28/02/2026
GIZA KABLA YA NURU
🔥 EPISODE 4: “Wale Aliowaamini Walianza Kubadilika”
Baada ya miaka kadhaa kupita, nilianza kuona mabadiliko yasiyo ya kawaida. Si mabadiliko yake tu — bali ya watu waliomzunguka. Kadri alivyokuwa anaanza kufikiria tofauti, ndivyo baadhi ya marafiki zake walivyoanza kumtazama kwa jicho lingine.
Mwanzoni ilikuwa ni utani. “Umeanza kujiona sasa?” “Mbona umebadilika sana?”
Lakini nyuma ya maneno hayo kulikuwa na kitu kizito — wivu, hofu, au labda kutokuamini.
Nilimwona akiumia, lakini bado alijaribu kubaki vilevile ili asipoteze watu. Alijishusha kidogo. Alipunguza ndoto zake hadharani. Alijifanya bado yupo pale pale.
Lakini ndani yake kulikuwa na mgogoro.
Alihisi k**a anajisaliti ili tu abakie kwenye kundi.
Siku moja aliniambia, “Inauma kuchagua kati ya kukua au kubaki na watu.” Huo ulikuwa ukweli mchungu aliokuwa anakutana nao kwa mara ya kwanza.
Na alipofanya uamuzi wa kuanza kuweka mipaka, baadhi yao waliondoka bila kuaga.
Hakulia mbele yao. Lakini nilijua kuna kitu kilikuwa kinapasuka ndani yake.
👉 Hakujua kwamba kuondoka kwao kulikuwa mwanzo wa kipindi cha upweke ambacho kingemfundisha ukweli ambao hakuna rafiki angeweza kumfundisha…
Je, ni nini kitaendelea.. endelea kufuatilia
Grow with DFM