka hivi tunavyoongea mtoto wa mtanzania maskini hana uhakika wa kuishi akiwa na afya tele kwa sababu serikali yetu pendwa iliondoa bima ya afya ya TotoAfyaKadi kwa kushindwa kugharamia ruzuku ya billioni 30.
Mpaka kufikia disemba mwaka 2024, zaidi ya asilimia 30% watoto wenye umri chini ya miaka mitano Tanzania walikuwa wamedumaa kwa kukosa lishe; yani kila watoto watatu unaokutana nao, mmoja kati yao ameduma.
Niwakumbushe tu pia kuwa ni watanzania wachache sana wenye uhakika wa kula mlo kamili kutokana na umaskini. Waziri wa fedha, Mwigulu Nchemba, alituambia mwaka juzi kuwa zaidi ya asilimia 30% ya watanzania hawana uwezo wa kujigharamia mahitaji ya shilingi elfu 49 tu kwa mwezi.
Hata ukisema tuishi kwa chakula cha shilingi elfu moja tu kwa familia nzima, kuna watanzania zaidi ya milioni 15 hawana uwezo huo.
Ukisema asilimia zilizobaki zina maisha mazuri utakuwa unajidanganya sana.
Ukitumia kipimo cha kipato cha shilingi elfu tano tu kwa siku utagundua karibu asilimia 50% ya watanzania hawana hiki kipato.
Ukikipandisha hiki kipato mpaka kufikia shilingi elfu 10 kwa siku, unawaacha nje zaidi ya asilimia 75% ya watanzania.
Hizi sio takwimu zangu, ni takwimu za Benki ya Dunia.
Ni kweli kwamba takwimu zinaweza kutengenezwa kutoa picha ya uongo, hata hivyo kwenye sayansi tumefundishwa namna ya kubainisha ukweli wake kupitia triangulation.
Namna nzuri ya kuthibitisha ni kuangalia takwimu za ajira nchini.
Kwa mujibu wa report ya ajira kwenye sekta rasmi Tanzania (Formal Sector Employment Report) ya mwaka 2024, ni watanzania milioni 3.7 tu ndio wenye ajira rasmi, kati ya watanzania milioni 65+ tulionao.
Ajira mpya zinazotolewa kwa mwaka ni 130,000 tu, na karibu asilimia 50% kati ya hizi ni ajira ni za kuziba nafasi.
Ukichanganya ajira zote rasmi na zisizo rasmi, tunatengeneza nafasi laki nne tu za ajira kila mwaka na hii ni kwa mujibu wa taarifa rasmi za Waziri Mkuu.
Wakati huo tuna vijana zaidi ya 1,000,000 wanaoingia kwenye soko la ajira Tanzania kila mwaka. Tumeamua kumwachia Mungu atende muujiza? 🤔
Kabla haujamalizia hiyo sentensi inayosema “mama amejitahidi ku……….”
Kumbuka deni la taifa limepanda kutoka trillioni 60ish mpaka zaidi ya trillioni 100 miaka hii minne tu.
Kumbuka CAG amesema tunatumia billioni 360+ kwa matumizi yasiyo ya lazima.
Je, hali hii itaendelea mpaka lini??🤔🤔
TUJIANGALIE.