01/05/2021
*HISTORIA YA WAMANDA *
Wamanda ni kabila la watu wa Tanzania wanaoishi katika Mkoa wa Njombe, Wilaya ya Ludewa.
Vijiji maarufu manda ni Igalu, Ilela, Iuilo, mbongo, masasi, ngelenge,Nsungu,kipingo,lihanguli.
Wenyeji wa Manda ni kabila la Wamanda na lugha yao ya asili ni Kimanda. Lugha hiyo hufanana sana na lugha ya Kingoni na ina maneno mengi ya Kiingereza mfano monire inayoendana na morning pia mbatata ni neno la kimanda likimaanisha viazi vitamu pia hata kibaiyolojia lina maana hiyo hiyo.
Wamanda wanapatikana katika wilaya za Ludewa, Mbinga na Nyasa kuanzia Lituhi, Ndongosi na kata za jirani upande wa wilaya ya Nyasa.
Pia wako katika Mkoa wa Ruvuma, Wilaya ya Mbinga. Katika wilaya ya Ludewa Wamanda wanapatikana katika kata za Manda, Ruhuhu, Luilo, Iwela, Mkomang'ombe, Ludewa na Masasi. Katika mkoa wa Ruvuma wanapatikana zaidi kaskazini mwa wilaya ya Mbinga.
Nimeandika hii sababu ya baadhi ya watu katika historia ya mwanzo kusema baadhi ya watu sio wangoni wakiwemo wamanda na wamatengo k**a hukusoma historia ya mwanzo "Historia na asili ya Wangoni" basi hipo hapa hapa gusa 👉 Dayocha
Wamanda kwa kiasi kikubwa wanaongea Kimanda, lugha yenye mchanganyiko wa Kingoni na Kinyasa kwa mawasiliano pia Ngoma za asili za wakazi wa Manda ni Mganda, Kihoda na Ligambusi.
Kiasili Wamanda ni Wangoni, ila, kutokana na mtengano wa kijiografia watu hao wametofautiana katika matamshi na baadhi ya misamiati. Natumaini zolanda inkomabakosi na abdul abubakar mndewa tunaelewana hapo kuhusu na . Kimanda mtu tunasema "mundu" kingoni sijuwi k**a inatofautiana na hilo neno maana ni kibantu naomba majibu sehemu ya comment wangoni wa songea maana mnatutenga wamanda.
Wamanda walio wengi ni Wakristo wa madhehebu ya kianglikana na Kikatoliki sababu ya kuwa na shule nyingi za kipindi hicho cha miaka ya nyuma. Kuna idadi ndogo sana ya Wamanda wanaoendelea kufuata dini asilia za Kiafrika. Hata hivyo, pamoja na kufuata Ukristo, Wamanda wengi bado wana mazoea ya kuendelea kuienzi mizimu na mahoka. Haya sasa najuwa kuna baadhi ya watu nimewaacha hapa kwenye mahoka ila msijali kuna watu watafafanua sehemu ya comment hapo chini nakutegemea faraja renatusi na thomas thomee na wamanda wengine.
Wakati wa ukoloni na mara baada ya uhuru Wamanda wengi walifanikiwa kusoma na kuwa na elimu nzuri wakapata nafasi nzuri serikalini. Mfano wa Wamanda waliofanikiwa kufikia nafasi za juu nchini Tanzania ni pamoja na hayati Horace Kolimba mbunge wa ludewa toka mwaka 1995 hadi 1996, Crispin Mponda, na Valieth aliyekuwa mbunge wa kwanza wa wilaya ya Ludewa kuanzi mwaka 1965 hadi 1970. Hawa ni baadhi bila kumsahau shangazi yangu mpendwa hayati magreth mlesa chale aliyekuwa diwani viti maarumu pale ludewa.
Kwa sasa kiwango cha elimu kwa Wamanda kipo chini sana kwa sababu mbalimbali, zikiwemo upungufu wa walimu katika shule za kata na hali ngumu ya uchumi inayosababisha wanafunzi wengi washindwe kumaliza japo kidato cha nne, au wakimaliza wanamaliza kwa madaraja ya chini sana, na hivyo kushindwa kuendelea.
Hili hata mimi pia nimelishuhudia maana nimesoma pale shule ya SEKONDALI MANDA kulikuwa na changamoto za walimu sababu ya mazingira shule ilipo ipo milimani na maji shida sana. Hali inayopelekea walimu wengi kutoka sehemu nyingine tofauti na kule kukimbia sababu ya usalama wa maji yanayoletwa na wanafunzi toka ziwa nyasa au mitoni kipindi cha mvua.Hila kwa sasa jitiada zinafanyika kumejengwa mabweni kule kule shule ya watoto wa k**e.
Wilaya ya Ludewa, pamoja na kujaliwa kuwa na utajiri mkubwa wa makaa ya mawe na chuma, wananchi wake bado wana hali mbaya ya kiuchumi na kwa ujumla Wamanda wanategemea misaada ya ndugu zao wanaoishi katika maeneo ya mijini kwa kiwango kikubwa.
Shughuli kuu za uchumi wa Wamanda ni pamoja na uvuvi wa samaki na ukulima wa mazao madogomadogo.kwenye uvuvi hapo kuna baadhi ya samaki maarufu sana ziwa nyasa k**a mbasa,ngumbu,mbufu,mbelele,likeru,makuku,ngorokoro,utapi,matuvi,nsenjere,masangalafu, sipa na samaki wengine ukiweza wataje hapo kwenye comment chini. Pia kwa wakazi wa dar es salaam unaweza kupata baadhi ya samaki wabichi kabisa toka ziwa nyasa na unga wa muhogo asilia kuna bro anauza ukiitaji nicheki nitaakuunganisha nae.
Chakula kikuu cha Wamanda ni ugali wa muhogo na samaki.ugali wa muhogo umegawanyika katika sehemu mbili ambazo ni bututu ambayo ni miogo ya kuanika kisha unasaga kupata unga pia kuna kondowoli ni miogo inaanikwa kwa muda kisha inarainika na kuanikwa ikiwa imeponda na kusagwa kupata unga.