
02/10/2024
Shirikisho la Soka la Senegal limetoa taarifa rasmi ya kuachana na kocha wao Mkuu wa timu ya Taifa hilo Aliou Cisse.
Baada ya kuwa na matokeo yasiyoridhisha ndiyo imepelekea Taarifa ya uamuzi huu kutolewa na Shirikisho la Soka la Senegal.
Shirikisho la Soka la Senegal kwa sasa linawapa kipaumbele makocha wa ndani kuliko makocha wa kigeni katika kutafuta kocha mkuu mpya.
Aliou CissΓ© alikuwa kocha mkuu wa Senegal tangu 2015. Aliiongoza SENEGAL kucheza mechi mbili mfululizo za Kombe la Dunia na kuwaongoza hadi kutwaa ubingwa wa Kombe la Mataifa ya Afrika kwa mara ya kwanza mwaka wa 2021.
Katika AFCON 2023, Senegal ilitolewa katika hatua ya 16 bora.
π°πͺπΊπ¬πΉπΏ
π°πͺπΊπ¬πΉπΏ