02/03/2025
Barcelona wanatazamia kumuongezea mkataba Raphinha ukiwa na kipengele cha kumuuza baada ya Kombe la Dunia la 2026 kwa mujibu wa ripoti kutoka nchini Uhispania.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 amekuwa miongoni mwa wachezaji bora zaidi wa Barcelona wa msimu huu, akifunga mabao 24 na kusaidia (assists)18 katika mechi 38 katika mashindano yote.
Klabu za Premier League na Saudi Pro League zimetajwa kuhitaji huduma ya Raphinha. Jarida la Uhispania Mundo Deportivo limeripoti kwamba Barcelona, ambayo hivi karibuni iliwaongeza mikataba Pedri, Gavi, Pau Cubarsi, Ronald Araujo na Inigo Martinez, wanapanga kuweka masharti mapya kwa Yamal, Jules Kounde na Raphinha, huku Wachezaji hao wakiwa tayari wamepewa ofa mezani.
โ๏ธ |