JikoPoint

JikoPoint Chombo cha kwanza cha habari za mtandaoni kuhusu chakula na nishati safi ya kupikia.

Pata maujanja ya namna ya kutumia vifaa na nishati mbalimbali safi za kupikia kupitia kwenye mitandao ya kijamii na kwenye tovuti yetu.

05/09/2026

Jinsi ya kupika pilau la njegere na nyama kwa kutumia Westpoint pressure cooker. Mapishi haya ni rahisi na haraka kwa sababu pressure cooker hii inapika kwa muda mfupi na kwa ubora wa hali ya juu.

Westpoint Pressure Cooker, inapika chakula kwa haraka na kwa ubora bila kupoteza ladha wala virutubisho. Pressure cooker hizi zinapatikana Jiko sokoni

15/08/2026

Ndio mapishi ya kisasa ni yale yanayotumia nishati safi na salama ikiwemo umeme, umemejua, gesi ya majumbani na asilia.

Nishati hizi zinapunguza ukataji wa miti ambayo inasaidia kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi na uharibifu wa mazingira.

Pia nishati safi inahimalisha mahusiano katika familia na kulinda afya za watumiaji.

Tumekumisi je wewe ulitumisi?Sasa tumerudi tena kuwafundisha mapishi kwa njia rahisi na yenye kuleta ladha mezani bila u...
15/08/2026

Tumekumisi je wewe ulitumisi?

Sasa tumerudi tena kuwafundisha mapishi kwa njia rahisi na yenye kuleta ladha mezani bila usumbufu.

Na safari hii mambo ni motooooo kuliko mwanzo usipange kukosa

kujiunga kwenye darasa letu tuma neno MAPISHI kwenda namba 0750 881 888 ujifunze bureeeee! šŸ‘©šŸ½ā€šŸ³

10/08/2026

Nishati ya kupikia ni miongoni mwa mahitaji muhimu ya binadamu duniani kote, hiyo ndio huwezesha mapishi ya aina mbalimbali za vyakula tunavyokula ili kuimarisha afya na kuwezesha utendaji wa shughuli za kila siku.

Raymond James (25) maarufu k**a Mr Majiko, ndiye mbunifu wa majiko hayo yanayotumia mawe, umeme kidogo pamoja na chenga za mkaa mbadala zinazotokana na vifuu vya n**i.

Kijana huyo mkazi wa Gongo la Mboto jijini Dar es Salaam, ameiambia Nukta Habari kuwa kukosa ajira ndio sababu kubwa iliyommchochea kubuni majiko hayo ili aweze kujiingizia kipato kitakachomuwezesha kuendesha maisha.

Siwezi kuisahau saladi ya Juliana TettiKuna baadhi ya ladha hazifutiki kirahisi kwenye kumbukumbu. Hata upite miaka ming...
01/08/2026

Siwezi kuisahau saladi ya Juliana Tetti

Kuna baadhi ya ladha hazifutiki kirahisi kwenye kumbukumbu. Hata upite miaka mingapi, kuna chakula ukikiona tu unarudi moja kwa moja kwenye siku ya kwanza ulipokila.
Hivyo ndivyo ilivyo kwa mwanadada Maphosa Banduka licha ya miaka 18 kupita, hadi leo hawezi kusahau kabisa saladi (watercress) aliyopikiwa mwaka 2008.
"Sijawahi kula mboga tamu k**a ile hata siku moja. Alikuwa akiikata kidogo kidogo, anaitia n**i na nyama kwa ndani weee. Ladha yake ilikuwa ya kipekee," anasimulia Maphosa huku akitabasamu anapokumbuka miaka hiyo.
Alipokuwa kidato cha sita, Maphosa alikuwa akiishi pamoja na Juliana Tetti (mama mlezi) ambaye hasa ndiye mtaalamu wa pishi la saladi lililomchanganya walipokuwa pamoja katika kijiji cha Mbokomu Kibonloni, wilayani Moshi vijijini.
Saladi ni mboga gani?
Saladi ni mboga ya majani inazopatikana zaidi katika maeneo yenye maji mengi k**a vile chemchemi na kando ya mito.
Mara nyingi hupatikana zaidi katika maeneo yenye hali ya hewa ya baridi k**a vile Kilimanjaro, Arusha na Iringa.
Mbali na kuwa na harufu nzuri, saladi ni mboga laini yenye ladha tamu ambayo wengi hupenda kula na ugali.
Kulingana na tovuti ya masuala ya afya, healthline saladi ni mboga ya majani yenye virutubisho vingi inayotoka katika familia ya ā€˜Brassicaceae’.
Kikombe kimoja cha saladi kina takribani kalori 4 pekee, lakini hutoa zaidi ya asilimia 100 ya kiwango cha kila siku kinachohitajika cha vitamini K, vitamini A na vitamini C.
Pia, ina viambata muhimu vya asili vinavyojulikana k**a ā€˜antioxidants’ na ā€˜isothiocyanates’, ambavyo tafiti zinaonyesha vinaweza kusaidia kuilinda mwili dhidi ya baadhi ya magonjwa sugu, ikiwemo magonjwa ya moyo na aina mbalimbali za saratani, k**a saratani ya utumbo mpana, mapafu, tezi dume na matiti.
Juliana na pishi la saladi
Maphosa anasimulia kuwa kabla ya kuanza mapishi, Juliana aliichambua vizuri saladi na kuisafisha vizuri kwa maji safi kabla ya kuanza kuikata.
Wakati akisubiri saladi ichuje maji, Juliana aliandaa tui la n**i pamoja na viungo vingine ikiwemo kitunguu maji, nyanya, karoti, giligilani pamoja na binzari nyembamba.
Pishi hili pia huchangwanywa na nyama, hivyo wakati anaandaa viungo tayari, nyama ya ng’ombe ilikuwa inaiva jikoni. Hakika k**a ungeona maandalizi ya pishi hilo ungedhani kuwa Juliana anaandaa rosti ya biryani, lahasha ilikuwa ni saladi!
Juliana alianza kupika saladi kwa kuweka mafuta ya kupikia robo kijiko kwenye chungu cha asili kilichokuwa jikoni, kisha vitunguu ambavyo alikaanga mpaka vilipo pata rangi ya kahawia na kuegeza kwa dakika 2 kabla ya kuweka karoti na nyama.
ā€œKwa jinsi alivyokuwa fundi wa mapishi natamani angekuwa na Pressure Cooker kutoka jikosokoni.co.tz k**a ninayotumia sasa, maana pishi lingekuwa pambe hatari,ā€ anasimulia Maphosa ambaye uso wake ulikuwa na bashasha kana kwamba alikuwa anaona pishi hilo wakati huo na si miaka 18 iliyopita.
Baada ya kuweka nyama Juliana aliweka nyanya na kuzipika kwa dakika 5 hadi zikalainika kabla ya kuweka saladi juu ya mchuzi kisha akafunika kwa dakika mbili kabla ya kuweka tui la n**i na kuiacha ichemke tena kwa dakika saba.
ā€œAliniambia kwamba siku nikipika mwenyewe basi nihakikishe kuwa pishi hilo haliivi kupita kiasi kwani saladi ni mboga yenye maji mengi na laini hivyo huiva kwa haraka sana,ā€ anasema Maphosa.
Maphosa anasimulia kuwa chakula kilipoandaliwa na kuwekwa mezani, hakuna siku alikula k**a hiyo, anasema alitamani ugali usiishe kwenye sahani.
Ni miaka 18 sasa imepita tangu apikiwe pishi hilo, lakini kwa Maphosa saladi ya Juliana Tetti bado inabaki k**a kipimo cha mboga tamu zaidi kuwahi kula.
Wakati mwingine, si chakula pekee kinachobaki kwenye kumbukumbu, bali ufundi wa mapishi na jinsi unavyokiandaa chakula chako unapokuwa jikoni.
Je, na wewe una chakula ambacho kimebeba simulizi ya maisha yako?, K**a jibu ni ndio unaweza kukoment hapa.

28/07/2026

Unapotaja makabila yaliyopo nchini Tanzania si rahisi kuliacha kabila la Wasukuma ambalo ni miongoni mwa makabila maarufu kati ya zaidi ya makabila 120 yaliyopo nchini.

Licha ya kuwepo karibu katika kila mkoa, asili ya kabila hili ni maeneo ya Kanda ya Ziwa Victoria, Kaskazini mwa Tanzania.

K**a yalivyo makabila mengine kabila hili pia lina mila na desturi zake ambazo ukiacha mambo mengine kuna vyakula vya asili ambavyo hupendelea.

Mbali na ugali dagaa ambao Wasukuma hupendelea zaidi kuna chakula kinaitwa ā€˜Michembe’

Michembe ni chakula kinachotokana na viazi vitamu vilivyokatwa vipande vidogo mithiri ya ā€˜Crips’ lakini yenye upana kidogo kiasi ambacho haiwezi kuvunjika kirahisi, kisha vipande hivyo huanikwa juani na kukauka kaukau, kiasi ambacho hakuna mdudu ataweza kupenya, pindi vinapo hifadhiwa.

Ukiachana na Michembe kuwa chakula nyuma yake pamefichwa teknolojia ya uhifadhi wa chakula kwani Wasukuma hukausha viazi hivyo k**a njia ya kuhifadhi kwa ajili ya matumizi ya baadae ikiwa wamepata mavuno mengi.

Chakula hiki ni chakula cha asili cha Wasukuma lakini kinaweza kuliwa na mtu yeyote hivyo Jiko Point leo tumekuletea makala hii kukuelekeza namna ambavyo unaweza kuandaa chakula hiki na kukifurahia.

Pishi la ugali n**i lilivyomdatisha Invocavity"Yaani wakishua mn**ingua sana! Ugali wa n**i tena? Hapa ni hasara tupu."S...
28/07/2026

Pishi la ugali n**i lilivyomdatisha Invocavity

"Yaani wakishua mn**ingua sana! Ugali wa n**i tena? Hapa ni hasara tupu."Sikubishana naye.

"Usiniambie tena mambo ya ugali wa n**i." Hilo ndilo neno ambalo sikuamini ningelisikia kutoka kwa rafiki yangu Invocavity.

Ilikuwa ni Jumapili, moja ya siku ambazo napenda kutumia muda wangu mwingi jikoni kujaribu mapishi tofauti. Siku hiyo nilikuwa nimeamua kupika ugali wa n**i, chakula ambacho huenda hata wewe umeshangaa kukisikia.

Nakumbuka siku hiyo niliamka muda wa saa tano asubuhi. Baada ya kujitupia juba na kanga kubwa ya Kizanzibar nilielekea gengeni kwa mama Dokta kununua mahitaji.

Kwa kuwa nilikuwa peke yangu nilinunua unga wa Sembe nusu niliweka na akiba ikitokea hata mgeni amekuja basi nusu inatosha, kisha nilichukua n**i kubwa mbili, vitunguu maji, samaki wa sato aliyekaangwa, nyaya, karoti, kitunguu swaumu , pilipili mboga/hoho, mchicha na ngogwe/nyanya chungu huyo nikarudi nyumbani na kifurushi changu cha madikodiko.

K**a nilijua, wakati naandaa mahitaji yangu, mara ghafla rafiki yangu Invocavity akaingia jikoni akiwa ameshika tumbo kwa njaa, akanita kwa jina lake la utani k**a kawaida ya watu wa Chuga ā€œmama mzuri, unapika nini?"

"Ugali wa n**i," nikamjibu huku nikiendelea kukuna n**i. Hakumaliza hata sekunde mbili alicheka sana ilibakia kidogo nimfukuze.

"Yaani wakishua mn**ingua sana! Ugali wa n**i tena? Hapa ni hasara tupu."Sikubishana naye. Nilijua sahani ndiyo ingetoa majibu.

https://nukta.co.tz/pishi-la-ugali-n**i-lilivyomdatisha-invocavity

23/07/2026

Kwa miongo kadhaa, wanasayansi duniani wamekuwa wakiuita chakula cha baadaye kutokana na kiwango chake kikubwa cha protini, vitamini na madini muhimu kwa mwili wa binadamu.

Wakati mataifa mengi yakitumia fedha nyingi kuuzalisha kwa teknolojia ya kisasa, Tanzania imebarikiwa kuwa na mazingira ya asili yanayoweza kuukuza.

Lakini je, Watanzania wengi wanaijua spirulina? Inapatikana wapi? Na kwa nini wataalamu wanaamini inaweza kuwa sehemu ya suluhisho la changamoto za lishe na uchumi?

Umeshawahi kuona bata mwenye kilo 14? Kwa wengi hii inaweza kuwa ndoto au suala la kusadikika lakini hivyo sivyo wanavyo...
21/07/2026

Umeshawahi kuona bata mwenye kilo 14? Kwa wengi hii inaweza kuwa ndoto au suala la kusadikika lakini hivyo sivyo wanavyoamini mamia ya Watanzania waliotembelea banda la mifugo katika maonyesho ya 50 ya kimataifa ya biashara Dar es salaam (sabasaba).

Mbona bata huyu mkubwa hivi?, ni mzito hadi mkono wangu unashindwa kumshika, analiwa kweli? Nyama yake ni tamu k**a bata wengine? Anauzwa Shilingi ngapi?

Waliuliza baadhi ya Watanzania waliofika katika viwanja vya saba saba wakitaka kujua zaidi kiundani bata Bukini ama kwa kimombo African Goose.

Kwa hali ya kawaida hata wewe ungevutiwa, kwanza ana rangi nyeupe na kijivu angavu inayomfanya aonekane vyema hata akiwa mbali mwendo wa madaha, urefu na sauti ya kuvutia k**a king’ora inayomfanya yeyote anayepita karibu na banda hilo kusimama kidogo.

Katika maji yenye chumvi nyingi ambayo kwa wengi huonekana hayafai kwa maisha ya kawaida, kuna mmea mdogo unao kuwa kimy...
20/07/2026

Katika maji yenye chumvi nyingi ambayo kwa wengi huonekana hayafai kwa maisha ya kawaida, kuna mmea mdogo unao kuwa kimya kimya lakini wenye thamani kubwa kuliko wengi wanavyodhani.

Mmea huo tunaouzungumzia katika makala hii unaitwa Spirulina ambao umejizolea umaarufu kutokana na utajiri wake mkubwa wa virutubisho.

Kwa miongo kadhaa, wanasayansi duniani wamekuwa wakiuita chakula cha baadaye kutokana na kiwango chake kikubwa cha protini, vitamini na madini muhimu kwa mwili wa binadamu.

Wakati mataifa mengi yakitumia fedha nyingi kuuzalisha kwa teknolojia ya kisasa, Tanzania imebarikiwa kuwa na mazingira ya asili yanayoweza kuukuza.

Lakini je, Watanzania wengi wanaijua spirulina? Inapatikana wapi? Na kwa nini wataalamu wanaamini inaweza kuwa sehemu ya suluhisho la changamoto za lishe na uchumi?

Address

Dar Es Salaam

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when JikoPoint posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to JikoPoint:

Shortcuts

Share

l="false"> Add listing
  • Login
  • Subscribe

    We will notify you when anything happens in Dar es Salaam.