PN Mediatz

PN Mediatz PRENOVA TV is an online media platform based in Tanzania that shares news, entertainment, lifestyle updates, and trending stories.

29/09/2026

Shabiki wa Taifa Stars kutoka Dakawa, Mkoani Morogoro, amefunguka baada ya mchezo wa leo dhidi ya Madagascar uliomalizika kwa sare ya bao 1-1.

FT: MADAGASCAR 🇲🇬 1-1 TANZANIA 🇹🇿 ⚽N.Fontaine 51'                   ⚽ Cyprian Kachwele 39'Mchezo wa kufuzu AFCON 2027Cc:...
29/09/2026

FT: MADAGASCAR 🇲🇬 1-1 TANZANIA 🇹🇿
⚽N.Fontaine 51' ⚽ Cyprian Kachwele 39'

Mchezo wa kufuzu AFCON 2027
Cc:🎥

29/09/2026

Hukumu katika kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu, itasomwa Novemba 6, 2026 saa tatu asubuhi, ikiwa ni baada ya majaji kupitia ushahidi wa pande zote mbili na kufanya maamuzi.

Hayo yamesemwa leo Septemba 29, 2026 na Jaji Dunstan Ndunguru ambaye anaongoza jopo la majaji waliokuwa wanasikiliza shauri hilo la uhaini namba 19605/2025.

Jaji Dunstan Ndunguru amesema kwamba, kutokana na aina ya ushahidi uliowasilishwa na pande zote mbili, wao k**a majaji pia watahitaji muda wa kutosha ili mwisho waje na maamuzi ambayo yameandaliwa vyema.

Kabla ya majaji kutoa uamuzi huo, upande wa mashtaka ulikuwa ukiendelea na mawasilisho ya hoja za mwisho ambapo baada ya kuhitimisha waliwasihi majaji kuja na uamuzi mzuri, wakisema wao wamehakikisha wamethibitisha mashtaka.

29/09/2026

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi, amefika katika Kituo Kikuu cha Mabasi cha Magufuli jijini Dar es Salaam kuwasikiliza madereva wa mabasi ya masafa marefu wanaopinga mfumo wa kukatwa pointi kwenye leseni zao kwa makosa ya barabarani.

Katambi amesema amefika katika kituo hicho kwa maelekezo ya Waziri Mkuu, akieleza kuwa lengo ni kusikiliza hoja za madereva na kuhakikisha suala hilo linapatiwa ufumbuzi unaozingatia haki kwa pande zote.

Hatua hiyo imekuja wakati madereva wa mabasi ya masafa marefu wakiendelea na mgomo kupinga utekelezaji wa mfumo huo.

MADAGASCAR 🇲🇬 1-1TANZANIA 🇹🇿  kipindi Cha pili kinaendelea gusa LINK HAPA CHINI kuangalia live.👇https://www.youtube.com/...
29/09/2026

MADAGASCAR 🇲🇬 1-1TANZANIA 🇹🇿 kipindi Cha pili kinaendelea gusa LINK HAPA CHINI kuangalia live.👇
https://www.youtube.com/live/xTHoeNx71Pc?si=sqAIGrI3E2nS57AT

Enjoy the videos and music you love, upload original content, and share it all with friends, family, and the world on YouTube.

29/09/2026

MADAGASCAR 🇲🇬 1-1 TANZANIA 🇹🇿
56'
Cc:🎥 Azam Sports

29/09/2026

Mshanii wa Bongo Fleva, Godfrey Tumaini maarufu k**a Dudu Baya, leo Septemba 29, 2026 amemuomba radhi msanii mwenzake, Omary Nyembo “Ommy Dimpoz”, kutokana na kauli aliyotoa dhidi yake.

Akizungumza kupitia ujumbe aliouchapisha mtandaoni, Dudu Baya amesema:

“Nilitumwa jina la Ommy Dimpoz ili ujumbe ufike dunia nzima kwa sababu wewe ni maarufu, wewe ni Mdogo wangu na tunaheshimiana sana najua nilikukera, nilikuudhi, naomba uniwe radhi, nisamehe sana.”

Dudu Baya alitoa kauli hiyo dhidi ya Ommy Dimpoz wakati wa Tamasha la Miaka 30 ya Bongo Fleva lililofanyika Septemba 19, 2026 katika Viwanja vya General Tyre, Arusha.

29/09/2026

HT: MADAGASCAR 🇲🇬 0-1 TANZANIA 🇹🇿
⚽ Cyprian Kachwele 39'

Mchezo wa kufuzu AFCON 2027
Cc:🎥

MADAGASCAR 🇲🇬 VS TANZANIA🇹🇿 Angalia live mechi ya kufuzu AFCON Kwa kugusa Link hapa chini 👇 👇 https://www.youtube.com/li...
29/09/2026

MADAGASCAR 🇲🇬 VS TANZANIA🇹🇿 Angalia live mechi ya kufuzu AFCON Kwa kugusa Link hapa chini 👇 👇
https://www.youtube.com/live/pQieehaUETI?si=CUmmZNiLRBd7rMJJ

Enjoy the videos and music you love, upload original content, and share it all with friends, family, and the world on YouTube.

29/09/2026

Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Nchini (DCEA) imebaini uwepo wa watu wanaotumia misafara na magari ya kubebea misiba kusafirisha Dawa za Kulevya, hivyo kutoa onyo kali kwa wote wanaojihusisha na michezo hiyo michafu na kwamba operesheni kali dhidi yao inakuja.

Kamishna Jenerali wa DCEA Aretas James Lyimo amesema mamlaka hiyo, inafuatilia kwa karibu tarifa zake fiche, na kwamba pale itakapohitilafisha kuna watu wamefanya hivyo hawatasita kusimamisha misafara huo, na kwamba kuanzia gari lililo bobea misiba na wote wanaosindikiza watak**atwa.

Ametoa onyo hilo alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam leo, Jumatne Septemba 29, 2026, ambapo katika taarifa yake amesema pia mamlaka hiyo imebaini uwepo wa baadhi ya watendaji wasio waaminifu walio nje ya mamlaka yao wanaodaiwa kutumia mwanya wa udhibiti wa biashara hiyo haramu kuihushisha na vitendo vya rushwa na uhalifu.

Amesema baadhi ya watu hao wamekuwa wakiwalenga wahalifu wa biashara ya Dawa za Kulevya, kuwak**ata na kuwanyang’anya dawa hizo, kisha kuwashinikiza kutoa rushwa, jambo ambalo amelikenemea vikali na kuwata wahusika kuacha mara moja.

Aidha, katika eneo la ukaguzi wa abiria katika Bandari ya Dar es Salaam, DCEA imebaini matukio ya usafirishaji wa Dawa za Kulevya kupitia abiria, ambapo mbali na Watanzania waliok**atwa pia imewak**ata raia wa Uturuki akiwa na Gramu 1.87 za Bangi aina ya Skanka, raia wa Kenya akiwa na Gramu 3.89 za Mirungi na raia wa Nigeria akiwa na Gramu 4.6 za Bangi.

Sambamba na hilo, katika operesheni zilizofanyika Mkoani Arusha, raia wawili wa Afrika Kusini walik**atwa wakiwa na jumla ya Gramu 65.8 za Bangi aina ya Skanka.

Address

P. O. Box 977
Dar Es Salaam
255

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when PN Mediatz posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share

Category