PR ICON

PR ICON kuwa updated na story kali na za kusisimua about PUBLIC RELATIONS ACTIVITY, SUPER BRAND COMPANY BEIN

DKT. MWINYI : AFRIKA SIO SOKO LA TEKNOLOJIA PEKEE, BALI IZALISHE YENYEWE ILI KUKIDHI MAHITAJI YA NDANI📍 ZANZIBAR. RAI hi...
01/10/2026

DKT. MWINYI : AFRIKA SIO SOKO LA TEKNOLOJIA PEKEE, BALI IZALISHE YENYEWE ILI KUKIDHI MAHITAJI YA NDANI

📍 ZANZIBAR.

RAI hiyo imetolewa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, wakati akifungua wa Hafla ya Uzinduzi wa Sera ya Kidigitali ya Zanzibar na Maonesho ya Teknolojia na Akili Unde (Tech and AI Expo Zanzibar 2026) , tarehe 29 Septemba 2026 - Golden Tulip Airport Hotel - Zanzibar.

"Afrika sio soko la kununua teknolojia pekee, bali pia inapaswa kuzalisha teknolojia yake yenyewe ili kuongeza miliki-bunifu, hakimiliki bunifu, na kujenga kituo shindani cha uwekezaji kitakachoratibu ulezi wa vipaji vya ndani."" Alisema Dkt. Mwinyi

Akifafanua zaidi, Rais Mhe. Dkt. Mwinyi amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) inajenga uchumi thabiti wa Kidigitali na imedhamiria kujenga uchumi ulio Imara, Jumuishi na unaoendeshwa kwa msingi bunifu ili kufikia maono ya Dira ya Zanzibar 2050 na Dira ya Taifa ya 2050.

Aidha, amebainisha kuwa ili kuhakikisha adhima hiyo inafanikiwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeanzisha Wizara mahsusi ya Mawasiliano, Teknolojia ya Habari na Ubunifu , imezindua Sera ya Kitaifa ya Kidijitali ya Zanzibar 2026 na kuandaa Mwongozo wa Kitaifa wa Matumizi ya Akili-Unde (Zanzibar AI Strategy Framework) itakayosimamia uwajibikaji wa teknolojia hizo , kukuza uchumi wa Zanzibar na kuimarisha upatikanaji wa huduma kwa Sekta ya umma.

"Mafanikio ya Mwongozo huu hayatakuja yenyewe, bali yanategemea kiasi kikubwa uwezo wetu wa kujiendesha na kujenga msingi imara wa miundombinu muhimu ya kidigitali, kusimamia Ubora na Usahihi wa Twakimu, kujenga rasilimaliwatu yenye ujuzi na maarifa, pamoja na kusimamia misingi ya Utawala Bora ili kuendelea kujenga imani kwa Wananchi " alisisitiza Dkt. Mwinyi.

Uzinduzi wa miongozo na Maonesho hayo unaweka alama muhumi ya Serikali katika kuwezesha ujenzi wa Uchumi imara wa kidigitali unafungamana na utekelezaji wa Dira ya 2050 - Zanzibar, Dira ya Taifa 2050 na Ajenda ya Umoja wa Barani Afrika - 2063 na STISA-2034 zote zikilenga kufungua fursa ya Ajira kwa Vijana wabunifu, wataalamu wa takwimu na wajasiriamali wa kidijitali ili kuchochea Mageuzi katika Sekta za Kimkakati k**a Utalii, Uchumi wa Bluu , Kilimo , Afya na Uimarishaji wa Huduma za umma.

30/09/2026

MHE. MCHENGERWA, ATOA MAAGIZO BODI MPYA YA WADHAMINI MUHIMBILI.

DAR-ES-SALAAM.

Waziri wa Afya Mhe. Mohamed Mchengerwa (mb) ameiagiza Bodi mpya ya Wadhamini ya Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kusimamia kwa karibu ubora wa huduma, uwajibikaji, matengenezo ya maboresho ya miundombinu ili kukamilisha utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa Muhimbili Mpya.

Mhe. Mchengerwa ametoa maagizo hayo leo tarehe 30 Septemba 2026 - Jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa Bodi ya Wadhamini ya Hospitali ya Taifa Muhimbili pamoja na miradi minne (4) ya kimkakati iliyotekelezwa na hospitali hiyo, inayojumuisha Ujenzi wa Vyumba vya Kisasa vya Upasuaji vya Mama na Mtoto, (Modular Theatre), Mtambo wa Kuzalisha na Kusambaza Hewa Tiba pamoja na gari maalum la kubebea miili ya wagonjwa.

Aidha, Mhe. Waziri amesema kuwa Bodi hiyo mpya imepewa dhamana kubwa ya kusimamia taasisi ambayo ni kituo cha mwisho cha rufaa nchini na yenye jukumu la kutoa huduma za kibobezi kwa wagonjwa kutoka maeneo mbalimbali.

“Bodi haiteuliwi ili ikae; inateuliwa ili isimame kwa ajili ya mgonjwa, isimame kwa ajili ya ukweli na isimame
hata pale ambapo kusimama kunagharimu,” amesema Mhe Mchengerwa.

DKT. NUNGU : TAFITI ZITOKE KWENYE MAABARA , SASA NI UTEKELEZAJI Windhoek - NAMIBIA. Serikali kupitia Tume ya Taifa ya Sa...
30/09/2026

DKT. NUNGU : TAFITI ZITOKE KWENYE MAABARA , SASA NI UTEKELEZAJI

Windhoek - NAMIBIA.

Serikali kupitia Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) imeongoza mjadala wa Uimarishaji wa Taasisi za kiafrika kupitia Mkutano wa Mwaka wa Mabaraza ya Sayansi, unaojumuisha Nchi wanachama 20 pamoja na Nchi Tano (5) zilizoomba kujiunga na Umoja wa Mabaraza hayo. Mkutano huo ulianza Tarehe 28 Septemba ukitarajia kutamatishwa tarehe 02 Oktoba 2026 - Jijini Windhoek- Nchini Namibia.

Akizungumzia nafasi ya Tanzania katika Ufunguzi ya Mjadala wa Kitaalamu ( Technical ) , Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Dkt. Amos Nungu ameyataka Mabaraza hayo kuondoa Tafiti katika Maabara, badala yake zitumike kupanga vipaumbele vya Maendeleo ya Taifa, Leo tarehe 30 Septemba 2026 huku akisisitiza kuwa wakati wa ahadi umepita na sasa ni wakati wa utekelezaji.

"Nguvu ya muungano wa Mabaraza ya Sayansi k**a SGCI, hupimwa kwa kile ambacho nchi na wanachama wake wanaweza kufanya pamoja, kwa umahiri na uthabiti wa hali ya juu" – Dkt. Amos Nungu

Aidha, Dkt. Nungu ameyataja maeneo matano (5) yanayohitaji uimarishaji , Kwanza ni Ufadhili wa Tafiti zinazojibu Vipaumbele vya Taifa husika, Pili, ni kuhakikisha Usimamizi wa Ufadhili wa Ruzuku unaendana na ongezeko la thamani ya Kila shilingi katika Tafiti ilete tija katika jamii husika.

Vilevile, Dkt Nungu ameongeza kuwa Eneo la Tatu (3) ni kuhakikisha Ujumuishi unatafasiriwa kwa vitendo ili kuwafikia wanufaika ambao ni kundi la Wanawake na Vijana na kuhakikisha matokeo-tafiti hayo yanatumika kutatua changamoto za jamii.

Eneo la Nne (4) , kuongeza wigo wa Mashirikiano wa diplomasia ya Sayansi inayojikita katika Afya , Chakula , Tabianchi na Maendeleo ya Teknolojia. Pia, Eneo la Tano (5) na la mwisho ni kuhakikisha kuna kuwa na Ujenzi wa miundombinu ya Uhifadhi wa Maarifa Ndani ya Taasisi za Mabaraza hayo.

Pia, ametoa Rai kwa Mabaraza hayo kubainisha maeneo yanayohitaji kujenga uwezo zaidi na kuimarisha mbinu za kujifunza kwa pamoja ili Mabaraza hayo yaweze kupima Mafaniko yao kwa shahidi zinaonesha jinsi gani Tafiti zinavyoboresha Maisha ya Watu.

Ujumbe wa Tanzania nchini Namibia unadhihirisha dhamira ya Serikali ya Tanzania kwa kuongeza Uwekezaji katika kuimarisha rasilimali-watu kuchochea Ajira, kukuza uchumi-maarifa na Maendeleo ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu ifikapo Mwaka 2050, na kufungamanishi Taifa la Tanzania na Utekelezaji wa Ajenda ya Umoja wa Afrika wa 2063 na STISA 2034 ili Tanzania iendelee kujiimarisha na isiishie kuwa mshiriki pekee bali ni nguzo imara ya ushirikiano wa kisayansi barani Afrika.

Awamu mpya ya SGCI ya miaka mitano, kuanzia 2026 hadi 2030, ina ahadi ya dola za Canada milioni 57, sawa na takribani dola za Marekani milioni 42, kwa shughuli za SGCI katika nchi zinazoshiriki. Dkt. Nungu amesema mafanikio ya mpango huo yanapaswa kuonekana katika uwezo wa taasisi kuendesha programu bora za utafiti, kuwafikia watafiti wengi zaidi na kutumia matokeo ya tafiti katika maamuzi yenye manufaa kwa wananchi. COSTECH ni mwanachama wa SGCI kwa upande wa Tanzania.

VETA YAWAFUNGULIA VIJANA MLANGO WA AJIRA MIGODINIGEITA. Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) imesema inaan...
30/09/2026

VETA YAWAFUNGULIA VIJANA MLANGO WA AJIRA MIGODINI

GEITA.

Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) imesema inaandaa vijana wenye ujuzi unaoendana na mahitaji ya sekta ya madini, hususan uendeshaji wa mitambo. Kauli hiyo imetolewa tarehe 29 Septemba 2026 na Afisa Mkuza Mitaala wa VETA, Mhandisi Audiface Tarimo, wakati wa Maonesho ya Tisa (9) ya Kitaifa ya Teknolojia ya Madini yanayoendelea mkoani Geita.

Kwa kushirikiana na Chama cha Watoa Huduma Sekta ya Madini Tanzania na Mamlaka hiyo ya VETA imeandaa mitaala sita (6) mipya inayojumuisha: Bogie Operation, Jumbo Operation, Solo Operation, Cubex Operation, Charge Up Operation, na Lifting and Rigging, huku Mafunzo hayo yakitarajiwa kuanza rasmi katika Chuo cha Mamlaka ya Elimu na Mafunzo - VETA Moshi.

Aidha, baadhi ya wakufunzi wa VETA wamepata mafunzo nchini Finland na sasa wanawanoa walimu wenzao nchini ili kuwafikia vijana wengi zaidi na kuwawezesha kunufaika na fursa za sekta ya madini.

PROF. NOMBO : TUMEPATA UJUZI, WAFADHILI NA FURSA MPYA KWA VIJANA NA WALIMU NCHINI CHINA. SHANGHAI, CHINA. Katibu Mkuu wa...
29/09/2026

PROF. NOMBO : TUMEPATA UJUZI, WAFADHILI NA FURSA MPYA KWA VIJANA NA WALIMU NCHINI CHINA.

SHANGHAI, CHINA.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia (WyEST), Prof. Carolyne Nombo, amesema Tanzania inajivunia kuwa miongoni mwa nchi zilizochaguliwa kushiriki Jukwaa la Kimataifa la Mashindano ya Ujuzi Duniani (World Skills Competition) , tarehe 28 Septemba 2026 yanayofanyika Shanghai, China.

Amesema maandalizi ya ushiriki huo yalianzia Jijini Tanga wakati wa Wiki ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu iliyoratibiwa kuanzia tarehe 15 - 24 Agosti 2026, ambapo Vijana wa Kitanzania walishindana katika fani tisa (9) na washindi hao wanaandaliwa kushiriki ngazi ya Afrika kisha ngazi ya dunia.

Prof. Nombo ameeleza kuwa ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na Mhe. Lela Mohammed M***a, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, umeshiriki mikutano na warsha mbalimbali (side-talks) na kujifunza namna-bora ya uendeshaji mashindano hayo kwa viwango vya kimataifa.

"Cha muhimu zaidi, k**a Tanzania tumejifunza namna ya kupanga mashindano haya kulingana na vigezo vilivyowekwa kimataifa," amesema.

Katibu Mkuu huyo amezungumzia pia kutanuka kwa wigo na diplomasia ya Uwekezaji katika Sekta ya Elimu kwa kuelekeza kuwa Ziara hiyo, imezaa matunda na kufungua milango ya ushirikiano na wafadhili wakubwa, zikiwemo kampuni za SoftTech, FESTO, Samsung na Bosch k**a Kampuni pekee za kigeni zilizoonesha utayari wa kushirikiana na Wizara hiyo katika maandalizi ya mashindano ya ndani ya nchi na uendelezaji wa rasilimali ya ndani yenye ujuzi kwa vijana.

Ujumbe huo pia ulilenga kuimarisha zaidi uwezo wa walimu kufundisha masomo ya Sayansi, Teknolojia , Uhandisi na Hisabati - STEM na kufanikiwa kutembelea Kituo cha Kambi Maalumu ya Mafunzo ya Walimu kinachotambuliwa na UNESCO kilichopo Chuo Kikuu cha Shanghai Normal. Aidha, Pande hizo mbili (2) zimekubaliana kuimarisha mafunzo kwa walimu wa masomo ya STEM. Prof. Nombo amesema hatua hii inaendana na maboresho ya Sera na Mitaala nchini.

"Mkiona matokeo ya Sayansi yakitangazwa, kuna uboreshaji wa ufaulu. Hii haiji kwa bahati mbaya, bali kwa sababu Serikali imewekeza katika mafunzo," ameongeza.

Aidha, timu hiyo imekiri kuwa matumizi ya Teknolojia ya Darasa-Janja imesaidia kiasi kikubwa kupunguza Uhaba wa Walimu mara baada ya kukutana na kampuni ya Edu-Tech ikiwa ni kampuni pekee ambayo tayari imesaidia uwekaji wa madarasa janja kwa baadhi ya Shule na Taasisi. Teknolojia hiyo imerahisisha ufundishaji wa masafa marefu kwa kuwezesha mwalimu mmoja kufundisha shule zaidi ya moja kwa wakati mmoja, hivyo kupunguza uhaba wa walimu wa Sayansi. Hivyo Serikali inaendelea kufanya Majadiliano na wadau hao ili kupanua mpango uweze kunufaisha zaidi sekta hiyo ya Kimkakati ifakapo mwaka 2050.

Prof. Nombo amehitimisha kwa kusema ushiriki huu unaendana na Sera ya Elimu na Mafunzo ya 2014, Toleo la 2023, pamoja na Dira 2050, zinazolenga kuzalisha Watanzania wenye ujuzi.

"Vijana wa Kitanzania wajue jukwaa la kimataifa lipo kwa ajili yao pia," amesisitiza.

NDEJEMBI: "TUJINYIME, TUAJIRI VIJANA 10,000!"ARUSHA | Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius...
28/09/2026

NDEJEMBI: "TUJINYIME, TUAJIRI VIJANA 10,000!"

ARUSHA |

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius Ndejembi, amewaagiza Wenyeviti wa Bodi na Wakuu wa Taasisi na Mashirika ya Umma kuweka mazingira wezeshi na kupunguza matumizi ya Serikali ili kutoa ajira kwa vijana 10,000 hatua inayolenga kuwajengea uwezo rasilimaliwatu ya ndani kuelekea utekelezaji wa Dira ya 2050.

Mhe. Ndejembi ametoa agizo hilo alipokuwa akihutubia Kikao Kazi cha Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa Taasisi na Mashirika ya Umma ( C- CEO Forum) , Leo tarehe 28 Septemba 2026 - Ukumbi wa Kituo cha Mikutano ya Kimataifa- AICC - Jijini Arusha .

Akifafanua mpango huo, Makamu wa Rais amependekeza vijana 10,000 wenye taaluma tofauti hususani wahandisi ili wapelekwe kwenye Taasisi za Umma ili kupata ujuzi kwa vitendo.

"Tuchukue vijana 10,000, ma-engineer, tuwapeleke TANESCO, TPA, TANROADS au popote kule. Serikali inaweza kuwalipa shilingi TZS laki tano (5) , laki saba (7) au milioni moja (1). Hiyo ni sawa na shilingi bilioni 120 kutoka kwenye trilioni 1.3 ili kuweza kuwanoa vijana wetu kwa gharama ndogo na Faida ni kubwa kwa Taifa" alisisitiza

Mhe. Ndejembi ameongeza kuwa gharama hiyo ni uwekezaji wa muda mrefu na mpango huo unaweza kufanikiwa endapo Serikali itaamua kubana matumizi yasiyo ya lazima.

"Gharama hii tukijinyima, tunakwenda kuandaa 'workforce au human capital ya Tanzania' ambayo ndiyo inakwenda kujenga uchumi wa Taifa letu," ameongeza.

Makamu wa Rais ameeleza kuwa fedha hizo zinaweza kupatikana endapo viongozi wataamua kujinyima na kuamua kusitisha matumizi yasiyo ya lazima k**a michapalo, gala dinners na ziara za mafunzo (study tours) nje ya nchi. Amesema uamuzi huo unaweza kulivusha Taifa na kupanua wigo wa uwekezaji katika kuwanoa rasilimaliwatu wa nchi.

RAIS SAMIA AMSHIKA MKONO , BINTI MBUNIFU WA TEKNOLOJIA YA KILIMO YA NDEGE NYUKI (DRONES).  Dodoma. Rais wa Jamhuri ya Mu...
26/09/2026

RAIS SAMIA AMSHIKA MKONO , BINTI MBUNIFU WA TEKNOLOJIA YA KILIMO YA NDEGE NYUKI (DRONES).

Dodoma.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amempatia mbunifu kijana, Ndg. Tarsila Mellita kiasi cha Shilingi Milioni TZS. 20 ili kuendeleza bunifu ya teknolojia ya ndege nyuki (drones) za kunyunyizia viuatilifu katika mashamba makubwa nchini.

Rais Samia alitimiza ahadi hiyo kupitia mwakilishi wake, aliyeitoa wakati akitembelea Mabanda ya kilele cha Maonesho ya 33 ya Kilimo (Nanenane), Siku ya Tarehe 8 Agosti 2026, yaliyofanyika katika Viwanja vya John Samuel Malecela, Nzuguni, Jijini Dodoma.

Katika maonesho hayo, Tarsila alimweleza Mhe. Rais kuwa drone ya mfano (prototype) aliyoibuni iligharimu Shilingi Milioni 4.5. Aliomba Shilingi Milioni TZS 20 ili kutengeneza drone kubwa zaidi yenye uwezo wa kubeba lita 20 za viuatilifu ili Teknolojia hiyo iwezeshe wakulima kunyunyizia mashamba makubwa kwa haraka, usahihi na gharama nafuu hatimae kuchangia ukuaji wa Sekta hiyo ya Kimkakati ifakapo mwaka 2050.

Akizungumza baada ya kupokea fedha hizo, Tarsila, ambaye ni mbunifu kutoka kampuni ya Nyika Venture, alitoa shukrani zake kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa usaidizi huo.

"Tuna furaha kubwa sana kwa Mhe. Rais kumtuma mwakilishi wake kutukabidhi ahadi ya Shilingi Milioni 20 aliyotuahidi. Sisi k**a Nyika-Venture tunayo furaha kubwa kwasasa tunaweza kutengeneza drone kubwa zaidi. Tunamshukuru sana Mhe. Rais kwa kutuona na kutushika mkono sisi vijana. Kwasasa Kilimo Si lazima kushika jembe shambani, ila tukitumia teknolojia tunaweza kufanya kilimo kwa urahisi," alisema Tarsila.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Ndg. Gerald Mweri, alimshukuru Mhe. Rais kwa kutimiza ahadi hiyo. Aliahidi kuwa Wizara itaendelea kutoa fursa kwa vijana wengi zaidi kutumia ujuzi na ubunifu wao katika kuendeleza sekta ya kilimo nchini.

Hatua hii inaonesha dhamira ya Serikali kutanua wigo wa Uwekezaji, Matumizi na Maendeleo ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu kwa vijana k**a nguzo ya kilimo cha kisasa na kuthibitisha bunifu za ndani zinaweza kutoa suluhisho halisi kwa changamoto za wakulima wa Kitanzania.

MITIHANI YA TAIFA YASONGEZWA MBELE KUKWEPA EL-NINO. Dar es Salaam – Serikali imesogeza mbele ratiba ya Upimaji na mitiha...
25/09/2026

MITIHANI YA TAIFA YASONGEZWA MBELE KUKWEPA EL-NINO.

Dar es Salaam –

Serikali imesogeza mbele ratiba ya Upimaji na mitihani ya Taifa ya mwaka 2026 kutoka ratiba ya awali kufanyikia Novemba kuhamishiwa Mwezi Oktoba - 2026 ili kutekeleza Agizo la kudhibiti athari zinazoweza kujitokeza mara baada ya utabiri wa Hali ya Hewa ya uwezekano wa kuongezeka kwa mvua kubwa za El-Niño kuonesha athari kubwa msimu wa vuli.

Hayo yamebainishwa na Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Wanu Hafidh Ameir alipozungumza na waaandishi wa Habari, Leo 25 Agosti 2026 - Jijini Dar es salaam. Aidha, Hatua hiyo inalenga kulinda usalama wa wanafunzi, walimu, wasimamizi pamoja na vifaa na nyaraka za mitihani.

Mhe. Wanu ameeleza kuwa uamuzi huo umetokana na taarifa rasmi ya utabiri iliyotolewa tarehe 18 Agosti 2026 na baadae tahadhari iliyotolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu tarehe 2 Septemba 2026 ilielekeza Mamlaka husika kuchukua hatua za haraka baada ya utabiri kuonesha uwezekano wa El-Niño itakayoathiri kuanzia Oktoba 2026 hadi Januari 2027, huku mwezi Novemba ukitarajiwa kuwa na mvua nyingi zaidi.

Kwa mujibu wa utabiri huo mvua hizo zinatarajiwa kuanza wiki ya nne (4) ya Septemba mpaka kwanza(1) ya Oktoba 2026 kwa Kanda ya Ziwa Victoria inayojumuisha Mikoa ya Kagera, Geita, Mwanza, Shinyanga, Simiyu na Mara, pamoja na mkoa wa Kigoma upande wa Magharibi. Vilevile, Mikoa ya Kaskazini ikijumisha Arusha, Manyara na Kilimanjaro, mvua zinatarajiwa kuanza kati ya wiki ya kwanza (1) na ya pili (2) ya Oktoba 2026.

Aidha, Mhe Wanu ameeleza kuwa Kutokana na hali hiyo, Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) limefanya marekebisho ya Upimaji wa Kitaifa wa Darasa la Pili (2) , Darasa la Nne (4) na Kidato cha Pili (2) unaotarajia kufanyika mwezi Oktoba 2026. Aidha, Mtihani wa Kidato cha Nne (4) utaanza Oktoba 2026 na kukamilika mwanzoni mwa Novemba 2026.

Mhe. Wanu alibainisha athari za kimazingira, miundombinu na Afya zinaweza kuharibu barabara, kuchelewesha usafirishaji wa mitihani vituoni, kusababisha kukatika kwa umeme na huduma za mawasiliano, pamoja na kuathiri usafi, vyoo na upatikanaji wa maji safi katika vituo vya usimamizii wa mitihani.

Naibu Waziri huyo amesisitiza kuwa Upimaji wa Mitihani Kitaifa unahusisha zaidi ya Shule 21,353 kwa Upimaji wa darasa la Kwanza (1) na Darasa la Nne (4) na Upimaji wa Kidato cha Pili (2) utahusisha Shule 21008, huku athari hizo zikitarajiwa kuathiri idadi kubwa ya wanafunzi chini ya umri wa miaka 11, hivyo Wizara inachukua hatua hizo ili kuwawekea mazingira salama na rafiki kwa Wanafunzi wa shule za kutwa na watahiniwa wa kujitegemea kudhibiti athari hizo endapo mafuriko na changamoto za usafiri zingejitokeza.

Mhe. Wanu ametoa Wito kwa Kamati za Mitihani za Mikoa na Halmashauri pamoja na wakuu wa shule kushirikiana kwa karibu na Wizara na NECTA ili mitihani iendeshwe kwa ufanisi, utulivu na usalama. Vilevile, ameahidi kuwa Wizara itaendelea kushirikiana na Mikoa, Halmashauri na wadau wengine ili kuhakikisha maandalizi yote yanakamilika kwa wakati, pamoja na kuwasihi wanafunzi, wazazi na walezi kufuatilia taarifa rasmi, huku ratiba kamili ikitarajiwa kutangazwa na Katibu Mtendaji wa NECTA.

ARUSHA: WANUFAIKA 50 WA SAMIA SCHOLARSHIP, WAINZA SAFARI YA KITAALUMA KWA KISHINDO. Na F.A, ArushaNaibu Waziri wa Elimu,...
24/09/2026

ARUSHA: WANUFAIKA 50 WA SAMIA SCHOLARSHIP, WAINZA SAFARI YA KITAALUMA KWA KISHINDO.

Na F.A, Arusha

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Wanu Hafidh Ameir, amesema Serikali itaendelea kuhakikisha Vijana wa Kitanzania wanapata maarifa na ujuzi ili kukidhi Ujenzi wa Uchumi kidigitali kupitia program ya Samia ScholarshipExtendedDS/AI+ kwenye Sayansi twakimu (Science Data) na Akili Unde (AI), tarehe 23 Septemba 2026 jijini Arusha.

Mhe. Wanu amewapongeza wanufaika hao 50 waliochaguliwa kujiunga na program hiyo, huku akionesha furaha yake ya Ongezeko la Wasichana kujiunga na Masomo ya Sayansi kutoka ongezeko la Asilimia 14 kwa kundi la awali lililobeba idadi ya Wasichana Saba (7) kwa Mwaka 2025/26, hadi kufikia ongezeko la Asilimia 18 kwa ongezeko la idadi ya wasichana kufikia Tisa (9) kwa Mwaka huu wa Fedha. Wanufaika hao wamepiga kambi maalum ya mafunzo chuo cha Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela (NM-AIST).

Aidha, Mhe. Wanu amewasihi wanufaika hao kujifunza kwa wivu mkubwa na bidii ya hali ya juu ili kutumia vizuri nafasi hiyo adhimu kwa kujijengea nidhamu, maarifa, na kuacha utamaduni wa Sekondari bali wajiandae Kitaaluma za Chuo Kikuu ili mchango wao usaidie Taifa kufikia maono na msingi wa Dira 2050.

"Niwapongeze kwa bidii mliyoionesha shuleni. Muendelee nayo hapa, kwa sababu nafasi hizi ni chache na ni wachache sana wanaopata fursa hii," amesema Mhe. Wanu.

Kwa upande wake, Makamu Mkuu wa Taasisi ya NM-AIST, Prof. Maulilio Kipanyula, amesema wanufaika hao waliripoti chuoni hapo tarehe 14 Septemba 2026, wanataraji kupokea mafunzo kwa kipindi cha miezi 10 ili kuwajengea tabia za kizalendo na kuwaandaa kwa mazingira ya taaluma na kazi mara baada ya kufanya mtihani wa awali ya Kiingereza na Hisabati ili kubaini maeneo ambayo kila mwanafunzi anahitaji msaada zaidi.

"Tutaleta wakufunzi mbalimbali watakaowapitisha katika maeneo muhimu kabla ya kwenda kusoma shahada za kwanza nje ya nchi," amesema Prof. Kipanyula.

Akizungumza kwa niaba ya wanufaika, Ndg. Lewis Mwasha na Ndg. Laurencia Thobias wameishukuru Serikali kwa kuendelea kutoa ufadhili wa masomo hayo ya Sayansi kwa Vyuo Vikuu mahiri vya Nje ya Nchi ili vijana hao waweze kujikwamua na hatimae kufikia Maendeleo ya Taifa na kuahidi kutambua Uwekezaji unaofanywa na Serikali kuchochea Maendeleo ya Sekta ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ili kuchangia uchumi wa sasa na wa baadaye.

"Tunaipongeza sana Serikali yetu na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, na kwa kipekee tunampongeza Mama Samia kwa kuamua kuwekeza kwetu sisi vijana," amesema Mwasha.

UWEKEZAJI: TEKNOLOJIA , RASILIMALI-WATU, NA   MIUNDOMBINU, VYAINNG'ARISHA TANZANIA KWA ASILIMIA 80 UMOJA WA  KIMTAIFA. N...
23/09/2026

UWEKEZAJI: TEKNOLOJIA , RASILIMALI-WATU, NA MIUNDOMBINU, VYAINNG'ARISHA TANZANIA KWA ASILIMIA 80 UMOJA WA KIMTAIFA.

NEWYORK, Marekani.

Na F.A ,

Hayo yamebainishwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius Ndejembi alipomwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Mkutano wa 81 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA81), Tarehe 22 Septemba 2026 - Makao Makuu , Newyork- Marekeni.

Mhe. Ndejembi amesema Taifa hilo limepiga hatua kwenye uimarishaji wa Sekta ya Afya kupunguza vifo vya mama na mtoto kwa kipindi cha miaka Saba (7) toka Asilimia 51 kwa Mwaka wa Fedha wa 2015 hadi Asilimia 81 kwa Mwaka wa Fedha 2022 jambo ambalo limeiheshimisha nafasi ya Tanzania Kimataifa na kumfanya Mhe. Rais Samia na kuwa Kinara wa Afya ya Mama na Mtoto katika Anga la Umoja wa Nchi za Afrika.

Makamu wa Rais ametangaza kuwa Tanzania ikichaguliwa kugombea Kiti Kisicho cha kudumu cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ( Non-payment UN Security Council) kwa kipindi cha 2029 - 2030 itasimamia diplomasia ya Uzuiaji migogoro, Utatuzi wa migogoro kwa amani, kuongeza wigo wa Ushiriki wa wanawake na vijana katika amani, na mageuzi ya ulinzi wa amani.

Aidha, Mhe. Ndejembi ameelekeza kuwa Serikali ya Tanzania imeendelea kuimarisha Uwekezaji kwenye Nishati Safi na Mabadiliko ya Tabianchi na Upatikanaji wa nishati hiyo kupitia ongezeko la Uzalishaji wa Bwawa la Julius Nyerere - JNHPP linalozalisha jumla ya megawati 2,115 sawa ongezeko la Asilimia 46% , Umeme Jua na Upepo kuzalisha megawati 650 sawa na ongezeko la Asilimia 14% , na Jotoardhi megawati 130 sawa na ongezeko la Asilimia 3%, huku Tanzania ikilenga ongezeko hilo kufikia asilimia 80 ifikapo Mwaka 2034, na fedha zaidi zinahitajika zaidi kudhibiti na kuongeza uhimilivu wa mabadiliko ya tabianchi kwa njia ya ruzuku, mikopo nafuu, na msaada wa Kiteknolojia ifikapo Mwaka 2050.

Kwa Upande mwingine, Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) itaendelea kuiunga Mkono Serikali kuweka mazingira-wezeshi ya ufhadhili wa Tafiti za Mabadiliko ya Tabianchi, Mazingira, kushajihisha matumizi ya teknolojia mpya. Jumla ya Tafiti 50 zilizokwishafadhiliwa kupitia fungu la uhimilivu wa mazingira na Serikali ilishatenga jumla Bilioni 6.3 kuongeza uhimilivu na jumla ya wakulima 15000 ya mifumo mbadala wa nishati ya Jua kwa ajili ya umwagiliaji (Solar-powered Irrigation).

Address

Kimara
Dar Es Salaam
1061

Telephone

+255719831083

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when PR ICON posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to PR ICON:

Shortcuts

Share