seeker.tz

seeker.tz Balozi wa
Talented | video & habari za Simbasc

𝗗𝗢𝗡𝗘 𝗗𝗘𝗔𝗟✅Taarifa za ndani zinasema Tajiri wa Klabu ya SimbaSC ndugu Mo Dewji amewaomba viongozi wa timu hiyo wahakikish...
07/04/2025

𝗗𝗢𝗡𝗘 𝗗𝗘𝗔𝗟✅

Taarifa za ndani zinasema Tajiri wa Klabu ya SimbaSC ndugu Mo Dewji amewaomba viongozi wa timu hiyo wahakikishe kijana anavaa Jezi nyekundi msimu ujao pale Msimbazi😂

Kijana yupo tayari anasubiri Mabosi tu waamue, Simba na Mzee Bahresa ni simu moja tuuu.

Kila la kheri Maestro Feisal Salamu⚽

LEO ATEBA AJIONGEZEA MUDA WA MAZOEZI KUIVUSHA SIMBA MBELE YA AL MASRYMshambuliaji wetu mahiri na namba moja wa timu yetu...
07/04/2025

LEO ATEBA AJIONGEZEA MUDA WA MAZOEZI KUIVUSHA SIMBA MBELE YA AL MASRY

Mshambuliaji wetu mahiri na namba moja wa timu yetu ya Simba Sc Leo Ateba ameamua kujiongezea Dozi ya Mazoezi kuelekea mechi na Al Masry

👉Ateba amepania kufanya makubwa kuelekea mchezo huo kwa maslahi mazuri kwa timu yetu na Mashabiki wa Mnyama.

Ateba bado anayo nafasi ya kufanya vyema kuelekea mchezo wetu wa marudiano
Tumsapoti mwenetuuu hii tunaenda kuipambania kwa nguvu Moja na kuvuka pamoja 🔥

🔴

Simba Queens iko kwenye mpango wa kuachana na Kocha Mkuu, Yussif Basigi mwishoni mwa msimu huu kutokana na kile alichoki...
07/04/2025

Simba Queens iko kwenye mpango wa kuachana na Kocha Mkuu, Yussif Basigi mwishoni mwa msimu huu kutokana na kile alichokionyesha Ligi Kuu kutowaridhisha mabosi wa timu hiyo.

Kocha huyo aliyejiunga na Simba akitokea Hasacaas Ladies ya Ghana na ukiwa ni msimu wake wa kwanza kwenye ligi, amepoteza mchezo mmoja dhidi ya Yanga Princess na sare mmoja dhidi ya JKT na ameshinda 12.

Basigi alichukua mikoba ya Juma Mgunda aliyebeba ubingwa wa WPL msimu uliopita bila ya kupoteza mchezo wowote akiifunga Yanga na JKT nyumbani na ugenini, kabla ya kutimkia Namungo.

Kikosi cha Simba jana kilikamilisha maandalizi yake katika mji wa Ismailia kuelekea mchezo wa mkondo wa kwanza robo fain...
01/04/2025

Kikosi cha Simba jana kilikamilisha maandalizi yake katika mji wa Ismailia kuelekea mchezo wa mkondo wa kwanza robo fainali ya kombe la Shirikisho la CAF dhidi ya Al Masry ambao utapigwa kesho Jumatano

Simba ilikamilisha maandalizi yake katika uwanja wa Suez Canal ambapo leo kikosi kinaelekea mji wa Suez ambako mchezo huo utapigwa

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba Ahmed Ali amesema kikosi kitaondoka Ismailia majira ya mchana kuelekea Suez mji ulioko umbali wa kilomita 80 kutoka Ismailia

"Tumekamilisha maandalizi yetu hapa Ismailia na leo majira ya mchana timu itaondoka hapa kuelekea mji wa Suez ambao ni umbali wa kilomita 80 mwendo wa masaa mawili hivi

"Jioni timu itafanya mazoezi ya mwisho katika uwanja wa Suez ambao utatumika katika mchezo wa kesho," alisema Ahmed

Kikosi cha Simba kimefanya mazoezi ya kwanza tangu kimefika Misri hapo jana Usiku kuelekea mchezo wao dhidi ya Al Masry
29/03/2025

Kikosi cha Simba kimefanya mazoezi ya kwanza tangu kimefika Misri hapo jana Usiku kuelekea mchezo wao dhidi ya Al Masry

26/03/2025

SIMBA YATANGAZA WACHEZAJI HAWA KUKOSA MCHEZO WA KESHO

23/03/2025

Magoli yote ya Simba Sc 4 vs 0 Kmc hapo jana mchezo wa kirafiki

Huyu Ahoua na Mutale wana balaaa sanaaaaaaaaaaaaaaa

23/03/2025

Tazama Goli la Nne la Simba dhidi ya Kmc angalia Mutale alivyokimbia na Mali 🔥🔥🔥🔥🔥

Matokeo ya Mchezo wa Kirafiki | Simba SC 4️⃣ vs 0️⃣ Kmc | Ateba kaweka mara Mbili 🔥 🔥Ateba⚽️⚽️Balua ⚽️Mashaka ⚽️🔗 Ila hu...
22/03/2025

Matokeo ya Mchezo wa Kirafiki | Simba SC 4️⃣ vs 0️⃣ Kmc | Ateba kaweka mara Mbili 🔥 🔥

Ateba⚽️⚽️
Balua ⚽️
Mashaka ⚽️

🔗 Ila huyu mtoto Mashaka wamwangalie kwa jicho la pili anajua goli lilipo

SASA NI MUDA WA FIFA KUJA BONGO NAPO MAANA HILI JAMBOLIMEZIDIShirikisho la mpira wa miguu duniani FIFA limeiondoa klabu ...
22/03/2025

SASA NI MUDA WA FIFA KUJA BONGO NAPO MAANA HILI JAMBO
LIMEZIDI

Shirikisho la mpira wa miguu duniani FIFA limeiondoa klabu ya León ya Mexico
kwenye mashindano ya klabu bingwa dunia klabu ambayo ilikuwa icheze na
klabu ya Chelsea kwenye hatua za mwanzo ya mashindano hayo.

Klabu hiyo ambayo anaichezea mchezaji wa zamani wa Real Madrid na Bayern
Munich James Rodríguez imeondolewa kutokana na kukiuka moja sheria za
mashindano hayo ambayo hayaruhusu vilabu viwili vinavyomilikiwa na
mmiliki mmoja hata kwa share ndogo tu kushiriki kwa pamoja kwenye
mashindano hayo.

Klabu ya León na klabu ya Pachuca zote zinamilikiwa na kampuni ya Grupo
Pachuca na kwa sasa FIFA inaangalia ni klabu ipi kulingana sheria za
mashindano hayo itachukua nafasi ya klabu ya Lean na itakapopatikana basi
itatangazwa rasmi.

TFF YATOZWA FAINI MILIONI 27Shirikisho la Soka Afrika CAF limetoa taarifa rasmi juu ya kumfungia kocha wa Taifa Stars Ad...
20/01/2024

TFF YATOZWA FAINI MILIONI 27

Shirikisho la Soka Afrika CAF limetoa taarifa rasmi juu ya kumfungia kocha wa Taifa Stars Adel Amrouche na kuitoza faini Tanzania (TFF) dola za kimarekani 10,000 (Ths 27,000,000/=)

CAF katika taarifa yao wanasema Amrouche amekutwa na hatia kwa kukiuka vifungu vya kanuni za nidhamu namba 82, 83, 84 na 131.

Amrouche ambaye ameonyesha nia ya kukata rufaa bado yupo na Stars huko Ivory Coast ingawa tayari TFF wamemsimamisha kazi na majukumu yake wamepewa wazawa Hemedi Morocco na Juma Mgunda.

Address

Dar Es Salaam

Opening Hours

09:00 - 17:00

Telephone

+255656831913

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when seeker.tz posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to seeker.tz:

Share

Category