Wakala TV

Wakala TV WAKALA TV
Entertainment • News • Lifestyle
Bringing stories to life
Tanzania
DM for promotions & collaborations

Shirika la Dawa Asilia na Ulinzi wa Mazingira Tanzania (TRAMEPRO) limetoa wito kwa wananchi, viongozi, waandishi wa haba...
28/09/2026

Shirika la Dawa Asilia na Ulinzi wa Mazingira Tanzania (TRAMEPRO) limetoa wito kwa wananchi, viongozi, waandishi wa habari na watumiaji wa mitandao ya kijamii kuhakiki taarifa kabla ya kuzisambaza, ili kulinda Umoja, Amani na Maendeleo ya Taifa.

TRAMEPRO imesema taarifa sahihi na za kuaminika zina mchango mkubwa katika kujenga uelewa, uwajibikaji, kulinda afya ya jamii na kuhifadhi mazingira.

Shirika hilo limetoa wito huo leo Septemba 28, 2026, wakati Tanzania ikiungana na dunia kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Upatikanaji wa Taarifa.

Aidha, TRAMEPRO imewasihi waandishi wa habari kuzingatia weledi na maadili ya taaluma, huku wananchi wakitakiwa kutosambaza taarifa ambazo hawajazithibitisha.

Umoja Tanzania Habari MitandaoYaKijamii UadilifuWaTaarifa

28/09/2026

WakalaTV Tanzania Inspirational UjumbeWaLeo

28/09/2026

Naibu Waziri wa Madini amewataka wachimbaji wadogo nchini kutokabidhi leseni zao kwa raia wa kigeni kwa kisingizio cha Technical Support.

Amesema msaada wa kiufundi unaruhusu wataalamu wa kigeni kutoa utaalamu, teknolojia na ujuzi, lakini si kuchukua na kuendesha shughuli za uchimbaji kwa kutumia leseni za Watanzania.

Kauli hiyo imetolewa wakati akifungua rasmi Maonesho ya 9 ya Teknolojia ya Madini mkoani Geita, akisisitiza wachimbaji kutumia fursa hiyo kuongeza ujuzi na uwezo wa kiteknolojia.
Wachimbaji Tanzania Serikali Teknolojia Habari BreakingNews WakalaTvInstagram

28/09/2026

Benki ya Azania imeingia mkataba na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kwa ajili ya kujenga vituo vya mafuta vijijini, hatua inayolenga kuwawezesha wachimbaji wadogo kupata huduma ya nishati kwa urahisi zaidi.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Maonesho ya 9 ya Teknolojia ya Madini Geita, Meneja wa Azania Bank Tawi la Geita, Rhoda Baluhya, amesema wachimbaji hao watanufaika na huduma hiyo kwa riba ya asilimia 5 tu.

💰 Aidha, Azania Bank inaendelea kutoa mikopo ya uwekezaji kwa ajili ya ujenzi wa migodi na mitambo ya kusafisha dhahabu (refinery).

🔥 Wachimbaji sasa mambo yameanza kubadilika!

UchimbajiMadini Dhahabu MiningTanzania WakalaTV Wakalatv1 Tanzania

27/09/2026

Katibu wa NEC, Idara ya Organizesheni CCM, Ndg. Paul Matiko Chacha, amewataka viongozi na wanachama wanaofanya makosa kutokujificha nyuma ya Chama Cha Mapinduzi.

Chacha amesema chama kitachukua hatua dhidi ya yeyote atakayekiuka Katiba, kanuni na taratibu za chama na jumuiya zake.

Aidha, amejibu hoja zinazoulizwa kuhusu alipo aliyekuwa Makamu wa Rais, Ndg. Emmanuel Nchimbi, akisema: “Mnaouliza yupo wapi, mmeenda nyumbani kwake mkamkosa?”

Amesema hayo Septemba 26, 2026, katika Mkutano Mkuu Maalumu wa CCM Mkoa wa Iringa, uliofanyika Ukumbi wa Ihemi.

Tanzania HabariLeo

27/09/2026

The Minister of State in the President's Office – Public Service Management and Good Governance, Hon. Ridhiwani J. Kikwete, has stated that the diplomatic relations between Tanzania and Germany have endured for a long time and are built upon foundations of mutual respect, genuine cooperation, and shared commitment.

25/09/2026

JETOUR Tanzania imezindua JETOUR Club na kutambulisha magari mawili mapya yenye teknolojia ya plug-in hybrid — JETOUR G700 na JETOUR F700.

Magari hayo yanaunganisha umeme na mafuta, yakilenga kuwapa Watanzania chaguo la usafiri wenye matumizi bora ya nishati kwa safari za mijini na masafa marefu.

Uzinduzi huo umefanyika chini ya kaulimbiu “Africa Expedition 2025”, kwa kushirikiana na Africarriers Group.

📍 Soma zaidi na tazama picha/video kupitia Wakala TV.

WakalaTV Tanzania

25/09/2026

Wanaume Wa Kisukuma ndo wanaume Wanao jua nini maana ya mwanamke, wanajua kuhudumia sana na kujali.
Mwanamke Mahusiano Upendo Uaminifu Heshima Wapenzi Tanzania❤️

25/09/2026

Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha, Dk. Nicas Mawazo, amewataka wamiliki wa viwanda kuhakikisha wanatunza mazingira yanayozunguka maeneo yao na kuacha shughuli zinazoweza kuathiri jamii.

Meya Mawazo amesisitiza umuhimu wa kusafisha mitaro, kujenga mifumo sahihi ya maji taka na kuhakikisha maji taka hayatorolewi kuelekea kwenye makazi ya wananchi.

Amesema hatua hizo zitasaidia kuzuia athari za kimazingira, ikiwemo mafuriko yanayosababishwa na kuziba kwa mitaro na mifumo ya maji.

MajiTaka Usafi Mafuriko Tanzania Habari BreakingNews NewsUpdate

24/09/2026

Address

Mbezi Beach
Dar Es Salaam
11101

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Wakala TV posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share