10/12/2025
SHABIKI ALIPOTAKA KUMPONZA GOVINDA
Govinda alikuwa moja ya mastaa wakubwa zaidi Bollywood miaka ya 1990 na 2000, umaarufu wake ukiwaficha hata mastaa wakubwa wa tasnia hiyo, akiwemo Amitabh Bachchan!
Mashabiki vijana walikuwa tayari kufanya chochote ili tu wamuone au kupata sahihi yake, wakifurika kwenye sets za filamu na matukio aliyohudhuria.
Mmoja kati ya hao alikuwa Santosh Rai, shabiki mkubwa wa Govinda ambaye mwaka 2008 alitembelea seti ya filamu ya "Money Hai Toh Honey Hai" huko jijini Mumbai, akitumaini kumuona staa wake kipenzi. Wakati wa picha kurekodiwa, alikaa kimya nyuma ya waigizaji na watu wa nyuma ya kamera akitazama kwa hamu kila kinachoendelea, bila kujua kuwa tukio hilo la ndoto yake lingegeuka kuwa la kushtua.
Kile kilichoanza k**a ziara ya kawaida kati ya shabiki na msanii wake, kiligeuka ghafla kuwa tukio la kushtusha baada ya Govinda kupoteza uvumilivu na kumpiga Santosh kofi mbele ya kila mtu. Kofi hilo lilikuwa fedheha kubwa kwa Santosh, ambaye alikuwa akimuabudu nyota huyu wa "Dostana".
Wakati Govinda akisema kwamba shabiki huyo “alileta kero kwa wacheza muziki wa kike” wakati wa ku-shoot, Santosh alisimulia upande tofauti kabisa wa tukio.
Akizungumza na Rediff, Santosh alisema: “Fikiria kupigwa na mtu uliyemchukulia k**a mungu.”
Kilichofuata kilikuwa kesi ya kisheria iliyodumu kwa miaka 9, ikirudi kwenye vichwa vya habari kila ilipofufuliwa. Santosh Rai aliwasilisha kesi ya kushambuliwa, akidai haki na fidia kwa aibu aliyopata.
Hatimaye kesi ilifika Mahak**a kuu, ambako majaji hawakusita kumkemea Govinda. Kwa mujibu wa Rediff, mahak**a ilimwambia Govinda, “Tuna-enjoy filamu zako, lakini hatuwezi kuvumilia wewe kumpiga mtu.”
Kadri kesi ilivyoendelea, timu ya wanasheria wa Govinda ilijaribu kuimaliza kwa njia ya maelewano, wakitoa msamaha na fidia ya rupia laki tano. Mahak**a ilibainisha kwamba angeweza kushtakiwa ikiwa Santosh angekataa msamaha huo, na angekabiliwa na kifungo cha hadi miaka miwili kwa vitisho na shambulio.
Mwaka 2017, Govinda aliomba msamaha hadharani kwa Santosh Rai, akitoa tamko la toba bila masharti na kutaka kutoa fidia ya fedha. Lakini Santosh alikataa fedha hizo, akiiambia Hindustan Times: “Nilitaka hak