14/09/2026
: Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amemteua Ndugu Hassan Ali Hassan kuwa Katibu wa Baraza la Wawakilishi.
Kabla ya uteuzi huo, Hassan alikuwa Mkurugenzi wa Idara ya Uandishi wa Sheria katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu. Aidha, Dkt. Mwinyi amewateua Ndugu Nassor Ahmed Mazrui na Ndugu Omar Said Shaaban kuwa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi.
Uteuzi huo umeanza rasmi tarehe 14 Septemba 2026, huku viongozi hao wakitakiwa kuripoti katika Baraza la Wawakilishi tarehe 16 Septemba 2026.