29/05/2026
KILA NILIPO MSAIDIA,NDIVYO NILIZIDI KUUMIA
Mimi ni binti wa miaka 26 nilianzisha mahusiano na kijana mmoja yeye anamiaka 28, huu ni mwaka wetu wanne kwenye haya mahusiano...kiukweli nimevumilia sana yaani nimemvumilia huyu kaka jamani😭😭, iko hivi tulipoanza mahusiano baada ya mwezi mmoja tu akanipeleka nyumbani kwao na wazazi wake pamoja na ndugu zake wakanipokea vizuri tu lakini mimi hadi leo sijamleta kwetu kiufupi hafahamiki kabisa zaidi ya rafiki zangu pekee..., huyu mwanaume hana maisha yaani ndio kwanza anajitafuta lakini namuona tofauti pia sababu ni mvivu naweza kusema hivyo...yule mtu wa kusikilizia michongo mimi niliamua kuamini katika yeye atafanikiwa ndani ya miaka hii yote hali ni ile ile,..ni kweli madili yake yakitiki anapata hela lakini sijawahi kupewa hata senti kumi yake..yani hata nikimuomba ela ya pedi anasema vumilia..mtu upo mwezini alafu uvumilie unawezaje🤔🤔 mimi nipo chuo lakini familia yangu ya kawaida sana sababu baba anamwanamke mwingine kiufupi tayari wametarikiana so mzee ananisomesha tu sasa huyu boyfriend wangu yeye akiwa na shida ya hela anahitaji nimsaidie hapo nifanye navyoweza nimpatie nikikosa hatuna maelewano mazuri Tena pale anapokuomba sio aombe tu yeye anatumia nguvu k**a alikukopesha anakudai hatari kwahiyo mimi najitahidi sana kumpangaa mzee anipe pesa ili nimpatie babe nikiamini nayeye atanisaidia ila mambo yamekuwa tofauti kabisa na nilivyotegemea nikimwambia shida zangu siku hiyo atatafuta ugomvi hata kosa la nyuma atakumbushia ili mgombane ajikaushe nikishasolve changamoto zangu anarudi..ndugu zake wanasema mimi nakula hela ya kaka yao huyu mwanaume anasema hela kila akipata anasaidia ndugu zake mimi nivumilie mambo yatakaa sawa hapa ndio bado tupo mbali hali ndio hivi je nikienda kuishi nae pamoja itakuwaje??.. sasa kuna siku alikuja kuniambia kuwa mama yake anataka mjukuu sijui anamwambia umri unaenda hivyo nimzalie mimi nilikataa lakini kuna siku alitaka tukutane nikamwambia nipo siku za hatari akasema atatumia kinga nilikubali sababu nimeshazoea huwa tunatumia siku k**a hizo sasa akanifanyia makusudi hii siku...lakini namshukuru Mungu sikupata mimba nilichokifanya nikatumia k**a kipimo kwake nikamwambia nina mimba..alikubali vizuri tu ila kwenye suala la pesa ni mvutano yaani k**a kweli ningeshika mimba basi akili ingenikaa sawa sasa yeye akaenda kuwaambia ndugu zake nina mimba na wakapanga waje nyumbani ili mimi kuzuia wasiweze kuja ikabidi nimwambie jamaa mimba imeharibika...sijui ndio lilikuwa kosa langu Mama ake anatangaza ukoo wao wote mie nimetoa mimba ya mwanae sehemu zote nilizopelekwa ambazo wananijua basi wamepata taarifa yangu ya kutoa mimba hao wifi ndio usiseme..Natamani sijui nimwambie huyu mama mkwe sijawahi kupata hio mimba naogopa naona k**a sio heshima..Nawaza huyu mwanaume ananipenda kweli au Vipi??? nashindwa kuanzisha mahusiano mapya nivumilie tena kiukweli sijui nifanyeje😭😭😭... nisaidie Dada angu ushauri mimi bado nampenda huyu kaka😭😭😭
Tumpatie ushauri binti yetu🙏🙏
@