05/08/2025
KWANINI WAZAZI WAKO WANALIA?
Mwanaume unaweza kuwa na pesa lakini tabia yako ikabadilika.
Badala ya kujali wazazi wako ukajali LUKU, vocha, nywele, kucha, wigi na pochi ya wanawake tena ambao umewapanga k**a matenga ya nyanyaπ
Badala ya kujali binti yako na kijana wako mdogo wanaosoma shule za kayumba wewe unawaacha kwa bibi yao kisa umeachana na mama yao kisa malaya wa pembeni.
Wanao wawili ni wadogo wanaugua wanavaa nguo zenye ukosi mchafu, sox za pundamilia zilizochafuka na viatu vilivyotoboka wewe upo mjini unaketi Bar na wanawake wazinifuπ₯²π₯΅
Mama wa wanao ameenda kwao anauza mbogamboga umemsababishia maumivu na kumtelekeza k**a vile pia hana haki na watoto aliobeba miezi tisa tumboni mwake.
Wazazi wako wanateseka na wanao utadhani wao ndio waliwazaa umeenda kuwasukumia hapo hata pesa huwatumii ya kulea wanao wanauza mazao yao wanauza mifugo yao kulea wajukuu wewe unaponda raha na marafiki walevi wavuta bangi na wanaoona FAHARI KUNUNUA MALAYAπ₯²π
Mungu amekujalia chanel unapata pesa unapata watu lakini wewe unaona wale watu k**a wapo tu siku zote na utapata pesa muda wote hivyo utahudumia wazazi na wanao tu kumbe unajidanganya.
Umri na muda unaenda inakuja siku huna tena nguvu mwanao wa k**e amepewa ujauzito kule kijijini amezalia tena pale kwa wazazi wako na amewaongezea mzigo na wewe huna tena nguvu umechoka na UKIMWI ulioupata mjini kwa ufahari wa kipumbavu umechoka na michepuko yenye sugu za UTI, umeanza kupoteza nguvu na figo hazifanyi kazi tena shauri ya pombe.
Mapafu yameharibika vibaya kwa moshi wa bangi, sigara na sh**ha ulizokuwa unavuta kwa masifa na mawenge, yale magari umeuza sasa umebaki kwenye kijumba cha ajabu ulichobahatika kujenga na hata saa ingine hujajenga.
ONE MAN DOWNπ
Mwanao wa kiume ni mwizi na ni mvuta bangi sasa k**a ungewekeza kwake huenda mwamba angekuokoa ni yeye sasa ananyanyua matairi ya pikipiki huku unasikia amegongwa na semi akapasuka kichwa na wewe unakufa na presha na kisukari hapo wazee wako kule kijijini Mungu alivyo wa pekee kwa namna walijitoa Mungu amezidi kuwapa neema nao wanakuja wakilia kukuzika bado wapo imara maana walifanyika Sadaka kukulea wewe na wanao ukiwa mwanaume mpumbafu usiyejielewa.
Ikawe siku ya ukombozi wako leo unaposoma ujumbe wangu huu MWANAUME Jitambue leo tusonge mbele acha tabia ambazo sio rafiki kwa uchumi wako, familia yako na wazazi wako leoππ½π₯π₯
Follow me ππ’π ππ¬π