
14/02/2025
Kwa mtazamo wa Kisayansi na Kiafya, gari lolote lililoegeshwa, iwe limezimwa au bado limewaka lakini halina mfumo wa Ubaridi (AC) unaofanya kazi ipasavyo, linaweza kuwa hatari kwa mtoto aliyeko ndani. Joto la gari iliyofungwa linaweza kupanda kwa zaidi ya nyuzi 10–15°C ndani ya dakika 10 za kwanza, na linaweza kufikia kiwango cha hatari cha zaidi ya 50°C ikiwa litaachwa kwa muda mrefu
Katika hali k**a hizi, Mtoto mwenye Umri chini ya Miaka 6 anaweza kupata Kiharusi cha Joto kali (Heat Stroke), hali inayoweza kusababisha Homa kali, Kuweweseka, Kuchanganyikiwa, Kuzimia, Kushindwa kufanya kazi kwa viungo Muhimu vya Mwili k**a Figo na hatimaye Kifo ikiwa haitadhibitiwa haraka.
Kwa kuzingatia haya, ni muhimu kuhakikisha kuwa mtoto haachwi ndani ya gari, iwe limezimwa au linawaka bila mfumo mzuri wa kuhifadhi Ubaridi na Kuruhusu kuingia na Kutoka kwa Hewa.
Kwa Tanzania, baadhi ya Mifano ya Vifo vya aina hii ni vile vilivyohusisha Watoto 2 Dar es Salaam (2007), Watoto 4 Zanzibar (2017) na Watoto wengine 2 Mkoani Shinyanga (2023)