01/09/2026
Kiongozi wa zamani wa magenge ya uhalifu nchini Marekani, Duane “Keffe D” Davis amepatikana na hatia ya mauaji ya daraja la kwanza kwa kuhusika katika kupanga mauaji ya rapa maarufu Tupac Shakur, yaliyotokea mnamo 1996.
Waendesha mashtaka walisema Davis ndiye aliyetoa silaha na kupanga shambulio hilo la kuvizia lililomuua Tupac huko Las Vegas, ingawa hakutuhumiwa kuwa ndiye aliyefyatua risasi.
Mahak**a ya Nevada ilifikia uamuzi huo baada ya majaji kujadili kesi hiyo kwa takribani saa tatu, Chanzo cha Davis kufanya mauaji hayo inadaiwa ni kisasi cha kushambuliwa kwa mpwa Davis na Tupac wakati huo.
Davis mwenye umri wa miaka 63,ndiye mtu pekee aliyekuwa kwenye gari ya waliomshambulia 2pac ambye yupo hai mpaka sasa na nakabiliwa na uwezekano wa hukumu ya kifungo cha maisha jela.