09/09/2025
Siku zimepungua, Masaa yanayoyoma dakika zinakimbia sekunde nazo si haba zinashika kasi,
Zile siku ambazo hututoa kimasomaso machizi soka,walevi wa kabumbu mateja wa kandanda zimegonga hodi, Lupaso huwa siyo uwanja tena hugeuka mbingu kwa siku hizi za Simba day na kileleni kwenye wiki ya wananchi
Udambwi na utamu wa Soka ambalo hutandazwa pale kwa Mkapa huwa ni kitu cha ziada sana ila watu huwa na uchu wa kuvijua vikosi vyao vya msimu, kuziona timu zao ambazo zilizama 'ndichi' kwa ajili ya Pre season kwa zaidi ya siku 30
K**a mnavyojua Soka na Muziki ni kopo na mfuniko
'Machizi' soka huwa tunatamani kupata burudani za A-listed artist kwenye siku zetu hizi za burudani, hii huwa ni zaidi ya Sikukuu kwetu
September 10,2025 Jumatano ni Siku ya Simba, Simba day:
Ukiachana na Show zitakazooneshwa na mtaalamu Babajar, Maema,Mpanzu na Sowah, kuna show ya mkali wa Show zote mjini, yaani mmaliza Pawa za masela na masinyirita
Wengi hatujamshuhudia Mbosso akiwa anazunguka kuimbia watu wengi hasa machizi soka kwenye stadium kubwa k**a Lupaso tena akiimbia timu yake kabisa ya damu yaani Simba SC, sasa nadhani atawaonesha, siandiki sana,
September 12,2025 Kilele cha wiki ya Wananchi,
Huku nyoka wote watatoka pangoni kwa sauti ya Zuhura, nyoka hao watakuwa na jukumu la kwenda kumjibu Zuhura Amanda ndiyo nani?
Kabla ya Ecua kuvunja nyonga za watu, basi zuhura atatunyonga kwanza juukwani tukiinama na kuinuka kisha tutaramba asali then kila mtu atapata nyumba ndogo
Hii ni zaidi ya burudani, nasema hivi kwa sababu wote tuna experience na kwenye show za aina hii, wote tulimuona kwenye Simba Day 2023 ambapo alirambiasha asali machizi soka wote pale Lupaso mwaka ule
SIJUI WEWE UNAISUBIRI SIKU GANI HAPA