10/09/2025
SAMIA AAPA KUIPANDISHA IGUNGA VIWANGO: HOSPITALI, MAJI NA BARABARA KWA WANANCHI
Mgombea Urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Samia Suluhu Hassan, amewahamasisha wananchi wa Igunga kuunga mkono utekelezaji wa Ilani ya CCM 2025, akisisitiza mafanikio yaliyopatikana na kutoa ahadi mpya za maendeleo zinazolenga kuboresha maisha ya kila mwananchi.
Dkt. Samia alisema wilaya ya Igunga imepata mafanikio makubwa katika sekta ya afya, ikiwemo ukarabati wa Hospitali ya Halmashauri na kukamilika kwa ujenzi wa jengo la wagonjwa mahututi, jambo lililoleta huduma bora kwa wagonjwa. Katika sekta ya elimu, idadi ya shule za msingi na sekondari imeongezeka, huku Chuo cha Elimu na Mafunzo ya Stadi (VETA) kikiwa ni jukwaa muhimu la kuwajengea vijana ujuzi wa kiufundi na stadi za maisha.
Sekta ya kilimo na biashara imeimarishwa kwa ongezeko la uzalishaji wa mazao ya chakula, upatikanaji wa mbolea na kuendelezwa kwa viumbeaji na uzalishaji wa vifaranga vya samaki. Aidha, mtandao wa barabara mjini na vijijini umeboreshwa, kurahisisha usafirishaji wa wananchi na bidhaa zao, jambo linaloongeza mapato na fursa za biashara.
Baada ya kufafanua mafanikio, Dkt. Samia alitoa ahadi zinazolenga kusukuma mbele maendeleo. Ahadi hizo ni pamoja na ujenzi wa vituo viwili vya afya Uswaya na Kining’inila, ukamilishaji wa maboma ya madarasa 180 katika shule za msingi, maboma ya maabara 20 katika shule za sekondari, na nyumba 37 za walimu.
Zaidi ya hayo, Dkt. Samia aliahidi ujenzi wa mabwawa na skimu katika vijiji vya Igurubi, Buhekela, Simbo, Itumba, Mwamapuli, Mwalunili, Makomelo na Mwashiku, pamoja na ujenzi wa Soko Kuu la wafanyabiashara wadogo na wakubwa, kuboresha maeneo ya uwekezaji, na kukamilisha maboma ya majosho 15 pamoja na mabirika ya kunyweshea mifuko 3.
Katika sekta ya michezo, ujenzi wa kiwanja cha michezo cha Halmashauri na jengo jipya la ofisi za Halmashauri unaendelea, kuimarisha burudani, michezo na utendaji bora wa utawala