BONGO FM - TZ

  • Home
  • BONGO FM - TZ

BONGO FM - TZ official bongo FM radio page

90.0 DSM/Mwanza/Kilimanjaro
89.7 Dodoma/Mbeya/Tanga
89.9 Arusha/Morogo
(1)

WATAWAPIGA MPAKA MTAJE JINA LAO LA UTOTONI.Klabu ya Tabora United ya mkoani Tabora wamepoteza mchezo mmoja pekee katika ...
13/12/2024

WATAWAPIGA MPAKA MTAJE JINA LAO LA UTOTONI.

Klabu ya Tabora United ya mkoani Tabora wamepoteza mchezo mmoja pekee katika michezo yao minne na timu zinazoshika nafasi nne za juu katika ligi Kuu Tanzania Bara yaani Azam FC, Simba SC, Yanga SC na Singida BS.

Tabora United 2-1 Azam FC✅
Tabora United 2-2 Singida BS🤝
Yanga SC 1-3 Tabora United✅
Simba SC 3-0 Yanga SC❌

Kwa sasa Tabora United wanashika nafasi ya tano wakiwa na alama 24 baada ya kucheza michezo 14 wakishinda michezo saba, sare tatu na kupoteza michezo minne katika Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu.

Huu unaweza kuwa muda sahihi kwa Simba kutia nywele zao maji kwani watakutana uso kwa uso December 28 katika uwanja wa Ali Hassan Mwinyi huko mkoani Tabora.

Nani analijua jina lao la utotoni hawa jamaa?🥹😁

🖥

Ulimwengu wa burudani unazidi kuwa moto na Jana Crown FM 92.1 imezinduliwa na msanii wa muziki wa bongo freva Alikiba
10/03/2024

Ulimwengu wa burudani unazidi kuwa moto na Jana Crown FM 92.1 imezinduliwa na msanii wa muziki wa bongo freva Alikiba

Taja ngoma tatu kali kutoka Kwa King kiba 👑
09/03/2024

Taja ngoma tatu kali kutoka Kwa King kiba 👑

Unazungumziaje kuhusu tamko hili ?Endelea kufuatilia ukurasa wetu BONGO FM Kwa habari za kote duniani
09/03/2024

Unazungumziaje kuhusu tamko hili ?

Endelea kufuatilia ukurasa wetu BONGO FM Kwa habari za kote duniani

TAARIFA: kutoka shirika la umeme nchini
08/03/2024

TAARIFA: kutoka shirika la umeme nchini

Je Ulisha wahi KUDUKULIWA ? Na Hackers (WADUKUZI)Udukuzi mtandaoni ni mchakato wa kuingilia kati au kubadilisha mfumo wa...
07/03/2024

Je Ulisha wahi KUDUKULIWA ? Na Hackers (WADUKUZI)

Udukuzi mtandaoni ni mchakato wa kuingilia kati au kubadilisha mfumo wa kompyuta au mtandao bila idhini. Udukuzi ulianza kabla ya kompyuta, pale watu walipotumia njia za kudanganya simu ili kupiga simu za bure au kufanya utani. Baadaye, udukuzi ulihusisha kubadilisha vifaa vya kompyuta au programu ili kuongeza utendaji au kufungua huduma mpya. Udukuzi ulipata umaarufu zaidi katika miaka ya 1970 na 1980, pale makundi ya watu wenye ujuzi wa kompyuta walipojaribu kuingia kwenye mifumo ya serikali, makampuni, au mashirika mengine. Baadhi ya wadukuzi walikuwa na nia mbaya, k**a vile kuiba taarifa, kusababisha uharibifu, au kudai fidia. Wengine walikuwa na nia nzuri, k**a vile kugundua udhaifu wa usalama, kuboresha programu, au kuchangia elimu. Kuna aina tofauti za wadukuzi, kulingana na malengo na maadili yao. Wadukuzi weupe ni wale wanaotafuta mianya ya usalama kwa niaba ya wamiliki wa mifumo, na kupewa malipo kwa kazi yao. Wadukuzi weusi ni wale wanaotumia mianya ya usalama kwa manufaa yao wenyewe, kwa kukiuka sheria au maadili. Wadukuzi wa kijivu ni wale wanaoangukia katikati, ambao wanaweza kufanya udukuzi kwa sababu tofauti, k**a vile utafiti, changamoto, au uanaharakati. Udukuzi umekuwa changamoto kubwa katika ulimwengu wa kidijitali, hasa kutokana na ongezeko la matumizi ya intaneti, kompyuta ndogo, na vifaa vingine vinavyounganishwa na mtandao. Udukuzi unaweza kusababisha hasara kubwa za kifedha, kisheria, au kimaadili kwa watu binafsi, makampuni, au serikali. Udukuzi pia unaweza kutoa fursa za ubunifu, ufanisi, au ushirikiano kwa watu wenye ujuzi na shauku ya kompyuta. Udukuzi ni sehemu muhimu ya historia na maendeleo ya teknolojia, na unaendelea kubadilika na kukua kila siku.

JE UNGEPENDA KUJUA JAMBO GANI KUHUSU TECHNOLOGIES ?

endelea kufuatilia ukurasa wetu Kwa habari za kote duniani

Rais Samia Suluhu Hassan ameongoza kikao cha Baraza la Mawaziri kilichofanyika Ikulu Tunguu, Zanzibar. Katika kikao hich...
07/03/2024

Rais Samia Suluhu Hassan ameongoza kikao cha Baraza la Mawaziri kilichofanyika Ikulu Tunguu, Zanzibar. Katika kikao hicho, Rais ametoa maelekezo kuhusu utekelezaji wa mipango na miradi ya maendeleo, pamoja na kusimamia utawala bora na uwajibikaji

Endelea kufuatilia ukurasa wetu Kwa habari za kote duniani

Juzi ilikuwa siku ya kuzaliwa ya Maria Branyas Morera Alisherehekea siku yake ya kuzaliwa, alitimiza miaka 117  tarehe 4...
07/03/2024

Juzi ilikuwa siku ya kuzaliwa ya Maria Branyas Morera Alisherehekea siku yake ya kuzaliwa, alitimiza miaka 117 tarehe 4 Machi 1907 huko San Francisco, Marekani.

Alithibitishwa kuwa mtu mzee zaidi duniani mnamo Januari 2023
📸: Guinness World Records

Endelea kufuatilia ukurasa wetu Kwa habari za kote duniani

Dayoo Ndani ya Bongo FM endelea kufuatilia ukurasa wetu Kwa habari za kote duniani
07/03/2024

Dayoo Ndani ya Bongo FM endelea kufuatilia ukurasa wetu Kwa habari za kote duniani

Prince Dube rasmi ameaga kuondoka kwa matajiri wa chamazi Azam Fc. Unafikiri anaelekea wapi?Endelea kufuatilia ukurasa w...
07/03/2024

Prince Dube rasmi ameaga kuondoka kwa matajiri wa chamazi Azam Fc. Unafikiri anaelekea wapi?

Endelea kufuatilia ukurasa wetu Kwa habari za kote duniani

Mwanzilishi wa Amazon Jeff Bezos Thamani Ya Utajiri Wake  kwa sasa inafikia $200bn, ikizidi $198bn ya mkuu wa Tesla Elon...
07/03/2024

Mwanzilishi wa Amazon Jeff Bezos Thamani Ya Utajiri Wake kwa sasa inafikia $200bn, ikizidi $198bn ya mkuu wa Tesla Elon Musk, Ripoti ya Mabilionea ya Bloomberg ilionyesha Jumanne Huyu Ndiye Mtu Tajiri Zaidi Duniani Akifuatia Mkuu Wa TESLA Elon musk

Endelea kufuatilia ukurasa wa Bongo FM Kwa habari za kote duniani

Tuna sikiliza BONGO FM karibu katika Dunia mpya wewe unasikiliza Ukiwa wapi ?Fuatilia ukurasa wetu Kwa habari za kote du...
06/03/2024

Tuna sikiliza BONGO FM karibu katika Dunia mpya wewe unasikiliza Ukiwa wapi ?

Fuatilia ukurasa wetu Kwa habari za kote duniani

Address


Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when BONGO FM - TZ posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to BONGO FM - TZ:

Shortcuts

  • Address
  • Alerts
  • Contact The Business
  • Claim ownership or report listing
  • Want your business to be the top-listed Media Company?

Share