Ostvtz

Ostvtz Ukurasa sahihi na Pekee kwa ajili ya Habari, Nichezo, Burudani na Makala.

Ingia Youtube Chanel yetu kupitia link hii
https://www.youtube.com/channel/UCQYhqW7mhf0rzvrASltoXVA

Timu Ya taifa ya tanzania  imefuzu katika fainali za afcon za mwaka 2024 zinazotarajiwa kufanyika nchini ivory costMafan...
07/09/2023

Timu Ya taifa ya tanzania imefuzu katika fainali za afcon za mwaka 2024 zinazotarajiwa kufanyika nchini ivory cost

Mafanikio hayo yamekuja baada ya taifa stars kutoka suluhu ya bila kufungana katika mchezo wao dhidi ya algeria ulichezwa nchini nigeria

Hii ni mara ya tatu katika historia ya Tanzania kufanikiwa kutinga kwenye fainali hizo kubwa zaidi za soka barani Afrika.

Jengo la Kitega Uchumi (Safina House) la Kanisa la AnglikanaTanzania, Dayosisi ya Central Tanganyika Dodoma ambalo limef...
15/08/2023

Jengo la Kitega Uchumi (Safina House) la Kanisa la Anglikana
Tanzania, Dayosisi ya Central Tanganyika Dodoma ambalo limefungulia Rasmi leo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Hafla ya ufunguzi imefanyika katika viwania vya Kanisa Kuu la Roho Mtakatifu Dodoma leo Jumanne tarehe 15 August 2023
Os Tv kwa Ajili Yako

Makamu wa Kwanza wa Rais TFF, Athuman Nyamlani (kulia) akikabidhi mchoro wa benchi la timu kwa Waziri wa Utamaduni, Sana...
27/07/2023

Makamu wa Kwanza wa Rais TFF, Athuman Nyamlani (kulia) akikabidhi mchoro wa benchi la timu kwa Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Balozi Pindi Chana (katikati) benchi hilo la kisasa kwa timu mwenyeji, timu ngeni na maofisa wa mchezo litagharamiwa na TFF katika sehemu ya maboresho ya uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Kufuatia kutungwa kwa Sheria ya Mipango ya Taifa ya Mwaka 2023 pamoja na uamuzi wa kuhamishia masuala a uwekezaji Ofisi ...
05/07/2023

Kufuatia kutungwa kwa Sheria ya Mipango ya Taifa ya Mwaka 2023 pamoja na uamuzi wa kuhamishia masuala a uwekezaji Ofisi ya Rais, hivyo Rais Samia Suluhu Hassan amefanya mabadiliko madogo ya Miundo ya Wizara na kufanya uteuzi wa viongozi k**a ifuatavyo kwenye taarifa kutoka kwa mkurugenzi wa mawasiliano ya rais.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi mbalimbali, Maspika, Naibu Masp...
03/07/2023

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi mbalimbali, Maspika, Naibu Maspika pamoja na Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa 53 wa Jukwaa la Mabunge ya Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC-PF) uliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Gran Melia Jijini Arusha 03 Julai, 2023.
 

Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Awamu ya Nne, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Mfuko wa Ushirika wa Wafadhili...
28/06/2023

Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Awamu ya Nne, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Mfuko wa Ushirika wa Wafadhili wa Elimu Duniani (GPE) Mhe.Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuanzisha mchakato wa mabadiliko ya Sera ya Elimu na Mitaal ili kukidhi mahitaji ya soko Kitaifa na Kimataifa.

Mhe. Kikwete ametoa pongezi hizo Juni 27, 2023 jijini Dodoma katika kikao na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kumpitisha kwenye kwenye Rasimu ya Sera ya Elimu na Mafunzo mwaka 2014 Toleo la 2023 na Mabadiliko ya mitaala.

Bunge la Tanzania limeidhinisha kwa kishindo Bajeti Kuu ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/24 yenye jumla ya Shilongi T...
26/06/2023

Bunge la Tanzania limeidhinisha kwa kishindo Bajeti Kuu ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/24 yenye jumla ya Shilongi Trillioni 44.39 ambapo mapato ya ndani yanatarajiwa.

kuwa Shilingi Tr 31.38 Sawa na Asilimia 70.7 % ya Bajeti yote

Mapato yatakayokusanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania -TRA yanakadiriwa kuwa Shilingi Trillion 26.73 na Mapato yasiyo ya Kodi (Wizara,Idara,Taasisi na Mamlaka za Serikali za Mitaa) yanakadiriwa kuwa Shilingi Tr 4.66.

Basi la kampuni ya Newforce lenye namba za usajili T.173 DZU,  limepata ajali eneo la Igando Mkoani Njombe na kusababish...
21/06/2023

Basi la kampuni ya Newforce lenye namba za usajili T.173 DZU, limepata ajali eneo la Igando Mkoani Njombe na kusababisha vifo vya Watu watano.
Kwa mujibu wa taarifa za awali zilizotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe Kamishna Msaidizi wa Polisi John Imori zimeeleza kuwa watu watano wamefariki dunia huku wengine kadhaa wakijeruhiwa katika ajali hiyo.

Chanzo cha ajali kinadaiwa kuwa ni Bus kujaribu kulipita gari lingine kimakosa.

Basi hilo la New Force lenye namba za usajili T.173 DZU linalofanya safari zake kutoka jijini Dar es salaam kwenda mkoani Rukwa Lilijaribu kulipita roli na kuingia mtaroni katika kijiji cha Igando kata ya Luguda wilaya ya Wanging'ombe Mkoa wa Njombe.

Ajali hiyo imetokea majira ya saa nane na nusu mchana wa Leo.

Os Tv kwa Ajili Yako

Wanafunzi 150 wa udaktari kutoka Chuo Kikuu cha Tiba, Sayansi na Teknolojia (UMST) cha Khartoum nchini Sudan wamehamishi...
19/06/2023

Wanafunzi 150 wa udaktari kutoka Chuo Kikuu cha Tiba, Sayansi na Teknolojia (UMST) cha Khartoum nchini Sudan wamehamishiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) ili kukamilisha mwaka wao wa mwisho wa masomo, kutokana machafuko ya kisiasa nchini mwao yaliyosababisha vyuo kufungwa.

Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa, akimkabidhi mchezaji wa Taifa Stars Simon Msuva fedha za goli la mama sh.10M zi...
19/06/2023

Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa, akimkabidhi mchezaji wa Taifa Stars Simon Msuva fedha za goli la mama sh.10M zinazotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan baada ya ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Niger mchezo wa kufuzu AFCON 2023.

Spika wa Bunge Mheshimiwa Dkt. Tulia Ackson (Mb), amezindua Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Bunge leo tarehe 18 Juni, ...
18/06/2023

Spika wa Bunge Mheshimiwa Dkt. Tulia Ackson (Mb), amezindua Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Bunge leo tarehe 18 Juni, 2023 katika Ukumbi wa Msekwa, Jijini Dodoma.

Dkt. Tulia, amewapongeza wajumbe na kuwataka kufanya kazi kwa bidii ili kuleta tija katika utendaji kazi wa Bunge.

Waziri wa , Dkt. , akionesha mkoba wenye Bajeti Kuu ya Serikali 2023/24 ya Sh. Trilioni 44.39 zinatarajiwa kukusanywa na...
15/06/2023

Waziri wa , Dkt. , akionesha mkoba wenye Bajeti Kuu ya Serikali 2023/24 ya Sh. Trilioni 44.39 zinatarajiwa kukusanywa na kutumika. Jumla ya mapato ya ndani yanatarajiwa kuwa shilingi trilioni 31.38, sawa na asilimia 70.7 ya bajeti yote.

Kati ya mapato hayo, mapato yatakayokusanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania yanakadiriwa kuwa shilingi trilioni 26.73 na mapato yasiyo ya kodi (Wizara, Idara, Taasisi na Mamlaka za Serikali za Mitaa) yanakadiriwa kuwa shilingi trilioni 4.66.

Klabu ya Yanga SC imethibitisha kuachana na Kocha wake raia wa Tunisia, Nasreddine Nabi baada ya kumaliza mkataba wake n...
14/06/2023

Klabu ya Yanga SC imethibitisha kuachana na Kocha wake raia wa Tunisia, Nasreddine Nabi baada ya kumaliza mkataba wake na kuomba kutoongeza mkataba mpya wa kusalia klabuni hapo

Taarifa rasmi ni kwamba kocha huyo anaenda kujiunga na timu ya Inayoshiriki Ligi kuu nchini afrika ya kusini.

Mwonekano wa ujenzi wa Daraja la JP Magufuli (Kigongo - Busisi), jijini Mwanza linalogharimu kiasi cha shilingi bilioni ...
14/06/2023

Mwonekano wa ujenzi wa Daraja la JP Magufuli (Kigongo - Busisi), jijini Mwanza linalogharimu kiasi cha shilingi bilioni 716.

Ujenzi wa daraja hilo umefikia asilimia 75.

Nyota wa Tanzania, Feisal Salum Toto amesaini na kutambulishwa rasmi kuitumikia Azam FC mpaka mwaka 2026Baada ya mazungu...
08/06/2023

Nyota wa Tanzania, Feisal Salum Toto amesaini na kutambulishwa rasmi kuitumikia Azam FC mpaka mwaka 2026

Baada ya mazungumzo ya pande zote mbili na kwa kuzingatia matakwa ya kimkataba kati ya Klabu na Mchezaji, Uongozi wa Young Africans Sports Club umefikia uamuzi wa kumuuza mchezaji huyo kwa Klabu ya Azam FC.

Mchezaji Feisal Salum ameuzwa kwenda Azam FC kwa dau ambalo halitawekwa wazi kutokana na makubaliano ya pande zote mbili.

Kupitia Kurugenzi ya Mawasiliano Ofisi ya Rais Ikulu imeripotiwa kuwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Dkt. S...
08/06/2023

Kupitia Kurugenzi ya Mawasiliano Ofisi ya Rais Ikulu imeripotiwa kuwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Dkt. Samia Suluhu Hassan, amefanya uteuzi huu mpya k**a ifuatavyo;

Amemteua Bw, Omar Issa kuwa Mkuu (Chancellor) wa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela (NM-AIST).

Bw. Issa ni mwenyekiti wa Bodi ya TANESCO na anachukua nafasi ya Mhe. Dkt. Gharib Bilali, Makamu wa Rais Mstaafu ambaye amemaliza muda wake.

Amemteua Prof. Abel N,  Makubikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mifupa (MOI). Prof. Makubi anachukua nafasi ya Dkt. respicious Boniface ambaye amemaliza muda wake.

Amemteua Dkt. Abdulhamid Yahya Mzee kuwa Mkuu wa Chuo (Chancellor) cha Taifa cha Ulinzi.

Anemteua Dkt. Edwin Mhede kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya NMB Plc kwa Kipindi cha Pili.

Uteuzi huu umeanza tarehe 06 Juni, 2023

Taarifa kwa umma kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA) ikitolea ufafanuzi taarifa zilizoenea mtandaoni kuhusu ban...
07/06/2023

Taarifa kwa umma kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA) ikitolea ufafanuzi taarifa zilizoenea mtandaoni kuhusu bandari ya Dar es Salaam kuuzwa kwa miaka 100 kwa kampuni ya DP WORLD (Dubai World) ya Dubai.
"Taarifa hizo ni za uongo na upotoshaji zenye lengo la kukwamisha mipango thabiti ya nchi katika kuongeza ufanisi wa sekta ya bandari kwa maslahi mapana ya Taifa" Imeeleza sehemu ya taarifa hiyo kutoka TPA.

Bodi ya Ligi Kuu nchini, TPLB kwa kushirikiana na wadau wengine wa Soka; Baraza la Michezo,BMT Mdhamini mkuu wa Ligi hio...
07/06/2023

Bodi ya Ligi Kuu nchini, TPLB kwa kushirikiana na wadau wengine wa Soka; Baraza la Michezo,BMT Mdhamini mkuu wa Ligi hio Benki ya NBC, Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini, TFF na Azam Media, imezindua "Kombe Jipya" lenye muonekano wa tofauti litakaloanza kutumika msimu huu wa 2022/23 kwa timu inayotwaa ubingwa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara.

Address


Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Ostvtz posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

  • Address
  • Alerts
  • Claim ownership or report listing
  • Want your business to be the top-listed Media Company?

Share