22/08/2026
Jana tulipata heshima kubwa ya kushiriki katika Mashariki Creative Economy Expo ’26, ambapo banda letu lilipata nafasi ya kutembelewa na Naibu Waziri wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Mheshimiwa Dennis Lazaro Londo.
Katika ziara hiyo, Mheshimiwa Naibu Waziri alipata fursa ya kujionea bidhaa zetu, hususan kazi mbalimbali za fasihi za Kiswahili zinazochapishwa na kusambazwa kwa lengo la kukuza lugha, maarifa, utamaduni na ubunifu wa Watanzania.
Vitabu hivi si bidhaa tu, bali ni hazina ya maarifa, utamaduni na urithi wa jamii. Kupitia riwaya, tamthiliya, mashairi na kazi nyingine za kifasihi, tunaendeleza matumizi ya Kiswahili, tunawapa nafasi waandishi na wabunifu, na kuhakikisha simulizi za jamii yetu zinaendelea kusomwa na vizazi vya sasa na vijavyo.