12/10/2024
TIMIZA WAJIBU WAKO K**A MKRISTO!
10 mwenende k**a ulivyo wajibu wenu kwa Bwana, mkimpendeza kabisa; mkizaa matunda kwa kila kazi njema, na kuzidi katika maarifa ya Mungu;
Wakolosai 1:10
Colossians 1:10
[10]That you may walk (live and conduct yourselves) in a manner worthy of the Lord, fully pleasing to Him and desiring to please Him in all things, bearing fruit in every good work and steadily growing and increasing in and by the knowledge of God [with fuller, deeper, and clearer insight, acquaintance, and recognition].
Maandiko haya yanaonyesha wazi kwamba kumbe Mkristo sio mtu wa kuishi hovyo hovyo tu, au kuishi unavyotaka bila utaratibu flani, mkristo ni mtu ambae inambidi aishi kwa kufuata kanuni na utaratibu uliowekwa mbele yake.
Usiishi k**a mtu aliyepotea njia katika wokovu, yaani umejikuta tu upo katika safari ya watu waliookoka lakini wewe bado ni wa njia ile iliyo pana inayokubaliana na kila jambo baya na ovu hapa duniani. Na neno utakatifu kwako ni k**a kituo cha polisi.
K**a watu tulio okoka, tunao wajibu wa kufanya katika huu mtembeo wa wokovu. Mtume Paulo anasisitiza tuenende k**a ulivyo "WAJIBU WETU"
Hii ina maana kwamba baada ya kuokoa(kumkiri Yesu Kristo kuwa Bwana na mwokozi wa maisha yako), kila mtu anawajibu wa kufanya ili kumpendeza Mungu. Ni kweli tumeokolewa kwa NEEMA, lakini kuishi kwa kumpendeza Mungu ni wajibu wetu na ni chaguo letu na huo ndio mwitikio wa kwanza wa kuonyesha ya kwamba wewe, mimi, sisi tumeokolewa kwa Neema.
Wengi wetu bado tunaishi maisha ya dhambi, maisha ya kujichanganya, maisha ambayo yanamchukiza Mungu kwa kuendekeza tamaa za dunia hii, maisha ambayo hayana tofauti na maisha ya mtu asiyemjua Mungu kwa kisingizio kwamba tunaokolewa kwa neema na sio kwa matendo yetu. Tunasahau ya kwamba matendo yetu ndio ushahidi tosha wa kuonyesha mabadiriko chanya katika maisha yetu, matendo yanaonyesha kwamba wewe umetubu (umegeuza nia na kumfanania Kristo).
Katibu cha Tito 2 v 11-12, unasema...
"Maana neema ya Mungu iwaokoayo wanadamu wote imefunuliwa; nayo yatufundisha kukataa ubaya na tamaa za kidunia; tupate kuishi kwa kiasi, na haki, na utauwa, katika ulimwengu huu wa sasa"
Katika maandiko hayo 👆 tunaona wazi kwamba si kuokolewa kwa neema tu, bali hiyo neema ituokoayo, inatufundisha kuukataa ubaya wote na tamaa za dunia hii. Hiyo neema inatufundisha kuishi kwa kiasi, kuishi kwa haki, na kuishi kwa utakatifu.
Ni wazi kwamba ikiwa umeokolewa kwa neema basi utakuwa na sikio la kuisikia neema ikikufundisha kuukataa ubaya wote na tamaa za kidunia.
Sasa, wajibu wetu k**a watu tulio okoka na kuoshwa kwa damu ya Yesu Kristo ni kuitikia kile neema inatufundisha ili tuweze kumpendeza Mungu.
Ndugu zangu, tuishi tukitambua kwamba Yesu yu karibu kuwachukua watu wake, ninakusihi kwa jina la Yesu uwe ni mtu wa kuutekeleza wajibu wako wa kumpendeza Mungu kila iitwapo leo.
Chaguo ni lako, kuishi kwa kuendekeza tamaa za dunia hii, au kuishi kwa kumpendeza Mungu.
Barikiwa sana na Mungu kwa kusoma ujumbe huu mfupi.