UMG Digital

UMG Digital Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from UMG Digital, Media/News Company, Kariakoo, Dar es Salaam.

Bunge la Jamhuri ya Zimbabwe limepitisha hatua yake ya kwanza ya usomaji bungeni kwa muswada tata ambao unaweza kuongeza...
03/06/2026

Bunge la Jamhuri ya Zimbabwe limepitisha hatua yake ya kwanza ya usomaji bungeni kwa muswada tata ambao unaweza kuongeza muda wa muhula wa Urais na Ubunge kutoka miaka mitano hadi saba katika sheria inayolenga kurekebisha katiba Pia muswada huo unalenga kubadilisha mfumo wa uchaguzi wa rais, ambapo badala ya kura ya moja kwa moja ya wananchi, bunge litakuwa na mamlaka ya kumchagua kiongozi wa nchi ambapo Ibara zenye utata zaidi zinapendekeza kuruhusu Rais Mnangagwa na wabunge kusalia ofisini hadi 2030 Marekebisho yaliyopendekezwa yamesababisha ghadhabu kwa wananchi na yanakabiliwa na changamoto kadhaa za kisheria. Wakosoaji wakiwemo Chama cha Wanasheria nchini humo wanasema mapendekezo hayo yanadhoofisha taasisi za kidemokrasia na kulimbikiza madaraka kwa rais. Makanisa makubwa na mashirika ya haki za binadamu wanasema mabadiliko hayo ni kinyume na katiba na yanahitaji kura ya maoni. Muswada huo Utasomwa mara ya pili Jumatano wakati wabunge watakapojadili uhalali wa marekebisho zaidi ya kumi na utahitaji angalau theluthi mbili ya kura katika Mabunge yote mawili ili kupitishwa. ‎

UTEUZI.
03/06/2026

UTEUZI.

SERIKALI imeendelea kuimarisha mifumo ya uratibu, kujiandaa na kukabiliana na maafa ili kuhakikisha misaada ya kibinadam...
02/06/2026

SERIKALI imeendelea kuimarisha mifumo ya uratibu, kujiandaa na kukabiliana na maafa ili kuhakikisha misaada ya kibinadamu inayotolewa inawafikia walengwa kwa wakati, ufanisi na kwa kuzingatia viwango vya kimataifa.

Hayo yameelezwa leo tarehe 02 Juni, 2026 na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Usimamizi wa Maafa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu), Kanali Selestine Masalamado, wakati wa ufunguzi wa warsha ya zoezi la uigaji la uratibu wa utoaji wa misaada ya kibinadamu na usafirishaji wakati wa dharura, mkoani Morogoro.

Amesema utoaji wa misaada ya kibinadamu na usafirishaji wa dharura ni nguzo muhimu zinazowezesha kuokoa maisha ya wananchi walioathiriwa na maafa, kupunguza mateso ya waathirika na kuharakisha urejeshaji wa hali za kawaida katika maeneo yaliyoathirika.

“Kwa kutambua umuhimu huo, Serikali imeendelea kuimarisha mifumo ya uratibu, kujiandaa na kukabiliana na maafa kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ili kuhakikisha misaada inawafikia walengwa kwa wakati, ufanisi na kwa kuzingatia viwango vya kimataifa vya utoaji wa huduma za kibinadamu,” amesema.

Vilevile, amelishukuru Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP), washirika wote waliohusika katika utekelezaji wa Mradi wa Field-Based Preparedness Project (FBPP), ambapo katika kipindi cha miaka miwili iliyopita, mradi huo umechangia kwa kiasi kikubwa kuimarisha uwezo wa taifa katika sekta ya utoaji wa misaada ya kibinadamu na usafirishaji.

Amesema Tanzania imefanikiwa kuanzisha Kikosi Kazi cha Kitaifa cha Uratibu wa utoaji wa misaada ya kibinadamu na usafirishaji wa dharura mwezi Julai 2025, ambacho kimekuwa jukwaa muhimu la uratibu na ushirikiano baina ya taasisi za serikali na wadau wa kibinadamu.

“Zoezi hili la uigaji limeandaliwa k**a jukwaa la kitaifa la kujifunza, kupima na kuboresha mifumo yetu ya uratibu wa shughuli za usafirishaji na utoaji wa misaada ya kibinadamu.”alieleza.

Dodoma 2 Juni, 2026: Serikali kupitia Wizara ya Fedha imeliomba Bunge kuidhinisha jumla ya shilingi trilioni 21.3 kwa aj...
02/06/2026

Dodoma 2 Juni, 2026: Serikali kupitia Wizara ya Fedha imeliomba Bunge kuidhinisha jumla ya shilingi trilioni 21.3 kwa ajili ya utekelezaji wa majukumu ya Wizara hiyo pamoja na taasisi zake kwa Mwaka wa Fedha 2026/27. Akiwasilisha Mapendekezo ya Mpango na Bajeti bungeni, Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis M***a Omar (Mb), alisema fedha hizo zitatumika kugharamia matumizi ya kawaida na maendeleo katika mafungu manane ya Wizara, ambapo kati ya fedha hizo, shilingi trilioni 19.4 zitatumika kwa matumizi ya kawaida huku shilingi trilioni 1.8 zikielekezwa kwenye miradi ya maendeleo. Alisema kuwa katika Bajeti hiyo, Serikali imepanga kuendelea kusimamia uchumi kwa weledi ili kuhakikisha ukuaji wa uchumi unafikia asilimia 6.3 mwaka 2026 huku mfumuko wa bei ukidhibitiwa kubaki katika katika wigo wa wastani wa asilimia 3 hadi 5. “Serikali pia inalenga kuimarisha nidhamu ya matumizi ya fedha za umma pamoja na kuongeza ufanisi wa ukusanyaji wa mapato ya ndani” alisema Mhe. Balozi Omar. Aidha, alibainisha kuwa Wizara imepanga kutenga shilingi bilioni 100 kila mwezi kwa ajili ya kulipa madeni ya watumishi, wakandarasi, wazabuni na watoa huduma ili kupunguza changamoto za malimbikizo ya madeni serikalini. Kwa upande wa mapato, alisema kuwa Wizara ya Fedha imekadiriwa kukusanya jumla ya shilingi trilioni 55.2, ambapo Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) inatarajiwa kukusanya zaidi ya shilingi trilioni 39. Katika hatua nyingine, aliliomba Bunge kuiidhinishiwa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi shilingi bilioni 132.2 kwa ajili ya kuimarisha shughuli za ukaguzi wa matumizi ya fedha za umma pamoja na kuendelea na ujenzi wa ofisi zake katika baadhi ya mikoa nchini. Mhe. Balozi Omar alieleza kuwa bajeti hiyo imeandaliwa kwa kuzingatia Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, Mpango wa Nne wa Maendeleo wa Taifa pamoja na Ilani ya CCM ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.

02/06/2026

Wambura, amewataka watendaji wa Kamisheni ya Uchunguzi wa Sayansi ya Jinai kuendelea kujiimarisha kitaaluma na kutumia teknolojia za kisasa katika kukabiliana na uhalifu unaozidi kutumia mbinu za hali ya juu. ‎ ‎ IGP Wambura amesema maendeleo ya sayansi na teknolojia yamebadilisha mazingira ya utendaji wa uhalifu, hivyo kuna umuhimu wa kuwa na wataalamu wenye uwezo wa kutumia mbinu za kisasa katika ukusanyaji na uchambuzi wa ushahidi ili kusaidia upatikanaji wa haki. ‎ ‎IGP Wambura amewapongeza pia watendaji wa Kamisheni hiyo kwa kazi wanayoifanya ya kufika katika maeneo ya matukio, kukusanya ushahidi na kusaidia uchunguzi wa kisayansi, akisisitiza kuwa hakuna uhalifu unaoweza kutendeka bila kuacha ushahidi unaoweza kusaidia kuwabaini wahalifu, hivyo amewataka watendaji hao kuzingatia weledi, uadilifu na kuendelea kujifunza ili kuimarisha utendaji kazi na kuongeza imani ya wananchi kwa mfumo wa haki jinai. ‎ ‎Aidha, katika hotuba yake amesema Jeshi la Polisi linaendelea kuwekeza katika mafunzo na teknolojia za kisasa ikiwemo uchunguzi wa vinasaba (DNA), uchambuzi wa kidigitali na mbinu nyingine za kisayansi, akisema uwekezaji huo unalenga kuifanya Kamisheni hiyo kuwa mhimili imara katika mapambano dhidi ya uhalifu wa kimtandao, uhalifu wa kimataifa na makosa mengine yanayohitaji uchunguzi wa kisasa unaozingatia ushahidi wa kisayansi.

02/06/2026

Msemaji wa timu za Taifa za soka, Haji Manara, amesema msafara ulioelekea Morocco una malengo mawili makuu ya kushangilia na kurejea nyumbani pamoja na mashujaa ambao ni timu ya Taifa ya vijana chini ya miaka 17 (Serengeti Boys). Akizungumza akiwa safarini kuelekea Morocco, Manara amesema hawajaenda kwa jambo lingine bali kushuhudia ushindi wa vijana hao katika fainali ya michuano ya AFCON U-17 dhidi ya Senegal. Ameongeza kuwa Rais Samia Suluhu Hassan ametoa ndege maalumu kufanikisha safari hiyo ya mashabiki na wadau wa soka, ikiwa ni sehemu ya kuonyesha kuiunga mkono Serengeti Boys. Fainali hiyo inatarajiwa kuchezwa leo, Juni 2, 2026, saa 4:00 usiku kwa saa za Afrika Mashariki.

01/06/2026

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM-TAMISEMI) Mhe. Prof. Riziki Shemdoe amesema jumla ya wanafunzi 246,197 wakiwemo wasichana 114,102 na wavulana 132,095 waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano mwaka 2026 wanatakiwa kuripoti shuleni kuanzia Julai 04, 2026 hadi Julai 31, 2026 kwakuwa muhula wa kwanza wa masomo utaanza Julai 06, 2026. Prof. Shemdoe amesema hayo leo Juni 01, 2026 katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi Ndogo ya Ofisi ya Waziri Mkuu-TAMISEMI Magogoni Jijini Dar es Salaam, wakati akitoa taarifa kwa umma kuhusu wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano na vyuo vya elimu ya ufundi kwa mwaka 2026. “Wanafunzi 172,114 sawa na asilimia 69.9 wakiwemo wasichana 85,987 na wavulana 86,127 wenye sifa wamechaguliwa kujiunga na kidato cha tano katika shule za sekondari za Serikali 856 zikiwemo shule za bweni 825, kutwa 25 na kutwa na bweni sita (06),” amefafanua Prof. Shemdoe. Aidha, Prof. Shemdoe amesema jumla ya wanafunzi 74,083 sawa na asilimia 30.1 wakiwemo wasichana 28,115 na wavulana 45,968 wamechaguliwa kujiunga na vyuo vya Ufundi. “Wanafunzi 3,144 wakiwemo wasichana 1,170 na wavulana 1,974 wamechaguliwa kujiunga na fani mbalimbali katika vyuo 04 vya elimu ya ufundi, vyuo hivyo ni Chuo cha Ufundi cha Arusha (ATC), Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT), Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST) na Chuo cha Maendeleo ya Maji (WMDI),” ameeleza Prof. Shemdoe. Prof. Shemdoe amesisitiza kwamba, uchaguzi wa wanafunzi wa kujiunga na kidato cha tano na vyuo vya elimu ya ufundi umefanyika kwa kuzingatia ufaulu na nafasi zilizopo katika shule; hivyo, hakutakuwa na fursa ya kufanya mabadiliko yoyote ya Shule kutokana na ukosefu wa nafasi. Sanjari na hilo, Prof. Shemdoe ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha nyingi zilizotumika kujenga miundombinu bora ya shule za kidato cha tano na vyuo vya kati ambayo itatumika kuwahudumia wanafunzi 246,197 waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano na vyuo vya elimu ya ufundi mwaka 2026.

01/06/2026

Serikali inaendelea na utekelezaji wa mpango wa ushirikiano kati ya vyuo na viwanda, unaolenga kuongeza ujuzi kwa vijana walioko vyuoni na wanaomaliza masomo katika vyuo mbalimbali nchini. Lengo ni kuwawezesha vijana kupata nafasi za kufanya mazoezi ya vitendo na kutumia maarifa waliyojifunza darasani katika mazingira halisi ya kazi. Mpango huu unasaidia kujenga ujuzi wa kivitendo na fursa ya kufanya ubunifu ambao unahitajika katika soko kwani waajiri wengi huitaji kuajiri wafanyakazi wenye uzoefu. Kupitia ushirikiano huo, Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya kimeingia mikataba na taasisi mbalimbali, na kupeleka walimu pamoja na wanafunzi kujifunza teknolojia za kisasa na kupata uzoefu wa moja kwa moja viwandani. Ujuzi wa vitendo unaopatikana kupitia mpango huu unawawezesha vijana kuwa wabunifu katika kutatua changamoto zinazokabili jamii, hususan katika sekta za ujenzi, kilimo, afya, biashara, na elimu.

01/06/2026

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Dk. Dorothy Gwajima (Mb), amesema jumla ya wazazi 469, 634 wamepatiwa elimu ya malezi kuhakikisha wanalea Watoto katika maadili na matunzo ndani ya familia. Dk. Gwajima ameyasema hayo leo Juni 1, 2026, Bungeni jijini Dodoma wakati akiwasilisha Hotuba ya Mapitio ya Utekelezaji wa Mpango na Bajeti ya Wizara kwa mwaka wa fedha 2025/2026 pamoja na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka wa fedha 2026/2027.

01/06/2026

Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Bw. Sixtus Mapunda, ameagiza kila kaya wilayani humo kuhakikisha inapanda miti mitano katika maeneo yao ili kukabiliana na uharibifu wa mazingira. Bw. Mapunda amesisitiza kuwa uongozi wa wilaya unatarajia kuanza operesheni maalum ya kaya kwa kaya ili kuwabaini wote watakaoshindwa kutekeleza agizo hilo. Ameweka wazi kuwa wananchi watakaokaidi agizo hilo watachukuliwa hatua kali za kisheria na kushughulikiwa k**a wahalifu wengine wowote. Kiongozi huyo ameyasema hayo wilayani Temeke mkoani Dar es Salaam wakati akishiriki zoezi la upandaji wa miti 500. Alifafanua kuwa zoezi hilo limefanyika kwa lengo la kuhimiza utunzaji endelevu wa mazingira pamoja na kupunguza athari za hewa ya ukaa nchini. Hatua hiyo inalenga kuigeuza Temeke kuwa ya kijani na kuhamasisha jamii kuwa mstari wa mbele katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi. Zoezi hilo limeungwa mkono na wadau mbalimbali wa utunzaji mazingira, akiwemo Bw. Amir Mpungwe, na Diwani wa Kata ya Kurasini, Bw. Selestine Nyakunga, ambao wameeleza umuhimu mkubwa wa upandaji miti na kudumisha usafi. Naye mkazi wa Temeke, Bi. Consolata Kabuhaya, amepongeza hatua hiyo na kueleza utayari wa wananchi katika kushirikiana na serikali kufanikisha kampeni hiyo ili kuboresha afya na mandhari ya wilaya yao.

Address

Kariakoo
Dar Es Salaam

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when UMG Digital posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to UMG Digital:

Share