R FIRST

R FIRST Welcome to the digital revolution of
News | Updates | Sports | Entertainment

05/03/2025
PART 1:Wengi hasa wafuatiliaji wa soka katika miaka ya 1990s mpaka 2000s wanamfahamu mtu anaitwa Ronaldo Luís Nazário de...
28/10/2024

PART 1:Wengi hasa wafuatiliaji wa soka katika miaka ya 1990s mpaka 2000s wanamfahamu mtu anaitwa Ronaldo Luís Nazário de Lima, alikuwa maarufu kwa jina la Ronaldo, mchezaji wa zamani wa vilabu vya Inter Milan, Barcelona, Real Madrid, PSV, Corinthians na timu ya taifa ya Brazili ambaye kwa sasa ni mfanyabiashara mkubwa na mmiliki wa timu ya La liga ya Real Valladolid.

Alikuwa mshambuliaji mahiri akitwaa kombe la dunia na Brazil mwaka 2002 na kutwa a tuzo ya mchezaji bora wa dunia mara 3. Wengi wanadhani jina la Ronaldo wa sasa limetokana na umaarufu wa Ronaldo wa zamani, la hasha Ronaldo wa sasa jina lake lina historia tofauti.

Cristiano Ronaldo Dos Santos Aveiro alizaliwa mwaka Februari 5, mwaka 1985 huko Funchal katika visiwa vya Madeira, kwa mama Maria Doroles Dos Santos Aveiro na marehemu baba yake Jose Dinis Aveiro.

Alipozaliwa tu baba yake akampatia jina la Ronaldo akimuona k**a Ronald Reagan (Rais wa Marekani) ajae.

Wakati huo baba yake hakuwa na wazo kabisa kuhusu mwanae kuwa mwanasoka, alimpenda sana Rais Reagan, ambaye wakati Ronaldo anazaliwa ndio alikuwa ametoka kuapishwa kuwa rais katika awamu yake ya pili ya uongozi

Google
Ronaldo ni mtoto wa mwisho katika familia ya watoto watatu waliozaliwa na wazazi wake, mwingine ni Maria Dolores mwenye fani ya upishi na Jose Denis Aveiro ambaye ni askari wa zamani, mtunza bustani na mtunza vifaa. Ana ndugu wengine wakubwa kaka yake Hugo, na dada zake wawili Elma na Liliana Cátia "Katia".

Katika utoto wake, Ronaldo alikuwa anadekezwa na kudeka kupita kiasi. Kuna wakati ndugu zake hasa kaka zake walilazimika kubeba makosa yake. Alijiliza na kujilalamisha kitoto kila alipoona amekosea, na kwa huruma zao ndugu zake wakubwa walibeba makosa yake mbele ya wazazi wao.

Baba yake José, alifariki mwaka 2005 Ronaldo akiwa na miaka 20 tu, huku mama yake akitibiwa saratani ya matiti mwaka 2007, ingawa anaendelea vyema sasa.

Kwahy debola atawakaba hawa😢
09/07/2024

Kwahy debola atawakaba hawa😢

Tumuite King au?
08/07/2024

Tumuite King au?

Pengine Ulikuwa unajiuliza nani hasa alihusika katika Uandishi wa Wimbo mpya wa The African Princess  Uliotumika Kusindi...
19/01/2024

Pengine Ulikuwa unajiuliza nani hasa alihusika katika Uandishi wa Wimbo mpya wa The African Princess Uliotumika Kusindikiza Siku ya Kuvishana Pete ya Uchumba kwa Haji Manara na Mchumba wake sasa majibu ni Mume wa Nandy Billnass ndiye Muandishi wa Kazi Hiyo.

Billnass ameweka wazi kwaKuandika Ujumb Ufuatao;

"Wimbo wangu wa pili kumuandikia Mama na wa 6 kumuandikia msanii tofauti na mimi…na aina tofauti ya mziki… Wimbo wa kwanza kumuandikia ulikuwa unaitwa Kwenye na Huu ni Wapili…unaitwa produced by Nafikiria Kuanza Kuandika Nyimbo na Kuuza kwa waimbaji wazuri…. ahsante umeutendea Haki Wimbo 📝 🙏🏿🙏🏿🙏🏿".

Nini Comment yako kwa Familia Hii..?

Wakati Watoto wa Temeke wako booth kuingiza Sauti kwenye mdundo wa ajabu mikono ya majani hawakujua k**a wanatengeneza S...
17/11/2023

Wakati Watoto wa Temeke wako booth kuingiza Sauti kwenye mdundo wa ajabu mikono ya majani hawakujua k**a wanatengeneza Smash Hit!! Sio Hit Song

Hawakujua wanatengeneza Goma litakalotamba Vizazi vingi vijavyo. Chege na Temba hawakujua goma hili watalitumia Kwenye Show zao za 2023 tena k**a Ngoma tegemeo Ni enzi za Jk wa msoga Balaa lilipikwa Bongo Records mpaka sasa Kelele zake hazipoi na mitaa haisahau

Zimelia Kwaito, zimelia Singeli Zimelia Afro Beat zimekuja kulia Amapiano ila kuna hii midundo ikisikika Wahuni lazima wanyanyuke asante Majani, Asante Master Asante Dunga msingi wa Ladha za Bongo

Wakati Wanaume Family wanaandika Historia na kuacha Urithi wa muziki kuna Mwanaume mmoja tokea Zanzibar alikua anapiga Hesabu za Kutimiza tu ndoto zake k**a Wachezaji wengine ila ya Mungu mengi alifanya kitu kilichobaki Historia kwenye mpira wa nchi

Abdi Kassim 'Babi' ama Ballack wa unguja ni jina maaarufu litakaloishi sana kwenye kumbukumbu za Lupaso, Kwanza Kwa kufunga Bao la kwanza Katika uwanja huo na pili ni ufungaji wa mabao yake katika uwanja huo

Mgosi, Okwi, Tambwe,Mayele, kagere,Boko na wengineo wamefunga sana Lupaso ila jina La Abdi linasalia kwenye kurasa ya peke yake uwezo wa kufunga mabao ya Kusisimua kutoka Maeneo magumu vinamfanya Babi kuishi katika Historia kwa vizazi vingi sana ilikua ni kuagiza Tu wapii? Dar mpaka moro

Watakuja wafungaji mahiri siku moja atasahaulika Kagere na Mayele hata rekodi ya Mmachinga itavunjiwa Lupaso ila Mkata nyuzi wa mwanzo Lupaso anasalia kua mmoja tu Abdi Kassim na jina lake litaishi hata uwanja ule ukizeeka

Wamepita Viungo wengi wanaojua kupiga makombora ila Jina la Babi limesalia kua juu ya wote, Ndemla, Feitoto nk

Asante Benja kwa Kutuachia Lupaso Asante majani kwa mdundo Adhim, Tmk wanaume Na mwanaume Wa Zenjibar tunakubali sana

K**a kunaendeka nijue k**a hakuendeki nijue Wapii? Dar mpaka Moro...

Habari Jirani … Tushauriane jambo hapa…🤔🤔🤔 Hivi hakuna uwezekano wa kuwachukua na kuwahifadhi ndugu zetu wenye changamot...
17/11/2023

Habari Jirani … Tushauriane jambo hapa…🤔🤔🤔

Hivi hakuna uwezekano wa kuwachukua na kuwahifadhi ndugu zetu wenye changamoto ya afya ya akili…ambao hulala nje ya nyumba na mitaa yetu…wakila mabaki ya chakula na takataka tulizozitupa jalalani…?😢😢😢

Hakuna uwezekano wa kuwatengenezea vituo maalum ambapo watapata tiba, chakula, malazi na mavazi?

K**a hili tutashindwa…! Hakuna uwezo wa kuwapatia angalau mlo mmoja ulio safi na salama nje ya nyumba na mitaa yetu?

Hakuna uwezekano wa kuwavika zile nguo ambazo hatuzitumii na wao wakasitirika?

Vibarikiwe vizazi 👼👼👼vya wale wote ambao hutoa sehemu ya mali zao kwa ajili ya hawa ndugu zetu.

USHAURI
• Tusiwaafanye sehemu ya burudani…tukiwatania na kuwacheka pale wanapofanya vituko ambavyo viko nje ya uwezo wa akili zao…tuwalee…tuwatunze…tuwajali na Mwenyezi Mungu atatuhifadhi sisi na vizazi vyetu.

Jirani, linda afya ya akili yako🧠🧠🧠 kwa gharama yoyote ile…samehe na sahau, kula vizuri, pumzika, lala vizuri na fanya mambo yote kwa kiasi.

Nikutakie siku njema…usisahau kunywa maji safi na salama ya Uhai

   

MMAKONDE HARMONIZE, katikati ya Uvamizi wa Amapiano na ladha za Mandela wa Kusini mwa Afrika, anapita yeye na Bongo Flev...
17/11/2023

MMAKONDE HARMONIZE, katikati ya Uvamizi wa Amapiano na ladha za Mandela wa Kusini mwa Afrika, anapita yeye na Bongo Fleva to the rescue! Kijana pekee aliyepita kwenye mikono ya Diamond ambaye ndie alisababisha Chibu wa Morogoro aache mziki kwa muda na kuendelea na mambo mengine, ulitaka afanye nini k**a una Rajab wa Tandahimba anaimba na anakufanya unavimba?

Mwanafunzi pekee aliyemuelewa vyema Mwalimu wake, aliketi vyema kwenye kilinge cha Mziki na kuchota uchawi wa Chibu, mdomoni watasema hana anachofanya ila moyoni watu wanakiri kuwa Mmakonde ni ‘Chizi Mziki’ ambaye aliwahi kumnyanyua JPM wa Chato kwenye kiti na alimfanya Samia wa Kizimkazi atabasamu kwenye Bongo Fleva na sio mahadhi ya Pwani.

Kwa Mapresenter wote, kwa Vijana wote na watu wote wa mziki ambao hawakubahatika kumwona Chibu wa miaka 13 nyuma basi huyu hapa ndio yeye ni copy yake hii, ni kila kitu hiki! Mmakonde alielewa Module zote, akapata coursework akapiga UE yake na sasa yupo kwenye ajira na Konde Gang yake, anaiokoa Bongo Fleva yake kutoka mikononi mwa Wazulu.

Mmakonde akijua kitu amejua, wapo imara sana! ni ‘Chizi Mziki’ anajua sana😀💪

Ee ndio ndio! Jicho likae kijanja, mara moja moja🎶😀

Address

Dar Es Salaam

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when R FIRST posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share