15/10/2025
Wachezaji wengi sana wa timu ya taifa ya Afrika Kusini wamekuwa na mwendelezo mzuri wa kuipatia timu ya taifa Faida na siyo kwa bahati bali ni Mipango ambayo imewekwa kusimamia soka lao
Wachezaji wengi wamecheza michuano ngazi za vijana mpaka kufika national team hivyo mwendelezo huu umeifanya timu ya taifa kuwa na Structure inayoeleweka
Mfano Teboho Mokoena ,
✅Kacheza AFCON U20
✅Kacheza AFCON U23
✅Then anacheza AFCON na Senior Team
✅Kacheza World Cup U20
✅Kacheza Michuano ya Olympic U23
✅Anaenda Kucheza World Cup na Senior Team
Ukitaka kuelewa nachomaanisha , Kawaangalie wale Vijana wa U20 wa Afrika kusini ambao wamecheza michuano ya Kombe la Dunia huko Chile ..
Hao hao baadae utakuja kuwakuta wengi wapo na timu ya taifa ya U23 na baada ya miaka kadhaa utakuja kuwakuta wapo Senior team.. 100%
Kwa hali hii unakosaje kuwa na timu yenye maelewano na muunganiko unaoeleweka !
Football ukifanikiwa kwa shortcut basi ni 5% ila ukifuata njia zake 95% Utafanikiwa kwa Ukubwa .
[📸 ]