
05/09/2025
: Hali ya mshangao mkubwa imeibuka nchini Brazil baada ya bilionea kijana mwenye umri wa miaka 31 kutoka jimbo la Rio Grande do Sul kuacha urithi wake wote kwa nyota wa soka Neymar Jr, licha ya wawili hao kutokuwahi kukutana maishani.
Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya kimataifa, tajiri huyo aliyekuwa hana mke wala watoto, aliandikisha wosia wake rasmi mwezi Juni 2025 katika ofisi ya serikali, akishuhudiwa na mashahidi.
Katika wasia Huo, alitamka wazi kuwa mali zake zote ikiwemo majumba, kampuni na uwekezaji ambazo zinakadiriwa kufikia zaidi ya dola bilioni 1 (sawa na zaidi ya shilingi trilioni 2.5 za Kitanzania) ziende kwa Neymar pekee.
Sababu kubwa iliyompelekea kufanya uamuzi huo ni kuvutiwa na
unyenyekevu wa Neymar na ukaribu wake na baba yake, akidai kuwa aliona thamani na utu katika tabia ya nyota huyo wa Brazil.
Kwa sasa, urithi huo mkubwa unasubiri uthibitisho wa kisheria katika mahak**a za Brazil kabla ya kuhamishwa rasmi kwa Neymar.