Proud Momy Era

Proud Momy Era Elimu ya lishe kwa watoto na wajawazito | uzazi salama na malezi🤰🏽
➡️ Follow & Contact Us Kwa Bidhaa Za Lishe
☎️ whatssap 0719481396 kuungwa group

Kujiunga na darasa la wajawazito,WhatsApp +255 719 481 396 ❤️
07/06/2026

Kujiunga na darasa la wajawazito,WhatsApp +255 719 481 396

❤️

30/05/2026
27/05/2026

Kujiaandaa kujifungua kunahusisha mwili, akili, na maandalizi ya mtoto ili siku ikifika uwe mtulivu na salama. Haya ni mambo muhimu ya kujiandaa:
1. Hudhuria clinic vizuri
Usikose miadi ya kliniki.
Fuatilia:
-presha
-sukari
-uzito wa mtoto
-maendeleo ya ujauzito

2. Andaa begi la hospitali mapema
Ni vizuri kuandaa kuanzia wiki ya 32–36.
Vitu muhimu:
-nguo za mtoto
-diapers
-wipes
-blanket
-pedi za uzazi
-nguo zako za kujifungulia
-chupi
-sabuni/toothbrush
-kadi ya clinic
-simu + charger

3. Kula vizuri na kunywa maji ya kutosha
-Matunda
-Mboga za majani
-Protini
-Vyakula vya kuongeza damu
Epuka kukaa muda mrefu bila kula.

4. Pumzika vya kutosha
Mwili unahitaji nguvu kwa ajili ya labor.
-Lala vizuri
-Epuka stress nyingi
-Punguza kazi nzito sana

5. Jifunze dalili za labor
Dalili zinaweza kuwa:
-maumivu ya tumbo ya kurudiarudia
-maji kutoka
-ute wenye damu kidogo
-mtoto kupungua kucheza sana
Ukiona hizi, wasiliana na hospitali.

6. Jiandae kiakili
-Hofu ni kawaida, lakini:
-Fikiria mambo mazuri
-Omba sana
-Ongea na watu wanaokutia moyo
-Epuka stories za kukutisha

7. Panga usafiri wa kwenda hospitali
-Usisubiri dakika za mwisho.
-Jua utaenda na nani
-Weka namba muhimu karibu

8. Jitayarishe baada ya kujifungua pia
-msaada wa nyumbani
-chakula
-Mahitaji ya mtoto
-Muda wa kupumzika

Mama wengi hujiandaa kujifungua lakini husahau kujiandaa kipindi cha baada ya kujifungua.
Naomba Mungu akupe afya njema, kujifungua salama, na mtoto mwenye afya ♥️

21/05/2026

Mama mtarajiwa, kumbuka hili wakati wa Labor 👇

-Jitahidi usipige kelele sana wakati wa uchungu wa kujifungua.Sio kwa sababu hauna maumivu, bali kwa sababu utulivu wako unasaidia mwili wako kufanya kazi vizuri zaidi.

● Faida za kuwa mtulivu wakati wa Labor:

• Inakusaidia kudhibiti pumzi zako vizuri
• Inapunguza uchovu usio wa lazima
• Inarahisisha mtoto kushuka vizuri
• Inakupa nguvu ya kusukuma kwa ufanisi zaidi
• Inawasaidia wauguzi na wakunga kukuongoza vizuri

●Badala ya kupiga kelele:
✔️ Vuta pumzi ndefu, toa polepole
✔️ Sikiliza maelekezo ya mtaalamu
✔️ Tumia nguvu yako kusukuma, sio kupiga kelele
✔️ Jipe moyo unaweza! 💪

Kumbuka: Maumivu ni ya muda, lakini furaha ya kumbeba mwanao ni ya milele ❤️

Darasa la wajawazito lipo kqenye offer,Piga/Whatssap 0719481396 Kulipia kwa bei ya Offer na uungwe🤗

21/05/2026

Wewe ni shujaa Mama💪

20/05/2026

“Mama mpendwa 🤰,
- kila siku unayopitia ni hatua ya kuumba maisha mapya.
-Umejaa nguvu, upendo na ujasiri usioonekana kwa macho.
-Jitunze, jipende, na ujikumbushe kuwa unafanya jambo la ajabu sana.

Wewe ni shujaa💪

Karibu darasa la wajawazito,Apendae mafundisho hupenda maarifa.

Piga/Whatssap 0719481396.

18/05/2026

GROUP LA WAJAWAZITO,ADA NI ELF 10 TU MWAKA MZIMA.

Wewe ni mjamzito au umeshajifungua na unahitaji kujifunza mambo mbalimbali kuhusu ujauzito,changamoto zake,maandalizi ya kujifungua na malezi??Karibu kwenye group letu la wajawazito na malezi ujifunze yote hayo.

Tunakukaribisha wewe ambaye unatarajia mtoto au unapanga kupata mtoto. Hapa, utapata ushauri, msaada, na ushirikiano kutoka kwa wataalamu na wanawake wengine ambao wamepitia au wanapitia uzoefu sawa na wewe.

Jiunge nasi ili:

- Kujua dalili za uchungu,kila mwili ni tofauti jifunze na ujue dalili zake
-Kujiandaa na uchungu na kujua mbinu mbalimbali za kustahimili uchungu
-Lishe kwa mjamzito na mama aliyetoka kujifungua ili kupata maziwa ya kutosha
-Kushiriki uzoefu wako na kupata ushauri kutoka kwa wengine
- Kupata habari za hivi punde kuhusu afya ya uzazi na utunzaji wa mtoto
-Njia sahihi za unyonyeshaji ili usihangaike na maziwa mbandala
- Kujifunza kutoka kwa wataalamu wa afya na wataalamu wengine
- Kupata msaada wa kihisia na ushirikiano kutoka kwa wanawake wengine
-namna nzuri ya kufanya saving ili usipate shida kwenye maandalizi ya kujifungua
-Afya ya akili n.k
-Maombi ya kuombea uzao na msaada wa kiroho.(ISAYA 35:3)

Jiunge nasi leo na uwe sehemu ya jumuiya yetu ya wajawazito!

DARASA HILI NI LA MWAKA MZIMA.

Piga simu au tuma ujumbe whatssap 0719481396.

Address

Dar Es Salaam

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Proud Momy Era posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share