Jamiidiary

Jamiidiary No.1 Creative Updates in πŸ‡ΉπŸ‡Ώ | Fun | Music | Art

SERIKALI YABADILI MFUMO WA ELIMU β€” MIAKA 10 SASA NI LAZIMA! πŸ‡ΉπŸ‡ΏπŸ”₯Serikali ya Tanzania imetangaza rasmi kuwa elimu ya msing...
16/04/2026

SERIKALI YABADILI MFUMO WA ELIMU β€” MIAKA 10 SASA NI LAZIMA! πŸ‡ΉπŸ‡ΏπŸ”₯

Serikali ya Tanzania imetangaza rasmi kuwa elimu ya msingi sasa itakuwa ya lazima kwa kipindi cha miaka 10 πŸŽ“

πŸ“ Tangazo hilo limetolewa na Waziri Mkuu Mwigulu Nchemba, akieleza kuwa ni sehemu ya mageuzi makubwa chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan

Haya siyo mabadiliko ya kawaida:
- Ni mageuzi makubwa zaidi tangu mwaka 1967 πŸ“†
- Elimu ya lazima imeongezwa kutoka miaka 7 hadi 10
- Lengo: Kila mtoto apate elimu bora na ya uhakika

πŸ”₯ Nini kinabadilika hasa?
- Mitaala inaboreshwa πŸ“–
- Miundombinu ya shule inaongezwa 🏫
πŸ‘‰ Mfumo wa β€œsecond selection” umeondolewa ❌
- Ujenzi wa madarasa 79,000 umekamilika

πŸ› οΈ Elimu ya ufundi yapewa kipaumbele:
- Shule zimeongezeka kutoka takribani 5 hadi zaidi ya 300 😳
- Zingine zikilenga masomo ya kihandisi βš™οΈ

MWANASIASA MKUBWA AFRICA AHUKUMIWA MIAKA 5 JELA! 😳Mwanasiasa wa upinzani nchini South Africa, Julius Malema, amehukumiwa...
16/04/2026

MWANASIASA MKUBWA AFRICA AHUKUMIWA MIAKA 5 JELA! 😳

Mwanasiasa wa upinzani nchini South Africa, Julius Malema, amehukumiwa kifungo cha miaka mitano jela kwa kosa la kumiliki bunduki kinyume cha sheria na kufyatua risasi hadharani πŸ”«

⚠️ Chanzo cha kesi:
πŸ‘‰ Tukio lilitokea mwaka 2018
πŸ‘‰ Malema alionekana kwenye video akifyatua risasi hewani πŸŽ₯
πŸ‘‰ Ilikuwa ni sherehe ya miaka 5 ya chama cha Economic Freedom Fighters

Utetezi wake:
πŸ‘‰ Alidai alikuwa anachangamsha wafuasi tu
πŸ‘‰ Hakukuwa na nia ya kudhuru mtu

Lakini mahak**a ikaamua:
Kitendo hicho ni kinyume cha sheria
Kinaweka maisha ya watu hatarini ⚠️
Adhabu: miaka 5 jela ⛓️

Hongera
16/04/2026

Hongera

MAISHA BAADA YA CHEO YAFICHUKA HADHARANI!Aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii Hamis Kigwangalla amezua mjadala baada ...
16/04/2026

MAISHA BAADA YA CHEO YAFICHUKA HADHARANI!

Aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii Hamis Kigwangalla amezua mjadala baada ya kueleza wazi changamoto anazopitia baada ya kupoteza cheo 😬

⚠️ Alichosema:
β€œNilipokuwa waziri kila kitu kilikuwa rahisi…”
β€œSasa sina cheo, hata kuwafikia watu ni ngumu”
β€œWengine wanadhani nawatafuta kwa sababu ya pesa”
β€œHata benki hazisikilizi k**a zamani”

πŸ”₯ Mjadala umechukua sura mpya baada ya kauli ya mfanyabiashara Chris Lukosi

Anadai walikuwa marafiki kabla ya cheo 🀝
Alipohitaji msaada wa matibabu, alipigwa block 😳
Baada ya Kigwangalla kupoteza cheo, akaanza kumtafuta tena πŸ“ž
β€œCHEO NI DHAMANA… what goes around comes around”

🀯 Ukweli mchungu:
Watu wengi hukuheshimu kwa sababu ya nafasi, si wewe
Mahusiano mengi hubadilika pale mamlaka yanapoisha
β€œPower” inaweza kubadilisha watu… na pia marafiki

Jeshi la Polisi Tanzania kupitia taarifa rasmi limethibitisha kuk**atwa kwa watu sita wanaotuhumiwa kuhusika na mauaji y...
16/04/2026

Jeshi la Polisi Tanzania kupitia taarifa rasmi limethibitisha kuk**atwa kwa watu sita wanaotuhumiwa kuhusika na mauaji ya askari polisi Roland Mollel katika jiji la Arusha

πŸ“ Tukio limetokea Aprili 15, 2026 katika mtaa wa Mlimani, kata ya Muriet.

Kwa mujibu wa taarifa rasmi:
πŸ‘‰ Marehemu alikuwa akitoka kwenye shughuli zake binafsi baada ya kazi
πŸ‘‰ Taharuki ilizuka baada ya kusambaa taarifa za β€œwezi” eneo hilo
πŸ‘‰ Kundi la wananchi likaanza kushambulia watu waliokuwa wanapita 😳
πŸ‘‰ Askari huyo alikuwa ameongozana na bodaboda wakati wa tukio

πŸ”₯ Kilichofuata:
πŸ‘‰ Walivamiwa na kukimbizwa na kundi la watu
πŸ‘‰ Askari huyo akauawa katika tukio hilo la kusikitisha πŸ’”

Hatua zinazochukuliwa:
πŸ‘‰ Watu 6 tayari wapo mikononi mwa polisi
πŸ‘‰ Msako unaendelea kuwatafuta watuhumiwa wengine
πŸ‘‰ Uchunguzi unaendelea kukamilishwa

πŸ“’ ONYO KUTOKA POLISI:
Wananchi waepuke kuchukua sheria mkononi ❌
Tabia ya β€œmob justice” ni kosa la jinai βš–οΈ
Inaweza kusababisha madhara kwa watu wasio na hatia

Ripoti mpya ya mwaka 2025 kutoka Freedom House imeziorodhesha kwa mara ya kwanza Tanzania na Kenya miongoni mwa nchi zin...
16/04/2026

Ripoti mpya ya mwaka 2025 kutoka Freedom House imeziorodhesha kwa mara ya kwanza Tanzania na Kenya miongoni mwa nchi zinazotuhumiwa kufanya ukandamizaji wa kuvuka mipaka 😳

Ripoti inadai nini?
πŸ‘‰ Serikali zinaweza kuwafuatilia wakosoaji nje ya nchi 🌍
πŸ‘‰ Kuwak**ata au kuwarejesha kwa nguvu ✈️
πŸ‘‰ Kulenga watu waliokimbilia ughaibuni kwa usalama

Nchi zaidi ya 54 duniani zinahusishwa na vitendo hivyo tangu 2014
Hii ni zaidi ya robo ya mataifa yote duniani 🌐

πŸ“Š Nani wanaongoza?
πŸ‘‰ China ndiyo kinara duniani
πŸ‘‰ Ikifuatiwa na Vietnam πŸ‡»πŸ‡³
πŸ‘‰ Kisha Russia πŸ‡·πŸ‡Ί

😳 Afrika Mashariki nayo ipo:
πŸ‘‰ Tanzania na Kenya zimeingia kwa mara ya kwanza kwenye orodha
πŸ‘‰ Zimeungana na nchi k**a Afghanistan na Zimbabwe

Je, unadhani madai haya yana ukweli au ni wivu tu kutoka nje?

Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limepitisha rasmi bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka wa fedha 2026/2027 y...
16/04/2026

Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limepitisha rasmi bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka wa fedha 2026/2027 yenye thamani ya Tsh trilioni 12.5 πŸ’Έ

πŸ“ Bajeti hiyo iliwasilishwa Dodoma na Waziri Mkuu Mwigulu Nchemba na kupitishwa baada ya mjadala mzito bungeni.

⚠️ Fedha zitakavyogawanywa:
πŸ‘‰ Trilioni 8.7 – Matumizi ya kawaida 🏒
πŸ‘‰ Trilioni 3.7 – Miradi ya maendeleo 🚧

πŸ”₯ Serikali inalenga nini?
πŸ‘‰ Uboreshaji wa barabara πŸ›£οΈ
πŸ‘‰ Kuimarisha huduma za afya πŸ₯
πŸ‘‰ Huduma za jamii kuboreshwa 🀝
πŸ‘‰ Utawala bora kuimarika βš–οΈ
πŸ‘‰ Upatikanaji wa mafuta β›½
πŸ‘‰ Ajira kwa vijana kuongezeka πŸ‘¨β€πŸ’ΌπŸ‘©β€πŸ’Ό

So:
πŸ‘‰ Bajeti imepitishwa rasmi βœ…
πŸ‘‰ Sasa macho yote yapo kwenye utekelezaji πŸ‘€
πŸ‘‰ Wananchi wanasubiri kuona matokeo halisi

Je, unadhani bajeti hii italeta mabadiliko ya kweli au ni ahadi tu k**a kawaida yao?

Papa kajibu huku
16/04/2026

Papa kajibu huku

Familia ya Ashly Robinson ipo kwenye majonzi makubwa kufuatia kifo chake cha ghafla kilichotokea Zanzibar πŸ•ŠοΈπŸ“ Inaripotiw...
16/04/2026

Familia ya Ashly Robinson ipo kwenye majonzi makubwa kufuatia kifo chake cha ghafla kilichotokea Zanzibar πŸ•ŠοΈ

πŸ“ Inaripotiwa kuwa alikutwa hana fahamu katika villa ya ZURI, Nungwi, kabla ya kukimbizwa hospitalini na kutangazwa kufariki dunia Aprili 10.

Kinachoongeza maumivu: πŸ‘‰ Familia inahangaika kurejesha mwili Marekani πŸ‡ΊπŸ‡Έ
πŸ‘‰ Wameanzisha kampeni ya GoFundMe ya $50,000
πŸ‘‰ Tayari wamekusanya karibu $39,976 (~Tsh Milioni 101) πŸ’°

πŸ”₯ Maswali mazito yanaibuka:
πŸ‘‰ Nini kilisababisha kifo chake ghafla?
πŸ‘‰ Je, ni ajali, matatizo ya afya au kuna zaidi nyuma ya tukio hili?

πŸ•΅οΈ Uchunguzi unaendelea:
πŸ‘‰ Polisi wanachunguza uwezekano mbalimbali ikiwemo kujidhuru
πŸ‘‰ Inaripotiwa kulikuwa na mgogoro kati yake na mchumba wake Joe McCann kabla ya tukio
πŸ‘‰ Wahudumu wa hoteli waliwahi kuwatenganisha kabla ya tukio hilo

🌍 Tukio limeibua mjadala kuhusu usalama wa watalii
πŸ‘‰ Linaacha familia bila majibu ya moja kwa moja
πŸ‘‰ Linaonyesha gharama halisi za majanga ya ghafla kwa familia

Familia bado inasubiri majibu ya uchunguzi
πŸ‘‰ Michango inaendelea kukusanywa
πŸ‘‰ Ukweli kamili bado haujajulikana

Ni maneno ya jux sio yetu
16/04/2026

Ni maneno ya jux sio yetu

16/04/2026

Address

Dar Es Salaam

Opening Hours

Monday 09:00 - 19:00
Tuesday 09:00 - 19:00
Wednesday 09:00 - 19:00
Thursday 09:00 - 20:00
Friday 09:00 - 20:00
Saturday 09:00 - 20:00
Sunday 09:00 - 20:00

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Jamiidiary posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share