ITV EXTRA

ITV EXTRA Officially ITV EXTRA page

 : Moto mwingine umezuka katika Mlima Kilimanjaro, kaskazini mwa Tanzania, wiki tatu tu baada ya moto uliodumu kwa karib...
28/09/2026

: Moto mwingine umezuka katika Mlima Kilimanjaro, kaskazini mwa Tanzania, wiki tatu tu baada ya moto uliodumu kwa karibu wiki mbili kudhibitiwa katika mlima huo, ambao ni mrefu zaidi barani Afrika.

Mamlaka ya Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) imesema moto huo ulianza alfajiri ya Jumatatu katika eneo la Sangarini, karibu na mwinuko wa Kamwanga, kuelekea Shira Plateau upande wa magharibi wa mlima huo. Timu ya pamoja ya wazima moto, maafisa wa uhifadhi, wadau wa utalii na wananchi imepelekwa eneo hilo kwa ajili ya kudhibiti moto huo.

Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi wa TANAPA, Catherine Mbena, amesema chanzo cha moto huo bado hakijafahamika na uchunguzi unaendelea. Amesema juhudi za kuuzima zinakabiliwa na changamoto ya upepo mkali na uoto unaowaka kwa urahisi, huku moto ukiendelea katika eneo lililopo takribani mita 3,800 kutoka usawa wa bahari.

Hata hivyo, TANAPA imesema shughuli za utalii, ikiwemo upandaji wa Mlima Kilimanjaro, zinaendelea k**a kawaida. Moto huo umetokea muda mfupi baada ya moto mwingine upande wa mashariki wa mlima huo kuteketeza zaidi ya hekta 1,800 za uoto wa asili kabla ya kudhibitiwa.

28/09/2026

: Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu, amefika katika Mahak**a Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam, kuendelea na uwasilishaji wa majumuisho ya mwisho katika kesi ya uhaini inayomkabili.

Hata hivyo, leo Lissu ameiomba Mahak**a kumpa nafasi ya kuwasilisha masuala muhimu baada ya kuhitimisha majumuisho yake, akisisitiza kuwa masuala hayo ni muhimu kuzingatiwa na Mahak**a katika hatua za mwisho za kesi hiyo.

Kwa taarifa zaidi ufuate (follow) ukurasa wetu mpya wa Facebook EXTRA>>>> https://www.facebook.com/share/1QMjXDHqGv/?mibextid=wwXIfr

Powered by
‎
‎JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
‎-
‎Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M - Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
‎
‎ ITVTanzania
‎Follow
‎

 : Lionel Messi ameendelea kuonyesha ubora wake katika mipira ya adhabu baada ya kufunga bao lingine la free kick, huku ...
28/09/2026

: Lionel Messi ameendelea kuonyesha ubora wake katika mipira ya adhabu baada ya kufunga bao lingine la free kick, huku sasa akiwa amefunga mabao 4 ya free kick katika mechi 7 zilizopita.

Messi sasa amefikisha mabao 76 ya free kick katika maisha yake ya soka, akiwa amebakiza mabao mawili kufikia hatua nyingine kubwa ya kihistoria ya kuipita rekodi ya Juninho Pernambucano mwenye magoli 77.

Kwa taarifa zaidi ufuate (follow) ukurasa wetu mpya wa Facebook EXTRA>>>> https://www.facebook.com/share/1QMjXDHqGv/?mibextid=wwXIfr

Powered by
‎
‎JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
‎-
‎Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M - Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
‎
‎ ITVTanzania
‎Follow
‎

27/09/2026

: Katika kuadhimisha Siku ya Utalii Duniani, Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro (NCAA) imetumia fursa ya uwepo wake katika Jiji la Bali, nchini Indonesia, kutangaza vivutio vya utalii vya Tanzania na kuwaalika wageni kutembelea nchini.

Akizungumza katika eneo la Krisna Oleh-Oleh Bali, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi, Mariam Kobelo, ameeleza kuwa wametumia maadhimisho hayo ya Septemba 27 kufikisha ujumbe kuhusu utajiri wa Ngorongoro na vivutio vingine ili kukuza uchumi na kuunganisha mataifa.

Kobelo amewaalika wananchi na watalii kutoka mataifa mbalimbali waliopo Indonesia kuja kujionea wenyewe uzuri wa Tanzania, akisisitiza kuwa nchi hiyo haijabarikiwa tu kwa vivutio vya kipekee vya asili na utamaduni, bali pia ina amani na utulivu mkubwa unaowahakikishia watalii usalama wao wakati wote wa safari.

Aidha, Kobelo amebainisha kuwa uwepo wao Bali kwa ajili ya mafunzo umewapa fursa ya kujifunza matumizi ya mifumo ya kisasa na teknolojia katika kutangaza utalii.

Uzoefu na maarifa hayo waliyoyapata nchini Indonesia yatatumika kuendelea kuboresha mbinu za kuitangaza Tanzania na vivutio vyake ndani na nje ya nchi kwa ufanisi mkubwa zaidi.

27/09/2026

:Baadhi ya wanawake wanaofika katika Hospitali ya Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya kwa ajili ya kupata huduma za uzazi, wameilalamikia hospitali hiyo kuhusu uwepo wa mlinzi wa kiume katika eneo la kujifungulia, wakidai kuwa amekuwa akiwachungulia wanapokuwa katika mazingira ya kujifungua.

Wanawake hao wamesema kitendo hicho kinawanyima faragha na kuhatarisha heshima yao wakati wa kupata huduma hiyo, hivyo wameiomba uongozi wa hospitali kuchukua hatua na kuhakikisha usalama pamoja na faragha ya wazazi hao inalindwa.

Malalamiko hayo yametolewa na Balozi wa Nyumba Kumi, Shina Namba Nane, Tawi la Mtakuja, Grace Kandege, mbele ya Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi katika eneo hilo, Bi.Mary Mbwilo, wakati wa kikao cha wanachama wa chama hicho katika Kata ya Ubaruku.

“Pale Hospitali ya Wilaya, katika wodi ya wazazi, tunaomba tusaidiwe. Kwenye leba kuna mlinzi ambaye ni mwanaume, na huwa anatuchungulia hasa tunapokuwa katika hali zetu za kujifungua. Tunaomba hatua zichukuliwe ili kulinda heshima na faragha ya wazazi.”

Kwa taarifa zaidi ufuate (follow) ukurasa wetu mpya wa Facebook EXTRA>>>> https://www.facebook.com/share/1QMjXDHqGv/?mibextid=wwXIfr

 : Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba amewataka Watanzania wanaofanya kazi nje ya nchi watunze uaminifu na wafanye kazi kw...
27/09/2026

: Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba amewataka Watanzania wanaofanya kazi nje ya nchi watunze uaminifu na wafanye kazi kwa bidii ili wasiliharibu jina zuri la Tanzania.
‎
‎Alitoa kauli hiyo wakati akizungumza na madareva wa Kitanzania zaidi ya 500 walioajiriwa na kampuni ya usafirishaji ya MOWASALAT kwenye kikao kifupi kilichofanyika kwenye ofisi za kampuni hiyo, zilizoko Lusail Depot nje kidogo ya Jiji la Doha, Qatar.
‎
‎Dkt. Mwigulu ambaye yuko nchini Qatar kwa ziara ya siku tatu kwa mwaliko wa Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Mhe. Abdulrahman bin Jassim Al Thani alisema: “Fanyeni kazi kwa bidii ili muwe mabalozi kwa wenzenu walioko nyumbani. Kuweni waaminifu, tunzeni jina la nchi yetu ili wenzenu waweze kupata fursa za ajira katika nchi mbalimbali. Mkiaminiwa inakuwa rahisi kufungua milango kwa wenzenu.”
‎
‎Waziri Mkuu alitumia fursa kuwapa picha halisi ya maendelea yaliyofikiwa nchini Tanzania katika sekta za elimu, afya, maji, miundombinu na akawasihi waendelee kumuunga mkono Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwa amedhamiria kuwahudumia Watanzania.
‎
‎Akijibu hoja za madereva hao kuhusu kutotambuliwa kwa vyeti vyao pindi wanaporudi nyumbani, Dkt. Mwigulu Nchemba alimwagiza Waziri wa Mambo ya Ndani afuatilie suala hilo kwa kushirikiana na wizara husika.
‎
‎Kuhusu usumbufu wa kudaiwa vibali vya kazi na ushuru wa vyakula wanavyotaka kuondoka navyo, ambao wanaupata kwenye uwanja wa ndege wa Dar es Salaam wanapokuwa wanarejea kutoka likizo, Waziri Mkuu aliwahakikishia kwamba litafanyiwa kazi mara moja.

27/09/2026

:Mbunge wa Jimbo la Tunduru Kaskazini Ado Shaibu amekutana na wakulima na wafugaji katika Kata ya Chawisi ili kusikiliza kero zao na kutatua mgogoro wa mifugo kuharibu mashamba.

Wakulima walilalamikia kuwa mifugo inalishwa kwenye mashamba yao na vijana wa wafugaji wengine wanapiga watu na kusababisha fujo ambapo kwa upande wao, wafugaji walijitetea na kusema wanataka kuishi kwa amani na kuheshimu sheria.

Katika hotuba yake, Ado alisisitiza kuwa sheria ya nchi inahitaji utaratibu maalum pale kunapokuwa na kilimo na mifugo mingi pamoja.

“Bila utaratibu, leo mtagombana, kesho mtagombana,” alisema.

Aliahidi kukaa na viongozi wa wilaya, polisi na wadau wengine ili kutafuta suluhisho la kudumu kwa pande zote mbili.

“Sauti yenu nimesikia kwa uzito. Sitawasaliiti,” alimalizia.

 :Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba ameipongeza Serikali ya Qatar kwa kufanikiwa kuwa na matumizi makubwa ya teknolojia k...
27/09/2026

:Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba ameipongeza Serikali ya Qatar kwa kufanikiwa kuwa na matumizi makubwa ya teknolojia kwenye usafiri wa umma na hasa matumizi ya nishati safi.

Ametoa pongezi hizo leo Jumamosi, Septemba 26, 2026 jijini Doha, Qatar mara baada ya kupokea taarifa ya uendeshaji wa kampuni ya usafirishaji ya MOWASALAT kutoka kwa Waziri wa Uchukuzi wa Qatar, Sheikh Mohammed bin Abdullah bin Mohammed Al Thani.

Waziri Mkuu ambaye ameanza ziara ya kikazi ya siku tatu nchini humo, amesema ubunifu wao umesaidia kuondoa msongamano wa magari barabarani kwa sababu usafiri wa umma ni wa uhakika.

"Nyumbani tunalo tatizo la msongamano wa magari na kupitia teknolojia mnazotumia, Tanzania inaweza kujifunza mbinu mlizotumia ili nasi tuweze kukabiliana nalo," amesema.

Waziri amesema amefurahi kuona kampuni yao inatumia nishati safi kwa sehemu kubwa. "Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ni kinara wa nishati safi barani Afrika, na hii ni hatua nzuri kwetu. Tunatarajia kuwa wenyeji wa AFCON 2027, kwa hiyo itatufaa sana," amesema.

Waziri Mkuu ameishukuru kampuni hiyo kwa kuwaajiri Watanzania 722 katika nafasi mbalimbali. "Ni fursa kwa vijana wetu kukuza ujuzi na kujifunza teknolojia mbalimbali."

Mapema, Waziri wa Uchukuzi wa Qatar, Sheikh Mohammed bin Abdullah bin Mohammed Al Thani alimweleza Dkt. Mwigulu kwamba kampuni hiyo inatoa huduma za usafiri wa abiria kwa kutumia mabasi, taxi, usafiri kwa wanafunzi, matukio binafsi, ya kitaifa na ya kimataifa.

"Kwa mwaka 2025, kampuni yetu imetoa huduma kwa watu milioni 42. Tunayo magari 1,200 na njia za magari (routes) tulizonazo ni 128. Asilimia 70 ya magari yetu yanatumia umeme na kutokana na ubora na uhakika wa huduma zetu, tumeweza kuyatoa barabarani magari 12,363," alisema.

Alisema kutokana na teknolojia walizonazo, magari yao yanakuwa yanakaguliwa kwa mfumo wa kielektroniki. Yamewekewa mfumo unaowezesha kubaini changamoto kwa haraka badala ya kusubiri kufanyiwa ukaguzi na mafundi," alisema.

 : Viongozi na watu mbalimbali wamejitokeza katika Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam kwa ajili ya Hitma ya ...
26/09/2026

: Viongozi na watu mbalimbali wamejitokeza katika Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam kwa ajili ya Hitma ya aliyekuwa Mume wa Rais Samia Suluhu Hassan, marehemu Maalim Hafidh Ameir Hassan.

Tukio hilo linaenda sambamba na dua ambayo katika imani ya dini ya kiislamu ni msingi wa ibada ambayo Mwenyezi Mungu (Allah) anawakumbusha wanadamu kujiombea msamaha wao kwa wao na kuwaombea msamaha ndugu zao walio tangulia mbele za haki pamoja na kutoa shukrani.
Kwa taarifa zaidi ufuate (follow) ukurasa wetu mpya wa Facebook EXTRA>>>> https://www.facebook.com/share/1QMjXDHqGv/?mibextid=wwXIfr

Powered by
‎
‎JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
‎-
‎Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M - Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
‎
‎ ITVTanzania
‎Follow
‎

 : Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi, ametangaza kuwa nchi yake imeiwasilishia Marekani pendekezo la makuba...
26/09/2026

: Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi, ametangaza kuwa nchi yake imeiwasilishia Marekani pendekezo la makubaliano linaloweza kuwezesha kufunguliwa tena kwa Njia ya Bahari ya Hormuz ndani ya siku saba.

Akizungumza na wanahabari katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa (UN) jijini New York, Araghchi ameeleza kuwa hatua hiyo inawezekana ikiwa masharti yaliyopo kwenye Hati ya Maelewano (MOU) iliyosainiwa mwezi Juni yatatekelezwa, huku akibainisha kuwa mpango huo umewasilishwa Washington kupitia wasuluhishi wa Qatar.

Hata hivyo, afisa mmoja wa Marekani aliyezungumza na BBC amesema kuwa nchi yake ipo kwenye nafasi imara kwani ndiyo inayodhibiti Njia hiyo ya Hormuz kwa sasa, hivyo "hawana haraka" ya kufikia maamuzi.

Mgogoro huo ulipamba moto baada ya Marekani na Israel kufanya mashambulizi ya anga nchini Iran mnamo Februari 28, ambapo Iran ilijibu kwa kushambulia vituo vya kijeshi vya Marekani na Israel katika Eneo la Ghuba, pamoja na kuweka vizuizi katika Njia ya Hormuz.

Njia hiyo ya Bahari ya Hormuz ni kiungo muhimu sana kiuchumi kwani karibu asilimia 20 ya mafuta na gesi kimiminika duniani hupita hapo kabla ya vita hivyo kuanza.

Kufungwa kwake kumesababisha kupanda na kushuka kwa bei za nishati duniani, huku kukiongeza shinikizo la kisiasa kwa Rais Donald Trump kutafuta suluhu ya kukomesha vita hivyo, hasa wakati Marekani ikielekea kwenye uchaguzi wa Bunge utakaofanyika mwezi Novemba.

Kwa taarifa zaidi ufuate (follow) ukurasa wetu mpya wa Facebook EXTRA>>>> https://www.facebook.com/share/1QMjXDHqGv/?mibextid=wwXIfr

Powered by
‎
‎JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
‎-
‎Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M - Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
‎
‎ ITVTanzania
‎Follow
‎

Address

P. O Box 4374
Dar Es Salaam
14112

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when ITV EXTRA posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share